Picha: Watanzania mnakula sana mbwa bila kujua. Usijitapishe ukiona hii picha

Picha: Watanzania mnakula sana mbwa bila kujua. Usijitapishe ukiona hii picha

Kuna sehemu walikuwa wanauza supu ya mbuzi kumbe ni ya mbwa, walitundika kichwa, ngozi na miguu ya mbuzi kuaminisha kuwa ni mbuzi. Cha ajabu ukila nyama hiyo na kunywa supu yake unaanza kujisikia kiu kubwa, kumbe umekula mbwa
Tunagonga tu, kibaya ukijua unakula nini, nyama za wanyama kuanzia kwenye mishkaki,sambusa,supu,nyama choma na roast zinaliwa sana,

Kuna safari nilisafiri kwa treni, Kuna kituo nikanunua nyama ya kuku ,aisee sijui ilikuwa nini, kuku sio kuku kama limwewe,sijui lihondohondo,sijui lindege gani la ajabu.
 
Dar ndy kunaongoza Kwa kuliwa nyama za ajabu ajabu,hasa uswahilini

Unakuta jioni mtu amezungukwa na watu kibao unajiuliza anauza nn pale,ukisogea unakuta anauza supu,ukiangalia sasa hiyo supu,unauliza unataka koromeo,kwasukwasu,ubongo,nyama nyama au bandama? Watu wanadhani wanakula supu ya nyama ya ng'ombe Tu kumbe supu zingine za ajabu ajabu

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Sas kwa dar mbwa koko mbn adimu sana
Hao mbwa kishua si ni mamilion kuwanunua ili uwachinje uuze supu[emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my SM-G930F using JamiiForums mobile app
 
Huji kukuta mbwa kafa Iringa...ila wanapunguaga tu. Unashangaa tu kuna mnyama haonekani. Usihoji sana, unapotezea!
 
Back
Top Bottom