Picha za wakuu wa JWTZ tokea Tanzania ilipopata uhuru wake


mkuu JokaKuu historia ya nchi yetu inafichwa fichwa hata bila sababu za msingi. wizara inayohusika na utamaduni amkeni basi muweke kumbukumbu hizi. ni aibu sana kwa matukio ya miaka ya 60 au 70 kutokufahamika au kurekodiwa kwa ufasaha. nchi kama Ethiopia wameweza kutunza historia ya matukio ya miaka 3000 iliyopita, inakuwaje hapa inashindikana?
 
Daah safi sana kuna Jamaa alioa mtoto wa Gen. Robert aisee mbona jamaa anakoma maana anapigwa makonde na mitama ya kutosha kila kukicha. Watoto wa wanajeshi uwaone kwa mbali. Tamaa za fedha vyeo za baba zao zitatutokea puani
 
Twalipo ndo alikuwa mkuu wa majeshi kipindi cha vita ya kagera na sio msuguri kama unavyodai

Yupo sahihi kwani kasema Musuguli aliongoza vikosi vita ya Kagera. Na wakati huo Twalipo alikuwa mkuu wa majeshi.
 

Hv ndo huyohuyo alikuwa mkuu wa mkoa wa Kagera?
 
Last edited by a moderator:
Ni ukurya tu...si unajua tena nyerere aliwakabidhi wakurya jeshi?
Miaka yetu hiyo ya Gezaulole tulikuwa tunatranslate JWTZ kama Jeshi la Wakurya Tangu Zamani. LOL!
 
Hongereni jeshi letu. hv wanajeshi Wanawake wanaolewaga kweli?
 
Ubaguzi shida. Too light skinned.

..Col.Mahfudhi aliwekwa kizuizini akituhumiwa kuhusika na mipango ya mauaji ya Raisi Karume wa Zanzibar.

..baada ya kutolewa kizuizini alichukuliwa na Samora Machel kuwa mshauri wake wa ulinzi, na inasemekana pia alifundisha askari wa Museveni.

..Col.Ali Mahfudhi alifariki Msumbiji na amezikwa huko. Kuna watu wanadai amepewa heshima kwa kuzikwa ktk makaburi ya mashujaa.

..kuhusu tuhuma za ubaguzi wa ndugu zetu wenye "light skins" naomba nikupe challenge kidogo. Vipi kuhusu Maj.Gen.John Walden "black mamba" ambaye aliaminiwa ktk nafasi mbalimbali ktk vita vya Msumbiji, na hata vita vya Kagera? Vipi kuhusu Brig.Gen.Curthless ambaye alipanda vyeo na kutunukiwa nishani ya ushujaa na Raisi kutokana na kitendo chake cha kuwaokoa askari aliokuwa akiwafundisha wasilipukiwe na guruneti. Brig.Gen.Curthless alipoteza mkono wake ktk tukio hilo.
Ally Kombo, Echolima, Manyerere Jackton, VOICE OF MTWARA
 
Last edited by a moderator:
Hv ndo huyohuyo alikuwa mkuu wa mkoa wa Kagera?

..ndiye huyo huyo.

..pia aliwahi kuwa mkuu wa mkoa wa Tanga, Tabora, na Shinyanga.

..nimesoma kwamba baada ya kustaafu ameamua ku-settle Kagera akijihusisha na kilimo cha kahawa.

..majuzi nimeona kwamba kuna ukumbi wa mikutano ktk Chuo cha Maofisa Monduli umepewa jina la Tumainieli Kiwelu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…