Picha: Siku Magufuli alivyozindua kiwanda cha Rostam Morogoro

Picha: Siku Magufuli alivyozindua kiwanda cha Rostam Morogoro

Attachments

  • 20250830_080352.jpg
    20250830_080352.jpg
    31.6 KB · Views: 25
Hii ilikua ni February 12 mwaka 2021,na baada ya hapo hii ndo ilikua ziara yake ya mwisho kwani baada ya hapo alienda hadi Dsm mbezi kuzindua stend na ikawa ndo mwisho wa kuonekana kwake.

Nimeweka picha zote.

Rais Magufuli ampongeza Rostam Aziz kwa kuanzisha kiwanda Morogoro

Ijumaa, Februari 12, 2021

Muktasari:

Rais Magufuli amezindua Kiwanda cha Ngozi cha ACE Leather Tanzania Limited-Kihonda

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli ampongeza mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz kwa kuanzisha kiwanda mkoani Morogoro.

Mbali na pongezi hizo, Magufuli amemshukia mbunge wa Morogoro Mjini Aziz Aboud kwa kushindwa kuendesha viwanda.

“Nakupongeza sana Rostam kweli nakupongeza kwa sababu rafiki yako mbunge wa hapa ameshindwa kuendesha viwanda viwili. Mimi huwa ni mkweli nazungumza kwa uwazi, Aboud alichukuwa viwanda viwili vikubwa cha Calvan na Moplo.

“Kiwanda cha Moplo kilikuwa kinahusika na mafuta ya kupikia, mimi nasema hadharani sikufichi, ulipewa viwanda tangu mwaka 1996 hadi mwaka jana walipokunyang’anya uliwanyima ajira hata wapigakura wako,” amesema Magufuli.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo, Ijumaa Februari 12, 2021 wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha Ngozi cha ACE Leather Tanzania Limited-Kihonda, kinachomilikiwa na Rostam.

Katika maelezo yake Rais Magufuli amesema, “huu ndiyo ukweli na mimi nitabaki siku zote kusema ukweli, nasema uongo ndugu zangu? Aliitikiwa kweli na wananchi. Abood amekaa na viwanda vya Moplo na Calvan kwa zaidi ya miaka 25.

“Huyu leo simpongezi ingawa jana nilimpongeza kwenye viwanda ndugu Abood hujafanya vizuri. Nikiondoka Morogoro sijasema hili nitakuwa mnafiki,” amesema Rais Magufuli.

Katika hafla hiyo Rais Magufuli amesema Kiwanda cha Calvan kiliuzwa kwa Benki ya CRDB, ambayo hata hivyo hawakukiendeleza, huku akimuagiza Waziri wa Viwanda na Biashara, Geoffrey Mwambe kusimamia suala hilo na kiwanda hicho kifanye kazi.

View attachment 3458185View attachment 3458188View attachment 3458189View attachment 3458191View attachment 3458195View attachment 3458196
Wanamtandao sio watu wazuri!🙌
 
Kwahili nakataa. Magufuli alianza kutembea na AC na feni hata sehemu ambazo kwa mtu mwenye afya njema hapahitaji usaidizi wa hewa. Kuonesha alikuwa tayari amedhurika tazama mwonekano wale kwenye hizo picha.
Mbona hata Samia anatembea na feni na AC? Unajua kazi ya AC?
 
Watu wanazunguka mno, kifupi Rosti tamu na Juma Kaseja ndo "waliomtembeza" JPM kwa ushirikiano wa karibu na [emoji355]️[emoji817]
 
Kabisa alafu nachomlaum huyu msukuma ni Ile kuuwa wanaharakati angeanza na wana mtandao akampga TL risasi na Kuuwa Upinzani pengine angekaa na akina TL vizuri wangemsanua wanamtandao ni kina nani na jinsi wanavyomuwinda Pengine asingeua Upinzani kwa Ubabe wangeenda kuropoka ndani ya Bunge wanamtandao walivyo hatari na wanavyomuwinda Hii ndo Ile wanasema the enemy of your enemy is your friend.


Kweli nilikua Simpendi hata nyuzi nyingi nmemkandia ila Kuuwawa kwake kumeniumiza ukitegemea na Cake wanayokula kina Kiziga na Mama Abdul na Rostam
Huenda wapinzani wangekaa naye vizuri hata katiba mpya wanayotaka wangepata
 
Kabisa alafu nachomlaum huyu msukuma ni Ile kuuwa wanaharakati angeanza na wana mtandao akampga TL risasi na Kuuwa Upinzani pengine angekaa na akina TL vizuri wangemsanua wanamtandao ni kina nani na jinsi wanavyomuwinda Pengine asingeua Upinzani kwa Ubabe wangeenda kuropoka ndani ya Bunge wanamtandao walivyo hatari na wanavyomuwinda Hii ndo Ile wanasema the enemy of your enemy is your friend.


Kweli nilikua Simpendi hata nyuzi nyingi nmemkandia ila Kuuwawa kwake kumeniumiza ukitegemea na Cake wanayokula kina Kiziga na Mama Abdul na Rostam

..laana ya kuua wapinzani.

..kamdungua Ben Saanane na yeye kadunguliwa.
 
Sijui ni muda gani walimpiga tukio
Mshana kwa Picha Tu Huwezu Ona.. Vingine huwa ni Off Camera. Tena unakuta hata Picha zilizopigwa zimepigwa ki masta zaidi ili Hata Wachunguzi wasigundue Kitu..

Unless ulikuwa eneo la Tukio mwenyewe na Ukajua Kitu gani kilifanyika Sekunde kwa sekunde.

Na inawezekana hata ikawa si Kwa Tukio hili la Kuzindua kiwanda ikawa ni Jambo lililofanyika Hapa wakawa wanajifanya Wema si unajua mchawi anakuchekea mchana usiku anakuroga
 
Sasa Kwan nini alimpiga TL risasi kwa nini aliwapoteza kina Saa8 na Azori kwa nini aliua Upinzani Magu ilifikia stage akawa anawachukia watu wa Kanda flani Yani ww niambie labda angepaswa adili na hao wahuni wenzake
Soma kuna Uzi mmoja humu unamzungumzia TL kwamba Wanamtandao pia walimuweka kati na Kwa vile ni Muongea sana alitumiwa vizuri na Wana mtandao kuzoofisha mambo ya Jiwe.. Nahisi ni Uzi wa Yoga Dark Days
 
Back
Top Bottom