PICHA: Je Unaikumbuka Jambo Forums? Ulikuwa Wapi enzi hizo?

PICHA: Je Unaikumbuka Jambo Forums? Ulikuwa Wapi enzi hizo?

2006 mbali
Hahaaa ni mbali lakini si mbali kivile.

Ila idea ya kwamba tuna members humu ambao bado walikuwa wananyonya pacifier hiyo 2006, kwangu inachekesha. Si kwa ubaya lakini.

Halafu leo hii hao hao ndo ma baddies wa JF kwa sasa 🤣.

2006 nipo JF navurugana na akina Bi.Senti 50, Mwafrika wa Kike……huku nikimfukizia Nancy Swai [huyu mrembo wangu sijui alipoyeleaga wapi tu].
 
Huko India, sehemu zote huwa zina harufu ya curry? Hata ukiwa barabarani harufu ya curry ipo?

Kwenye vyombo vya usafiri je? Na kwenyewe kumejaa harufu ya curry?

Bro kama unaona Wahindi wananuka (samahani kwa Wahindi), basi haujakutana na Wachina na nchi yao (samahani kwa Wachina)
 
Bro kama unaona Wahindi wananuka (samahani kwa Wahindi), basi haujakutana na Wachina na nchi yao (samahani kwa Wachina)
Hahahaa najua Wachina nao personal hygiene ni changamoto.

Ila vikwapa vya Wahindi ni level nyingine kabisa.

Ile curry wanayowekaga kwenye misosi yao ni lazima itoke nwilini kwa namna moja ama nyingine.

Na mara nyingi huwa inatoka na jasho la mtu.

Halafu wenyewe wala huwaga hawana habari kabisa…..pua zao zimeshazoea.
 
Kitambo kidogo japo sio mbali sana, nimeanza matumizi ya internet 2004 enzi hizo nikiwa kidato cha pili, Nakumbuka kuna tovuti ya kusikiliza bongofleva ilikuwa inaitwa mzibo.com sijui kama bado inafanya kazi kwa sasa.

Jamiiforums nimeanza kuiona 2007 baada ya familia kuanzisha biashara ya internet cafe & stationary, Enzi hizo unanunua bando la Gb 8 kwa Tzs 220,000 kutoka TTCL broadband.

Kuna mzee alikuwa anakuja internet na muda mwingi sana alikuwa anasoma vitu Jamiiforums, nadhani ugonjwa ule alimuambukiza na Baba na ukaamia kwangu taratibu sana, kabla ya Jamiiforums nilikuwa member wa marafiki.com sijui kama hii wavuti nayo bado inafanya kazi au ilishajifia.

Nilijiunga Jamiiforums 2009 nadhan octoba ila sikujua jinsi ya kutumia vizuri hizi forums so ikawa ni sehemu yangu ya kusoma tu huku nikitumia kujuana na watu facebook zaidi ambayo nilijiunga 2008.

Uchanguzi wa 2010 ndio nilianza rasmi kuwa mtumiaji wa Jamiiforums na Jamiiforums ikawa ndio chanzo changu rasmi cha taarifa na maarifa na mpaka sasa nimeshakuwa addicted na hii site.

Nilikuwa sipendi kusoma ila Jamiiforums imenifanya nipende sana kusoma hasa kwa makala za Mshana, The Bold, Kiranga,Mzee Mwanakijiji, Nyani ngabu n.k

Nakumbuka kashfa za richmond, kagoda n.k jinsi zilivyokua za moto kwa mijadala ya hapa Jamiiforums.

Maujuzi mengi sana nimeyapata hapa, kuna kipindi wakati hizi android phone zinaanza kutoka basi kwa madini niliopata hapa nikawa nalia ujiko kazini, Yaani enzi hizo hata mtu kufanya setting za internet kwenye blackberry au zile huawei hajui.

Long live Jamiiforums, wish mpaka wajukuu zangu waje watumie huu mtandao, Kongole kwa Maxence, Mike na Le mutuz wanahisa wa kwanza kabisa kuwekeza muda na fedha zao kuendesha huu mtandao.
 
Back
Top Bottom