Picha za wakuu wa JWTZ tokea Tanzania ilipopata uhuru wake

Picha za wakuu wa JWTZ tokea Tanzania ilipopata uhuru wake

VOICE OF MTWARA,
Brig.Hassan Ngwilizi aliongoza vikosi vya Tz vilivyokwenda Msumbiji "operation safisha" na Seychelles "operation mahe".

Kuna mwana JF amepata kuandika kwamba Lt.Gen.Abdulrahmani Shimbo alikuwa miongoni mwa askari wa Tz waliotumikia Seychelles. Pia hivi majuzi Raisi alitoa nishani za "operation safisha" ya Msumbiji na Lt.Gen.Mwakalindile, Lt.Gen.Ndomba, pamoja na Brig.Gen.Hassan Ngwilizi, walikuwa miongoni mwa askari waliotunukiwa nishani hiyo.

Kitabu cha "war in uganda" kinaeleza kuhusu kikosi cha jwtz kilichokuwa mpakani mwa Msumbiji na rhodesia/zimbabwe btn 1975 na 78. Kikosi hicho kilirejeshwa Tz wakati vita ya Kagera ilipoanza.

Pia Ndani kitabu hicho kuna habari za askari wa tanzania waliopata mafunzo northern vietnam!!

Historia ya majeshi yetu inapaswa kuwekwa wazi haswa kwa vijana ili kuwajengea mwamko wa uzalendo kwa taifa lao.

Majuzi taifa limepatwa na msiba mzito wa kuondokewa na makamanda, Maj.Gen.Muhidin Kimario, Maj.Gen.Lupogo, na Maj.Gen.Makunda, ambao waliongoza vita vya Kagera/Uganda.

mkuu JokaKuu historia ya nchi yetu inafichwa fichwa hata bila sababu za msingi. wizara inayohusika na utamaduni amkeni basi muweke kumbukumbu hizi. ni aibu sana kwa matukio ya miaka ya 60 au 70 kutokufahamika au kurekodiwa kwa ufasaha. nchi kama Ethiopia wameweza kutunza historia ya matukio ya miaka 3000 iliyopita, inakuwaje hapa inashindikana?
 

Attachments

  • DSC06904[1].JPG
    DSC06904[1].JPG
    12.2 KB · Views: 766
Daah safi sana kuna Jamaa alioa mtoto wa Gen. Robert aisee mbona jamaa anakoma maana anapigwa makonde na mitama ya kutosha kila kukicha. Watoto wa wanajeshi uwaone kwa mbali. Tamaa za fedha vyeo za baba zao zitatutokea puani
 
Twalipo ndo alikuwa mkuu wa majeshi kipindi cha vita ya kagera na sio msuguri kama unavyodai

Yupo sahihi kwani kasema Musuguli aliongoza vikosi vita ya Kagera. Na wakati huo Twalipo alikuwa mkuu wa majeshi.
 
Ally Kombo,
Kiwelu aliongoza operation ya kumuondoa Amin ktk ardhi ya Tanzania. Yeye ndiye alikuwa mpiganishaji mkuu.
Baada ya ushindi huo Musiguri akapewa jukumu la kuongoza majeshi yetu ktk mapigano ndani ya Uganda. Kiwelu alirejea ktk nafasi yake ya mnadhimu mkuu.
Pia Kiwelu ameweka historia ya kutumikia nafasi ya chief of staff mara mbili. Mara ya kwanza chini ya Lt.Gen. Abdalah Twalipo, na mara ya pili na Gen.Mwita Kiaro. Kwa maana hiyo aliaminiwa na Raisi Nyerere, pamoja na Raisi Mwinyi.
Vilevile Kiwelu ndiye Mtanzania pekee aliyetunukiwa ngazi ya Generali bila kushika nafasi ya Mkuu wa Majeshi/cdf.
Mwisho, Gen.Kiwelu alipata kuteuliwa na raisi Mkapa kuwa balozi wetu Ufaransa. Echolima

Hv ndo huyohuyo alikuwa mkuu wa mkoa wa Kagera?
 
Last edited by a moderator:
Hongereni jeshi letu. hv wanajeshi Wanawake wanaolewaga kweli?
 
Ubaguzi shida. Too light skinned.

..Col.Mahfudhi aliwekwa kizuizini akituhumiwa kuhusika na mipango ya mauaji ya Raisi Karume wa Zanzibar.

..baada ya kutolewa kizuizini alichukuliwa na Samora Machel kuwa mshauri wake wa ulinzi, na inasemekana pia alifundisha askari wa Museveni.

..Col.Ali Mahfudhi alifariki Msumbiji na amezikwa huko. Kuna watu wanadai amepewa heshima kwa kuzikwa ktk makaburi ya mashujaa.

..kuhusu tuhuma za ubaguzi wa ndugu zetu wenye "light skins" naomba nikupe challenge kidogo. Vipi kuhusu Maj.Gen.John Walden "black mamba" ambaye aliaminiwa ktk nafasi mbalimbali ktk vita vya Msumbiji, na hata vita vya Kagera? Vipi kuhusu Brig.Gen.Curthless ambaye alipanda vyeo na kutunukiwa nishani ya ushujaa na Raisi kutokana na kitendo chake cha kuwaokoa askari aliokuwa akiwafundisha wasilipukiwe na guruneti. Brig.Gen.Curthless alipoteza mkono wake ktk tukio hilo.
Ally Kombo, Echolima, Manyerere Jackton, VOICE OF MTWARA
 
Last edited by a moderator:
Hv ndo huyohuyo alikuwa mkuu wa mkoa wa Kagera?

..ndiye huyo huyo.

..pia aliwahi kuwa mkuu wa mkoa wa Tanga, Tabora, na Shinyanga.

..nimesoma kwamba baada ya kustaafu ameamua ku-settle Kagera akijihusisha na kilimo cha kahawa.

..majuzi nimeona kwamba kuna ukumbi wa mikutano ktk Chuo cha Maofisa Monduli umepewa jina la Tumainieli Kiwelu.
 
Back
Top Bottom