Nimeongea jana na watu wawili mashuhuri pale Iringa (nahifadhi kwa sasa majina yao wasije potezwa) wakisikitishwa na kitendo anachofanyiwa aliyekuwa mbunge wao halali Peter Msigwa cha kubebeshwa Bango kama vijana wa Chipukizi. Ni kweli kwa sasa Msigwa anatumika kuitukana Chadema na hususani viongozi wake Mbowe na Lissu, na kuchonganisha na wengine.
Hiyo ni mission ya CCM kuelekea uchaguzi, lakini kumdhalilisha kwa kumbebesha mabango kama mzee yatima ni kuwatukana Watu wa Iringa walio wahi kumchagua kwa vipindi viwili huku cha Tatu wakiibiwa kura zao.
Hizi dharau haziendi kwa Msigwa au Chadema bali wana Iringa kuwa walikuwa wajinga kumchagua mtu wa hovyo kama mbeba mabango mpya wa CCM.
Msigwa aliyekuwa anaweza kuhenyeshana na kina Kinana leo hata katibu wa UVCCM Mwembetogwa anaweza kumpa majukumu?
#Wamelia sana!