Picha: Mbunge wa Mlimba akikagua Daraja la Sh. Milioni 31 lilojengwa kwa miti
Kunambi ni mtu makini sana ila kwa huu ukaguzi ni UTOPOLO amefanya.

Karne hii ya sayansi na technology unajenga daraja kwa miti? Wameshindwa kuweka column kila upande na beam? Daraja ambalo alizidi 15 meter unajenga kwa miti?
😂😂Hilo daraja lina tofauti gani na lile walilojenga wasukuma (source:Millardayo)
 
PICHA YA SIKU: Hili ni Daraja jipya katika Mto Mngeta uliopo katika mji wa Mlimba wilayani Kilombero.

Daraja hili limejengwa kwa miezi 7 kwa thamani ya shilingi milioni 31, na limejengwa kwa miti.

Pichani ni mbunge wa jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi, akikakagua mradi.

View attachment 1872581
Wadau mbona hamuongelei mda wa ujenzi?
 
Wakuu habari sio daraja hapa,habari ni kivipi mil 31 zitumike kujenga uchafu huu?

wameshindwa hata kujenga nguzo tu,then juu ndio watandike hizo mbao wakati wanatafuta hela ya kumimina slub?

wafungwe wote...hapo gharama kwa walichokifanya mil 6 zingetosha kabisa!
 
PICHA YA SIKU: Hili ni Daraja jipya katika Mto Mngeta uliopo katika mji wa Mlimba wilayani Kilombero.

Daraja hili limejengwa kwa miezi 7 kwa thamani ya shilingi milioni 31, na limejengwa kwa miti.

Pichani ni mbunge wa jimbo la Mlimba, Godwin Kunambi, akikakagua mradi.

View attachment 1872581

Hayo ndio makusanyo ya tozo za uzalendo za wiki hii nini?
 
Kuna watu wanakenua hapa ila utakuta huko ndio kwao na hawajatoa mchango wowote hata kwenye Hilo daraja la miti.
Mchango upi tena mkuu ,kodi ,tozo na chanjo havitoshi?sio kazi ya wananchi kujenga madaraja
 
Mbunge Unatumia FEDHA ya JIMBO kujenga Daraja la Aina hii kwa Tsh.Mil.31
Daraja la Mabanzi yanayopatikana kwa Michango ya Wananchi Ukweli Wabunge wetu Wapiga Kura sio Wajinga Kihivyo huu ni WIZI wa KODI za Masikini
20210729_144423.jpg
 
Mwananchi shituka, serikali inatakata watu wahamie kwenye mabenki siyo kurundika pesa kwenye simu. Mwananchi cheza na beat. Hamia Benki. Mabenki yana mawakala hadi vijijini, hamisha pesa benki kwenda benki, halafu yeye mtoaji atakatwa kiasi kidogo wakati wa kutoa.
 
Milioni SELASINI NA MOJA . Selasini na moja. Mungu ibariki Tanzania
 
unless hii habari ni fix, ila kama ni kweli - hii ni aibu kubwa wa CCM, kubwa mno.
 
Unanunua gari la mabilioni huku vyoo hakuna

Acha tu , kiongozi anaenda na gari la milioni 300 kwenda kuangalia shule haina choo cha shimo,shule haina maji ,inasikitisha sana.

Kuchimba kisima kikawaida ukiacha magumashi ni rahisi sana ,ukiweka rate ya 65k per meter! Means kisima cha mita 150 ni around 9m.

Kwasasa kuna vyoo vya kisasa visivyojaa ,kama vya shule unaweza kutengeneza kwa gharama hata haifiki milioni 10 ,ukiweka gharama za spetic 2.5m na majengo ya matundu matano ya kike na ya kiume.

Sasa kila kata zina shule ngapi za msingi na sekondari? Kiwastani kwenye kata hazizidi shule 6 za primary na sekondary means kila kata ukitenga 120m unamaliza tatizo la maji na vyoo katika shule zote za kata.....yaani hata bei ya robo ya VX haifiki.
 
Back
Top Bottom