Tunabishana kuhusu lifti, wakati kina mama wanajifungua hospitali wakiwa wamelala chini, shule hazina walimu, madaftari na madawati na waalimu hawalipwi na serikali, wagonjwa hawapati matibabu ya kutosha na waganga na watabibu hawalipwi vizuri wala hawalipwi kabisa, takataka zimejaa kila kona za miji yote Tanzania, mafuriko yapo kila mahali kwa sababu ya umbumbumbu wetu, "miji" yote ina foleni za kijinga tu, treni yetu imekufa na kila mzigo unasafirishwa kwa magari badala ya reli.
Watoto wetu mpaka waandamane ili waliiwe ada yao na hela za kujikimu.
Mahakama zote nchini zimeoza.
Ukiwa na shida ya siku moja ofisi ya ardhi inabidi uombe likizo ya mwezi kazini kwako.
Polisi wote wako busy kwenye misafara ya viongozi na sisi kunaambiwa kuwa kuna dhana ya polisi jamii na utii wa sheria bila shurti.
Maelfu ya wananchi hawajui kesho watakula nini.
Hivi ndio vitu vya kubishana na wala sio lifti na ghorofa ambazo sio zetu, hatuwezi kuwa wapangaji na wala hazituongezea tija katika kutatua matatizo yetu.