mkuu JokaKuu historia ya nchi yetu inafichwa fichwa hata bila sababu za msingi. wizara inayohusika na utamaduni amkeni basi muweke kumbukumbu hizi. ni aibu sana kwa matukio ya miaka ya 60 au 70 kutokufahamika au kurekodiwa kwa ufasaha. nchi kama Ethiopia wameweza kutunza historia ya matukio ya miaka 3000 iliyopita, inakuwaje hapa inashindikana?
..sisi hapa tumejikita kwenye siasa tu.
..kwenye nchi za wenzetu utakuta kuna minara ya kumbukumbu za mashujaa.
..pia sherehe za mashujaa, na kumbukumbu za kuanzishw kwa majeshi yao, ni matukio makubwa. utaona yanatangazwa kwenye vyombo vya habari kwa Raisi na viongozi mbalimbali kushiriki. pia huwa ni siku za mapumziko kwa wanafunzi na watumishi wa serikali.
..pia wanakuwa na vitu kama Kofia, t-shirts, beji, number za magari, vyote hivyo kuonyesha kumbukumbu, na kusherehesha ushindi wao, ktk vita mbalimbali.
..lakini zaidi ni huduma za afya wanazojitahidi kuwapatia mashujaa waliotumikia jeshini.
NB:
..lakini siyo matukio ya ushindi tu hukumbukwa. hata kule walikoshindwa wenzetu huwakumbuka wenzao "who paid the ultimate sacrifice." Kwa mfano, nimewahi kuona documentary ya Operation Eagles Claw ambapo Wamarekani walifeli ktk jaribio lao la kwenda kuwaokoa mateka waliokuwa wakishikiliwa Iran.
..Lakini kufeli kwa Operation Eagle Claw ndiyo chanzo cha wao ku-fine tune mbinu zao mpaka walipoweza kufanikisha operation ya kumuua Osama Bin Laden. Kama umetizama film ya kuuwawa Osama utaona pale helikopta moja ilipopata matatizo kuna jamaa mmoja aliyekuwa makao makuu ya CIA akifuatilia video feed toka Abottabad alisema "Operation Eagles Claw all over again!!". Hofu iliwatanda kwamba yaliyotokea Iran in 1980s yanajirudia Pakistan.
cc Echolima, Pasco, Nguruvi3, Kichuguu, Nguruvi3
Last edited by a moderator: