Picha: Kama umenunua Kiwanja, nyumba au Pagale ndani ya Jiji la Mwanza, ni zaidi ya 98% utakuwa umetapeliwa na huyu mtu

Huyu Bwana alimuuzia rafiki yangu kiwanja Nyamohongolo kule Majengo mapya karibu na kanisa la Eagt Kaguha
 
Huyu Bwana alimuuzia rafiki yangu kiwanja Nyamohongolo kule Majengo mapya karibu na kanisa la Eagt Kaguha
Alishapata haki yake. Kama hajapata tutafutane.

Huyu mtu au wafanyakazi wake wanauza viwanja mji mzima, kuanzia Kisesa mpaka Nyangomango, Buswelu Ilemela mpaka mpaka Nyamhongolo.

Wanashirikiana na Mzee mmoja ana vijana wake wanapenda kumuita Dokta.
 
Eneo tulinunua na tumepata hadi hati ila mwenye eneo halisi ndio ana kesi na huyo jamaa ila sisi tulishapata kiwanja chetu
 
Unamfahamu huyu mtu?

Maana mama yake nimewahi kukutana naye.

Huyo jamaa hata ukimwazima gari, akipata mteja barabarani analiuza.
Namfahamu vizuri, ndugu zake walijichanga wakamjengea mama yao nyumba. Mama akamuita jamaa aje na mkewe waishi nae baada ya kuona maisha yamewachapa, alichofanya akaiba documents za manunuzi ya kiwanja akaenda kutengeneza hati miliki kwa jina lake halafu akawa anatumia hati kudhamini watu mikopo. Nyumba ikachorwa inauzwa ndio bibi kushtuka yeye anajua nyumba haina hati kumbe mwanae kamzunguka
 
Jamaa ni tapeli san halafu hana akili. Siku zake zinakaribia.

Anakaa Buswelu, Nsumba ingawa sasa hivi anaishi kama digi digi, baada ya kujua lolote linaweza kumkuta akapangisha hapo kwake.
 
Mmezidi unyonge malizeni kazi hiyo kima aisee))
Mtu mmoja anawasumbua serious..))??
Mnawacheka wanaume wa DAR nanyi wa Mwanza ni wale wale...))
 
Kama utakuja kununua eneo hasa mini mikubwa, ni 98% hili tatizo litakukuta.

Na kinaua zaidi sometimes ni DHULMA za wazi. Unaweza kuuziwa sehemu, ukitoka anauziwa mtu mwingine. Hivyo hivyo hata watu 200.
Siku nitakayouziwa siku hiyo hiyo naanza ujenzi
 
Mmezidi unyonge malizeni kazi hiyo kima aisee))
Mtu mmoja anawasumbua serious..))??
Mnawacheka wanaume wa DAR nanyi wa Mwanza ni wale wale...))
Ndio tunakoelekea. Kiubinadamu nadhani hili ni chaguo la mwisho.
 
Siku nitakayouziwa siku hiyo hiyo naanza ujenzi
Utauana na mtu ambaye siyo mhusika.

Mfano: Wewe una eneo lako sehemu halafu haupo, baadaye kumbe kuna mtu ambaye humjui akaleta mtu pale ameshauziwa amemwaga mawe na kuanza ujenzi.

Kwahiyo utaanza na mwenye ujenzi mpigane muuane wakati tapeli alishakula kona???
 
Mmezidi unyonge malizeni kazi hiyo kima aisee))
Mtu mmoja anawasumbua serious..))??
Mnawacheka wanaume wa DAR nanyi wa Mwanza ni wale wale...))
Acha kusema wanaume wa Mwanza, mtu mmoja mpuuzi asijekufanya ukaona watu wa Mwanza wanyonge. Me nachojua wakuja ndio huwa wanapigwa, hata mimi nikiona mtu hajielewi akijilengesha na mmega mwenyewe si ndo katega
 
Hivi wizara ya ardhi inashindwa kuweka mfumo kua hakuna pesa kuingia kwa muuzaji mpaka hati halisi itoke ndio pesa ziingie kwenye account ya muuzaji kutoka escrow account.
 
Hivi wizara ya ardhi inashindwa kuweka mfumo kua hakuna pesa kuingia kwa muuzaji mpaka hati halisi itoke ndio pesa ziingie kwenye account ya muuzaji kutoka escrow account.
Hawawezi kuweka mfumo wakati hawajapima zaidi ya asilimia 98% ya ardhi
 
Mkuu huwa nashangaa sana watu wanatapeliwaje viwanja.

Mimi kabla ya kununua viwanja lazima nifanye yafuatayo:-

1.Kuongozana na muuzaji(Tapeli)hadi wizara ya Ardhi kwenye wilaya/Mkoa husika ili kujiridhisha kama eneo limepimwa,Haliko barabarani,au siyo eneo la wazi ambalo litakuwa na matumizi ya kiserikali hapo baadae.

2.Kwenye huo mchakato wote ni lazima nishirikishe au niwe na mwanasheria muda wote.

3.Kabla ya Kununua eneo husika ni lazima huyo dalali(Tapeli) niwe nina uhakika anatambulika kihalali na serikali pia na chama au umoja wa Madalali wa Wilaya/Mkoa husika.

4.Kabla ya kununua eneo husika ni lazima nitawatembelea majirani wa hilo eneo ili kuwapeleleza na kufahamu uhalali wa hilo eneo,Majirani huwa wanaelewa sana maeneo na majirani zao wanaopakana nao.

5.Kabla ya kununua eneo ni lazima nimwambie Dalali nikutane na mmiliki halali wa hilo eneo ili nijiridhishe.

6.Mwisho kabisa,ni lazima nikutane na Serikali ya mtaa kupitia kamati ya Ardhi ya mtaa husika ili kufahamu undani wa eneo ambalo ninataka kununua.

Mkuu kwa mchakato huu unadhani ni rahisi kunitapeli?,Kumbuka mchakato huo wote ninakuwa na mwanasheria ambaye nitamlipa kwa kazi hiyo tu.

Watanzaia wengi wanaingizwa mkenge kwa kupenda mserereko na kutofuata sheria husika.
 
Kabla sijakujibu nikuulize maswali manne:

- Uko Tanzania?

- Umewahi kununua ardhi, nyumba au pagale Tanzania?

- Umewahi kufika Halmashauri idara ya ardhi au Wizara ya ardhi, Tanzania?

- Unaijua sheria ya madai Tanzania?
 
Wengi wanataka vitu rahisi ndio tatizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…