Mkuu
DR Mambo Jambo umekumbusha vitu vingi sana aisee ni kweli huu mtandao tuna kila sababu ya kujivunia cha nyumbani 😀😀😀
Mijadala ya nyakati zile ilikuwa ni moto kweli na enzi nilikuwa sijapevuka vya kutosha miaka 23,24 hivi. Nakumbuka kuna kigogo mmoja wa kuitwa
Barubaru aisee huyu ni mtu mzito sana hauwezi kudhania nilikuwa namchokonoa na hoja mbovu mbovu mimi na Baba Mchungaji
Masanilo.
Kuna siku akajitambulisha yeye ni Dr wa Uchumi na Fedha na anafanya kazi Gulf Oils huko duniani akatoa na contacts zake za Tanzania na kwao ni Zanzibar, Mimi nilikuwa kule nikapiga zile namba na alipokea Mpambe wake akanipa direction alipo aisee nikaenda pale Serena Hotel nilikutana na Makomandoo wa JWTZ wanapalinda na alikuwa na kikao na Mheshimiwa mkubwa sana wa Serikali. Aisee mbona nilikimbia 🤣🤣🤣
Kuanzia siku ile nikajifunza adabu humu mitandaoni sio pakuchukulia poa.