Habari zilizozagaa kwa wananchi na makada wa CCM walio wengi na baadhi ya Wajumbe wengi wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ni kwamba Katibu Mkuu wanaomtaka baada ya kazi nzuri ya Dkt Emmanuel Nchimbi ni lazima awe sifa hizi zifuatazo au zaidi,
1. Anatafutwa Katibu Mkuu wa CCM hasa wa kupambana na Upinzani kwa hoja lakini mwenye weledi wa kutosha wa kuiongoza CCM kama chama dola kuelekea Oct 2025.
2. Anatafutwa Katibu Mkuu wa CCM asiye na makundi kwenye chama na mwenye historia ya kujenga hoja hasa anayetumia takwimu ( Political numbers ) lakini mwenye historia ya kueleweka na kukubalika Umma wa Watanzania wote bila kujali tofauti zao za kiitikadi, kiimani na hata kimichezo.
3. Anatafutwa Katibu Mkuu wa CCM anayeweza kufafanua vizuri mambo ya fedha na Uchumi na kueleweka kwa kuzingatia Chama Kikuu Cha Upinzani Tanzania Cha CHADEMA kimeteua viongozi wake wapya wenye hoja hasa za Kiuchumi na kifedha hivyo lazima tuwe na Katibu Mkuu atakayewajibu Wapinzani kwa Kadiri na namna watakavyokuja na hiyo ndio maana halisi ya siasa.
4. Anatafutwa Katibu Mkuu wa CCM anayeweza kutawala majukwaa mbalimbali pamoja Social media (mitandao ya kijamii) kwakuwa ndio hasa Upinzani wanatumia njia hiyo kujiimarisha kwa kwa sasa kwa mujibu wa TCRA Kuna zaidi ya Watanzania 40mil wanatumia mitandao ya kijamii hivyo CCM lazima iwekeze siasa zake zaidi huku kwa sasa kwani ndio kuna watu wengi na gharama ni nafuu.
Majina yanayotajwa tajwa zaidi huku mitaani kwa sasa ni haya matatu.
1. Cde Dkt Harrison Mwakyembe
View attachment 3345010
2. Cde Shaka Hamdu Shaka
View attachment 3345012
Pre GE2025 - PICHA: Ona Mapokezi kabambe ya Cde CPA Amos Makalla Kilosa kwa Mwenezi Mstaafu Cde Shaka Hamdu Shaka
3. Cde David Zachari Kafulila
View attachment 3345017
David Kafulila: Huyu Tundu Lissu ni muongo