Picha: Kajala na utajiri wa kutisha

Picha: Kajala na utajiri wa kutisha

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
AMA kweli fedha mwanaharamu ! Kama bado ulikuwa ukiamini kwamba Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu anayependelea kuitwa Madam ana mtonyo ( fedha) kumzidi aliyekuwa shosti wake, mwigizaji Kajala Masanja ' Kay ' , umekosea sana kwani upepo umegeuka.

Habari za ' ufukunyuku ' zinadai kwamba, kwa utajiri alionao kwa sasa , Kajala anaweza kudiriki kumwajiri Wema kama kisemavyo chanzo.

TUJIUNGE NA CHANZO

Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na wote kwa maana ya kutafuna pande zote , mwigizaji huyo ambaye enzi za ushosti wake na Wema alikuwa akionekana kama kijakazi, sasa fedha imemtembelea kiasi cha kutosha wakati mwenzake kwa bahati mbaya eti ' anatembelea ringi ' .

Chanzo kilisema kwamba Kajala kwa sasa ana maisha ya ' kitonga ' , amepanga kwenye nyumba nzuri ya ghorofa , ana kampuni yake ya filamu ( KAY Entertainment ) , magari manne, anatembea na wapambe ( walinzi) huku akaunti yake benki ikiwa imetuna.

"Kajala ameonesha jeuri ya fedha . Ametoka katika nyumba ya kawaida sasa analala angani. Kwa taarifa yenu amepanga ghorofa nzima maeneo ya Sinza -Madukani jijini Dar .

"Yupo vizuri, anamiliki ofisi kubwa ya kuzalisha sinema, magari mawili ya ofisi pamoja na magari mawili ya kutembelea ( Brevis na Harrier ) na anaishi katika nyumba anayolipa kodi kwa mwezi dola 2, 000 ( zaidi ya Sh . milioni 3.2 ) ," kilidai chanzo hicho na kudai kwamba si mbaya Kajala akamkumbuka mwenzake hata kwa kumwajiri kwenye kampuni yake . Pichani ni mjengo ambao Kajala Masanja amepanga .

KAJALA AMEHONGWA ?

Akizungumza na waandishi wetu , Kajala alisema anamshukuru Mungu kwani fedha hizo amezizalisha kupitia kazi zake pamoja na biashara mbalimbali alizokuwa akizifanya ,hajahongwa na mtu yeyote .

"Sijahongwa na mtu yeyote , kila mtu ana akili zake katika kutafuta fedha , nafanya biashara huku nikiigiza sinema zangu na Mungu amenijalia mambo yanakwenda vizuri, " alisema Kajala .

Kuhusu kumwajiri staa mwezake huyo, Kajala hakutaka kulizungumzia hilo.

WEMA HALI IPOJE ?
Utafiti umeonesha Wema ambaye alikuwa akimiliki magari kadhaa likiwemo la kufanyia kazi za sinema, kwa sasa amebakiwa na gari moja tu ambalo ni Toyota Harrier . Kama hiyo haitoshi , ilidaiwa kuwa hata akaunti benki haijanona na hata wapambe wa kutembea naye wameyeyuka.

Utafiti uliofanywa na Ijumaa Wikienda umebaini kwamba Wema aliyemlipia Kajala Sh . milioni 13 asiende jela mwaka jana,ambaye kipindi kifupi kilichopita alikuwa na kampuni ya kuzalisha sinema, wapambe,akaunti iliyonona benki , magari ya kifahari ya kutembelea na samani nyingine , nyingi zimepotea kama si kuyeyuka kabisa .

WEMA ATAFUTWA

Ili kutaka kujua anazungumziaje ' challenge 'hiyo ya kudaiwa kuporomoka kiuchumi,wanahabari wetu walimtafuta Wema kwa siku tatu mfululizo lakini hakupatikana huku simu yake ikiita muda mrefu bila kupokelewa.
 

Attachments

  • 1409549899071.jpg
    1409549899071.jpg
    37.7 KB · Views: 3,030
Hivi lasaba mmemaliza mtihani wa Taifa?
Huku hakuta kalika,ina maana badala ya kufuatilia form za kujiunga form one unamfuatilia kajala!

shame upon you
 
Teh teh teh nyumba iko Sinza Mugabe na hajapanga ghorofa nzima ye kapanga juu na chini anakaa mtu mwingine anaitwa Tamimu. Nyuma ya hiyo ghorofa kuna nyumba nyingine ndogo imepangishwa kifupi ni Apartments


Sent from my iPad Air using JamiiForums
 
Heheheheh ni cheke mie niongeze siku hii habari hata hisisimui tajiri kapanga ndo nini sasa
Haya yetu macho
 
kajala msukuma wa mwanza
wema mnyamwezi(wanawake wa kinyamwezi) wapo km wanawake wa pwani
KAY ana mtoto lazima akili ichangamke
 
ama kwa hakika ma staa wa bongo wana hela sana
 
Duh! Yaani miezi kadhaa tu iliyopita ilibidi alipiwe faini ili asiende jela, leo hii mara ameshakuwa tajiri wa kutupwa!!!
 
Duh! Yaani miezi kadhaa tu iliyopita ilibidi alipiwe faini ili asiende jela, leo hii mara ameshakuwa tajiri wa kutupwa!!!
Ndio hapo sasa Nimebaki mdomo wazi kwa mshangao.
 
Hivi lasaba mmemaliza mtihani wa Taifa?
Huku hakuta kalika,ina maana badala ya kufuatilia form za kujiunga form one unamfuatilia kajala!

shame upon you

Tuwaulize nyie chekechea mshaanza la kwanza? Maana kazi umbea tu hasubuh hasubuh mwenzenu nalipwa apa sijui wewe mwenzangu unayehangaika na umbea hasubh yote hii
 
Maisha yake kufanyaje binamu? Kuwa billionea au kuandikwa kwenye magazeti?

Maamuzi yake kujielezea kwetu juu ya namna kapata hela alizonazo. .maisha yake..anaamua aseme au.asiseme nini?
 
Back
Top Bottom