Picha: Kama umenunua Kiwanja, nyumba au Pagale ndani ya Jiji la Mwanza, ni zaidi ya 98% utakuwa umetapeliwa na huyu mtu

Unamfahamu huyu mtu?

Maana mama yake nimewahi kukutana naye.

Huyo jamaa hata ukimwazima gari, akipata mteja barabarani analiuza.
Duuuh[emoji2][emoji2][emoji2]
Basi mtu huyu kwa hakika atakuwa sio mzima kichwani.
 
Hawawezi kuweka mfumo wakati hawajapima zaidi ya asilimia 98% ya ardhi
Hapo ndio mfumo utamuumbua tapeli na kumsalimisha mnunuzi sababu mnunuzi atajua kwanza hiki kiwanja hakijapimwa, hakina hati ya umiliki.
 
Mkuu huwa nashangaa sana watu wanatapeliwaje viwanja.

Mimi kabla ya kununua viwanja lazima nifanye yafuatayo:-

1.Kuongozana na muuzaji(Tapeli)hadi wizara ya Ardhi kwenye wilaya/Mkoa husika ili kujiridhisha kama eneo limepimwa,Haliko barabarani,au siyo eneo la wazi ambalo litakuwa na matumizi ya kiserikali hapo baadae.

2.Kwenye huo mchakato wote ni lazima nishirikishe au niwe na mwanasheria muda wote.

3.Kabla ya Kununua eneo husika ni lazima huyo dalali(Tapeli) niwe nina uhakika anatambulika kihalali na serikali pia na chama au umoja wa Madalali wa Wilaya/Mkoa husika.

4.Kabla ya kununua eneo husika ni lazima nitawatembelea majirani wa hilo eneo ili kuwapeleleza na kufahamu uhalali wa hilo eneo,Majirani huwa wanaelewa sana maeneo na majirani zao wanaopakana nao.

5.Kabla ya kununua eneo ni lazima nimwambie Dalali nikutane na mmiliki halali wa hilo eneo ili nijiridhishe.

6.Mwisho kabisa,ni lazima nikutane na Serikali ya mtaa kupitia kamati ya Ardhi ya mtaa husika ili kufahamu undani wa eneo ambalo ninataka kununua.

Mkuu kwa mchakato huu unadhani ni rahisi kunitapeli?,Kumbuka mchakato huo wote ninakuwa na mwanasheria ambaye nitamlipa kwa kazi hiyo tu.

Watanzaia wengi wanaingizwa mkenge kwa kupenda mserereko na kutofuata sheria husika.
Unakuwa na mwanasheria wako unaenda hadi serikali ya mtaa na majirani unawauliza vizuri tu.

Na kupigwa unapigwa kama kawaida mkuu.,amini nisemacho.
 
Kwa ulivyoeleza ni ngumu kutapeliwa, lakin kuna mteja ataletwa ambaye atataka shortcut atauziwa kiwanja chako ulichonunua na kuwaachia mgogoro.
Utapeli wa ardhi hauna mahusiano na kutokujua. Unachanganyika na dhulma.

Kwasababu hata ukishajua sheria ya madai haitakusaidia.

Binafsi huyo jamaa documents zinahusisha mpaka wanasheria halali kabisa.
 
Hapo ndio mfumo utamuumbua tapeli na kumsalimisha mnunuzi sababu mnunuzi atajua kwanza hiki kiwanja hakijapimwa, hakina hati ya umiliki.
Ardhi iliyopimwa nchi hii ni kiasi gani?

Au fanya kwa Dar tu, ni asilimia ngapi ya Dar mji umepimwa?
 
Unakuwa na mwanasheria wako unaenda hadi serikali ya mtaa na majirani unawauliza vizuri tu.

Na kupigwa unapigwa kama kawaida mkuu.,amini nisemacho.
Ndio maana Mimi nawaambia Hawa watu hawajui wanachosema. Nina idha hawajawahi kununua ardhi hasa maeneo ya miji.

Yaani mtu anaamini eti ukienda na mwanasheria au ukienda ardhi hutatapeliwa.

Tena watu wa hivi, ndio Kutapeliwa ni dakika sifuri tu, Kwasababu wanaamini ardhi na wanasheria ndio mwisho wa matatizo.
 
Unakuwa na mwanasheria wako unaenda hadi serikali ya mtaa na majirani unawauliza vizuri tu.

Na kupigwa unapigwa kama kawaida mkuu.,amini nisemacho.
Ok mkuu hebu nielezee hapo namna utakavyopigwa!
 
Kwa ulivyoeleza ni ngumu kutapeliwa, lakin kuna mteja ataletwa ambaye atataka shortcut atauziwa kiwanja chako ulichonunua na kuwaachia mgogoro.
Mgogoro utakuwa kwake huyo aliyenunua baada yangu mkuu kwasababu mimi nyaraka zote nitakuwa nazo na hati juu!
 
Hati na documents kwa nchi hii ni vijikaratasi tu ambavyo havitaweza kukusaidia chochote.

Ipo siku utajua haya mambo kwa vitendo kabisa.
 
Hebu kajaribu kununua Kibaha, Mabwepande, Kivule, Kisemvule, Vikindu
Bro inshort utakavojiweka ndo matapeli watakavokuingia. Mi nna kiwanja kibaha, mapinga na Goba, kibaha na mapinga kuna utapeli wa kutisha, tapeli mmoja aliuza plot yangu cz sijaenda kusafisha wala kupaona for sometimes. Sikutaka kugombana na aliyeuziwa, kwenda polisi wa kwa mtendaji wa mtaa. Mi nlimtafuta aliyeuza nikamwambia ntakufanya usiyoweza kuhimili cz jamaa ndo tapeli mbabe maeneo yale, Akajua utani. Mwisho wa siku alimuita aliyemuuzia akamwambia usisogee kwenye kile kiwanja tena, nadhani walilipana. Kwa aliyoyaona mkewe aliamua kuondoka na jamaa utapeli aliacha.

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
 
sijaelewa hapo,kwa aliyoyaona KWA Mkewe au Kwa aliyoyaona Mkewe?
 
Bro inshort utakavojiweka ndo matapeli watakavokuingia. Mi nna kiwanja kibaha, mapinga na Goba, kibaha na mapinga kuna utapeli wa kutisha, tapeli mmoja aliuza plot yangu cz sijaenda kusafisha wala kupaona for sometimes. Sikutaka kugombana na aliyeuziwa, kwenda polisi wa kwa mtendaji wa mtaa. Mi nlimtafuta aliyeuza nikamwambia ntakufanya usiyoweza kuhimili cz jamaa ndo tapeli mbabe maeneo yale, Akajua utani. Mwisho wa siku alimuita aliyemuuzia akamwambia usisogee kwenye kile kiwanja tena, nadhani walilipana. Kwa aliyoyaona mkewe aliamua kuondoka na jamaa utapeli aliacha.

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
Sasa hizo mbinu zako zisizohusu polisi na mahakamani ndio tusaidiane. Kama uko tayari nije PM.

Nitakulipa kabisa.
 
Back
Top Bottom