Picha: Mbunge wa Mlimba akikagua Daraja la Sh. Milioni 31 lilojengwa kwa miti
PICHA YA SIKU: Hili ni Daraja jipya katika Mto Mngeta uliopo katika mji wa Mlimba wilayani Kilombero.

Daraja hili limejengwa kwa miezi 7 kwa thamani ya shilingi milioni 31, na limejengwa kwa miti.

Pichani ni mbunge wa jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi, akikakagua mradi.

Miaka 60 ya Uhuru Kuna uzinduzi wa daraja la miti.hongereni Sana maccm
 
๐Ÿคฃ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ milioni 31 ya Zimbabwe? ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ
PICHA YA SIKU: Hili ni Daraja jipya katika Mto Mngeta uliopo katika mji wa Mlimba wilayani Kilombero.

Daraja hili limejengwa kwa miezi 7 kwa thamani ya shilingi milioni 31, na limejengwa kwa miti.

Pichani ni mbunge wa jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi, akikakagua mradi.

Madaraja Kama Haya yalikuwepo miaka ya nyuma kidogo huko kwetu kibosho na yalikuwa yanapitisha magari ya mizigo na abiria bila Shida Kwa hiyo sishangai.

Utofauti naouona hapo ni kwamba hayo ya kwetu yalikuwa yanatumia miti mikubwa miwili bila kuunga inalazwa Kutoka upande A kwenda B hivyo hakuna hizo nguo zilizochimbiwa kwenye maji kisha wanatandika boriti nene juu ya hiyo miti.

Miti Ilikuwa imepandwa Katika pande zote za mto Karibu na Madaraja hivyo Ilikuwa ni kuukata unaoonekana unafaa unaangukia mpaka upande wa pili hivyo kazi inakuwa nyepesi hakuna cha mkandarasi ni kazi ya msaragambo wa kijiji.

Hili nilivyolitathimini hizo Nguzo zilizoshikilia reli za daraja yakija mafuriko hapo linasombwa chap.
 
Ushauri wangu hii picha na taarifa iishie hapa hapa TZ. Wenzetu njee ya Afrika, na hasa Mabeberu wakiiona watatushangaa.
 
Hapo palistahili kujengwa kwa bilioni kumi shilingi za Kitanzania. Shilingi milioni 31 ni ndogo sana, kwa kazi kubwa ya kizalendo kama hiyo. Kimsingi hajawatuibia sana!
Kwa lugha nyepesi hapo wametupapasa tu wala hawajatupiga.
 
Sisiem walichakachua advance ya fundi maiko, akaona isiwe shida kapiga kitu wooden
 
PICHA YA SIKU: Hili ni Daraja jipya katika Mto Mngeta uliopo katika mji wa Mlimba wilayani Kilombero.

Daraja hili limejengwa kwa miezi 7 kwa thamani ya shilingi milioni 31, na limejengwa kwa miti...
๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ Feasibility study ilifanyika
 
PICHA YA SIKU: Hili ni Daraja jipya katika Mto Mngeta uliopo katika mji wa Mlimba wilayani Kilombero.

Daraja hili limejengwa kwa miezi 7 kwa thamani ya shilingi milioni 31, na limejengwa kwa miti.

Pichani ni mbunge wa jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi, akikakagua mradi.

Kama hujawai kupata shida hasa za vijijini hasa adha ya mawasiliano kutokana mvua n Mito mikubwa, huwezi kuona thamani ya hili daraja, tujikumbushe daraja mneso/kiteputepu, ziwe na kamba/miti, kwanza mnajua alietoa hizo pesa, mnajua wamehangaika miaka mingapi, Mungu awasaidie likiharibika watatengeneza tena na kuongezea ujuzi na ubora. Hongereni kwa hio hatua
 
Ni nani mwenye mamlaka ya kukagua miradi inayotekelezwa na TARURA mfano ,ujenzi wa barabara na madaraja? Kwa Hali inayoendelea fedha nyingi sana zitaliwa na wajanja na barabara za vijijini zitabakia kuwa mbovu . Mfano,
Daraja la Mto Mngeta lilitumia Tsh. milion 31.
 
Kama hujawai kupata shida hasa za vijijini hasa adha ya mawasiliano kutokana mvua n Mito mikubwa, huwezi kuona thamani ya hili daraja, tujikumbushe daraja mneso/kiteputepu, ziwe na kamba/miti, kwanza mnajua alietoa hizo pesa, mnajua wamehangaika miaka mingapi, Mungu awasaidie likiharibika watatengeneza tena na kuongezea ujuzi na ubora. Hongereni kwa hio hatua
Suala siyo kuona thamani ya hiko kidaraja. Hapa hoja ni kwamba hivi tumekuwa maskini kiasi hicho!??? Kwa nini mzalendo mmoja asiseme anaacha ubunge au utumishi kama serikali haitagharimia daraja la maana!???

Huoni hayo milioni yanaenda kupotea ndani ya muda mfupi, baada ya tumbao hutwo kuoza!??? Hivi ile Benzi ya Mzee Ruksa na kasri ya Mzee wa Msoga ni sawa na madaraja mangapi yenye hadhi sawa na ile ya Magufuli ya Kakongo-Busisi!??? Tanzania inarudi haraka ilikotoka.

Simply, Bi Mkubwa kazi imemshinda mapema sana!!!
 
Back
Top Bottom