Kitambo kidogo japo sio mbali sana, nimeanza matumizi ya internet 2004 enzi hizo nikiwa kidato cha pili, Nakumbuka kuna tovuti ya kusikiliza bongofleva ilikuwa inaitwa mzibo.com sijui kama bado inafanya kazi kwa sasa.
Jamiiforums nimeanza kuiona 2007 baada ya familia kuanzisha biashara ya internet cafe & stationary, Enzi hizo unanunua bando la Gb 8 kwa Tzs 220,000 kutoka TTCL broadband.
Kuna mzee alikuwa anakuja internet na muda mwingi sana alikuwa anasoma vitu Jamiiforums, nadhani ugonjwa ule alimuambukiza na Baba na ukaamia kwangu taratibu sana, kabla ya Jamiiforums nilikuwa member wa marafiki.com sijui kama hii wavuti nayo bado inafanya kazi au ilishajifia.
Nilijiunga Jamiiforums 2009 nadhan octoba ila sikujua jinsi ya kutumia vizuri hizi forums so ikawa ni sehemu yangu ya kusoma tu huku nikitumia kujuana na watu facebook zaidi ambayo nilijiunga 2008.
Uchanguzi wa 2010 ndio nilianza rasmi kuwa mtumiaji wa Jamiiforums na Jamiiforums ikawa ndio chanzo changu rasmi cha taarifa na maarifa na mpaka sasa nimeshakuwa addicted na hii site.
Nilikuwa sipendi kusoma ila Jamiiforums imenifanya nipende sana kusoma hasa kwa makala za Mshana, The Bold, Kiranga,Mzee Mwanakijiji, Nyani ngabu n.k
Nakumbuka kashfa za richmond, kagoda n.k jinsi zilivyokua za moto kwa mijadala ya hapa Jamiiforums.
Maujuzi mengi sana nimeyapata hapa, kuna kipindi wakati hizi android phone zinaanza kutoka basi kwa madini niliopata hapa nikawa nalia ujiko kazini, Yaani enzi hizo hata mtu kufanya setting za internet kwenye blackberry au zile huawei hajui.
Long live Jamiiforums, wish mpaka wajukuu zangu waje watumie huu mtandao, Kongole kwa Maxence, Mike na Le mutuz wanahisa wa kwanza kabisa kuwekeza muda na fedha zao kuendesha huu mtandao.