Picha: Mbunge wa Mlimba akikagua Daraja la Sh. Milioni 31 lilojengwa kwa miti
Kwa hiyo, Samia anasema anaweka tozo kwenye mafuta na simu kwa ajili ya barabara za vijijini, yaani wakazidi kufanya mambo kama haya?

Kwa hizo milioni 31 ningewajengea daraja bora kuliko hili. Angalau columns zingekuwa za concrete na beams za mbao. Kuna siku moja hili daraja litaua, maana hawatajua hizo nguzo za miti kama zimeoza na lita- collapse.

View attachment 1872750
Tozo yako inaenda hapa kijana
 
Mkichagua upinzani sileti maendeleo,
alisikika mhuni mmoja huko kuzimu.
 
Madaraja ya aina hiyo nilipita ileje huko unatakiwa uwe na roho ngumu ukipita na roli lina mzigo bora hili linaonekana lina uimara kidogo...mbao kama wametoa kijijini gharama mbona kubwa kidogo au waliagiza hizo mbao...
 
Mwafrika ni nyani aliyechangamka Behaviourist . Kule kwetu ni moja ya sehemu wakoloni waliishi na kujenga shule miaka ya 1890. Mpaka sasa kuna madaraja yanayoungsnisha vijiji yalijengwa zaidi ya miaka 100 iliyopita.

Inashangaza sana ,yaani wanateketeza zaidi ya milioni 400 kumnunulia DED Vieite wakati hapo hapo ana mshahara wa zaidi ya milioni 6 huku wakishindwa kujenga daraja la kudumu lenye kuhudumia zaidi ya wakazi 1000 wa sehemu husika.
 
Kunambi ni mtu makini sana ila kwa huu ukaguzi ni UTOPOLO amefanya.

Karne hii ya sayansi na technology unajenga daraja kwa miti? Wameshindwa kuweka column kila upande na beam? Daraja ambalo alizidi 15 meter unajenga kwa miti?

Tena daraja ambalo hata boat hazipiti?
Wameshindwa kumwaga hata zege

Believe me hizo mbao watagawana baada ya kuanguka
 
Hiviii hata aibu hii ya kawaida tuu hawana?!? Hawajioni kama wako uchi kama hilo daraja lao.?? Wooii
 
Mwafrika ni nyani aliyechangamka Behaviourist . Kule kwetu ni moja ya sehemu wakoloni waliishi na kujenga shule miaka ya 1890. Mpaka sasa kuna madaraja yanayoungsnisha vijiji yalijengwa zaidi ya miaka 100 iliyopita.
ya miti kama hili?
 
Kuna watu wanakenua hapa ila utakuta huko ndio kwao na hawajatoa mchango wowote hata kwenye Hilo daraja la miti.
Hawajatoa vipi wakati maisha yao ya kila siku wanalipa kodi? Tena sasahivi kuna tozo ya miamala
 
CCM wakijaribu kushawishi umma kuwa wao siyo mafisadi.
AQaYr0.jpg
 
Maendeleo hayana chama
Wananchi watafaidi kodi zao kupita kwenye daraja la kizalendo lililojengwa na malighafi za hapa nchini[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kunambi maana yake nini kwa lugha yao? Majina yana maana
 
Tumeongeza tozo kwenye miamala ili tuwaletee maendeleo kama hayo au nasema uongo ndugu zangu?🤗🤗
 
Back
Top Bottom