nduza
JF-Expert Member
- Feb 7, 2019
- 1,595
- 2,503
hasara ya mali za watu, maisha pamoja na matumizi mabaya ya fedha za ummaYes hata mi nimeshangaa sana watu wanasifia ujinga!
Hizi kona kona ni hatari kwa vyombo vya usafiri, wamekwepa gharama za kujenga daraja na hizo kona kona wametumia lami badala ya concrite,
kwa mifumo ya magari jinsi ilivyo tairi za nyuma huwa zinajiburuza kwenye kona ( hasa malori)
Hiyo barabara haitachukua muda mrefu kuharibika na ni matumizi mabaya ya fedha za walipakodi.
Mfano mzuri wa kudeal na sehemu zenye kona ni barabara ya arusha to dodom, kama sikosei ilijengwa kwa ufadhili wa IMF. kwenye milima ya kolo pale wamepiga concrete mwanzo mwisho'
ukipita barabara ile utaona jinsi thamani ya pesa ilivyolindwa'
Barabara inayosifiwa hapa itatia hasara kwani itahitaji ukarabati wa mara kwa mara.
Akili ndogo inaangalia kurahisisha mambo tu bila kuangalia madhara yatakayokuja