Picha: Muonekano wa kuvutia wa Barabara ya Mbinga - Mbamba Bay

Dah umenikumbusha mbali sana aisee, hizo barabara zilikuwa hazifai,
Mbamba Bay fish 🐠 za kutosha huko

Njoo baada ya miaka miwili uone jinsi itakavyokuwa imechakaa!! Wanajenga chini ya viwango kutokana na usimamizi mbovu! Hizi barabara hazina DRAINAGE system hivyo maji ya mvua yanaharibu barabara kirahisi!!
 
Tatizo hizi barabara wanajenga bora liende, hii barabara naipa miaka miwili hamna kitu hapo
 
Sasa kuzunguka kote huko ili iweje, si kuna shortcut hapo? Haya ndiyo matatizo ya kuwapa kazi wakandarasi wazawa, hawana maajabu bali kulitia taifa hasara tu.
 
Hivi mnasifia nini hapo?

Hiyo barabara hamuoni kuwa ni sehemu hatari sana hizo kona zenye miteremko hatari iliyokaa upande upande ni salama kiasi gani kwanini hiyo barabara isiungane moja kwa moja litumike daraja hapo

Hizi ni akili za kimaskini sana tukae na records ajali zitakazotokea hapo kwa ujinga wa wachache
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…