Picha na Maelezo: Yaliyojiri ktk Viwanja vya Jangwani Mkutano wa UKAWA 26/10/2014

Status
Not open for further replies.
Taratibu CCM inaelekea ilikoelekea KANU ya Kenya!!
Watafurukuta lakini hawataweza.... haya ni matakwa ya MUNGU kwa watu wake!!!
Wewe ndio wasema hata mkakati wa kuungana umetoka CCM kaa kimya hujuwi kitu wewe! Sasa ndio mwisho wa upinzani nchini Subiri uone!
 
Huu muungano nina mashaka nao, huenda ni mbinu ya kuiangamiza CHADEMA kupitia CUF. Viongozi wa CUF ni vigeugeu, angalia Seif yeye ni msaka tonge haeleweki, Mwenyekiti wa CUF Lipumba alikiri mwenyewe kuwa Cuf ilimsaidia Kikwete ashinde. Sasa kwa historia hii bado nina mashaka na huu "UKAWA", kimbembe kitakuwa ni Chama gani kitoe mgombea Urais hasa kati ya CHADEMA na CUF, hapo ndiyo tunaweza shuhudia mwanzo wa mpasuko. Tuombe tu Mungu awasaidie.
 
Hivi ni kweli kabisa wanaaminiana toka mioyoni mwao? Hakuna ukigeugeu wowote ndani ya mioyo yao?

Tusubiri tuone wakati wa kuachiana vitongoji/vijiji/sheiya/kata/majimbo manake mtihani mkubwa upo hapo.

Mtu amewekeza miaka mitano au kumi leo unakuja kusema kwamba aaaaaah wewe hukubaliki tumwachie Makaidi!!
 
Umati huu ukijitokeza kupiga kura hapo sawa lakini kama ni kukusanyika tu! Hakuna mabadiriko
 
Ukitizama hizi picha kwa umakini, umati huu 95% ni vijana wa kiume kati ya miaka 25 na 35, 4% ni wanawake wa umri uleule lakini wamevaa skaf za CUF hivo si wana cdm na 1% ni wazee, lakini ukiangalia idadi ya watu Tanzania 60% ni wanawake 45% ni vijana kati ya miaka 25 hadi 35, hivyo waliohudhuria ni 24% ya watanzania ndo washabiki wa hizi siasa.

Je inakuwaje rika hili ndo limepata mwitikio? hawa wengi ni vijana wasiokuwa na ajira za uhakika kutokana na kutopata elimu stahiki na stadi za kazi, je kwanini vijana wa umri wa 16 hadi 24 hawako katika kundi hili ni kwa sababu wako mashuleni na vyuoni na waliomaliza wamepatiwa ajira hasa za ualimu jeshi na viwandani. Kundi hili halikubaliki katika ajira rasmi kwani mtakubaliana nami kundi hili ni watukutu wapiga videbe na wachora dili,

je nikweli? hapana wengi wao wanamajukumu ya kifamilia hivyo vipato vyao kwa maana ya mishahara na posho hazitoshi kuendesha familia ukizingatia bei ya sembe mchele sukari na mkaa vinapanda kila siku. Wanawake katika kundi hili hawamo kwani wengi wao wako kwenye ndoa na wanamajukumu ya kulea familia ila wako pamoja na waume zao kwani mahangaiko yao wanayaona dhahiri.

Mwitikio huu upo mijini zaidi hasa katika miji ya Dar Mwanza Arusha na Mbeya hii ni kutokana na kukosekana miradi yenye kuajiri vijana wengi, miradi mikubwa kama ya nssf na ppf inalenga kuajiri watu wachache na wafaidikaji wakubwa wamekuwa wachina. Mtakubaliana nami kwa kipindi chote cha JK hakuna mradi uliojiri vijana elfu 3 kwa mpigo, tofauti na wakati wa mkapa migodi ya dhahabu pekee iliajiri vijana zaidi ya elfu 15 kwa mpigo.

Kimsingi kwa miaka kumi tumekalia porojo zaidi huku fedha nyingi zikitumika katika mambo yasiyokuwa na tija kama tume ya warioba na bunge la katiba. kumkirimu Obama ziara za kuvishwa majoho na ujenzi wa bomba la gesi.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…