Huo ni uongo mkubwa sana unaowazulia akina zitto, wao wanataka "KWANZA" maendeleo ya WATU halafu ndipo maendeleo ya vitu.
Wao na hata mimi na hata baba wa taifa tunataka kwanza maendeleo ya watu ndipo maendeleo ya vitu, maendeleo ya watu ni kama:- Uhuru na haki zao, Afya (huduma za afya bora, madaktari, vifaa tiba, madawa nk ), maji safi ya kunywya nk, lishe bora, watu waweze kujijengea makazi bora nk, mzunguko mzuri wa pesa, mazingira bora ya kufanya biashara, kilimo ufugaji nk, (kuondoa kodi gandamizi), wafanyakazi wa serikali wapewe haki zao zilizopo kisheria nk, uhuru wa watu kupata habari na kutoa habari kuhusu nchi yao, usalama wa watu na mali zao, wananchi wapewe nafasi kuchangia katika uchumi wa nchi na kuepukana na uchumi dola nk,--- hiyo ni baadhi ya maendeleo ya watu kwanza baadaye ndipo maendeleo ya vitu yaje.