Pius Msekwa: Kwa mujibu wa Katiba, mpaka sasa Halima Mdee na wenzake hawana sifa za kuwa Wabunge

Pius Msekwa: Kwa mujibu wa Katiba, mpaka sasa Halima Mdee na wenzake hawana sifa za kuwa Wabunge

kesho kutwa chadema ipeleke majina stahiki wakaapishwe bungeni, hawa wasaliti warudi nyumbani wakalee familia
 
Spika Mstaafu wa Bunge, Pius Msekwa, amesema kwa mujibu wa katiba mpaka sasa Halima Mdee na wenzake 18, hawana tena sifa za kuwa wabunge

Kwa kuwa hawana chama kilichowapeleka Bungeni na hata wakihamia chama kingine hawawezi kupata nafasi hizo, labda mpaka uchaguzi ujao.

====

Mambo yameanza kuwa sio mambo.
@Pascal Mayalla umemsikia Mh Pius Msekwa
 
Hilo tunalijua vzr,na usifikiri Kama wao ni wajinga hawajui Sheria,ipo hv Jambo hili limefanyika makusudi na vyongozi wajuu wa chadema walilipa baraka japo hawawezi kukubali wanabakia wakisema nyaraka zimegushiwa,utakubaliana na mm kuwa tume inabarua ya uteuzi kutoka chadema na hiyo barua nikielelezo mahakamani kuwa wameonewa na kesi itaenda mahakamani na kusikilizwa chap shahidi no moja akiwa mwenyekit wa tume na ina tolewa hukumu ndani ya mwezi mmoja na bunge lijalo kina Halina ndani ya mjengo
Lazima utakuwa mtoto wa shehe yahya.
 
Msekwa karudia ukweli ambao uko wazi kabisa. Hata sisi tusio wanasheria tunajua hivyo. Basi tu serikali hii imeamua neno lake ndio liwe katiba na wala siyo katiba yenyewe. Nawashangaa sana akina Ndugai na Kilangi wanapotetea kuvunjwa kwa sheria kwa manufaa yao.

Kitu ambacho hawajui ni kuwa sheria ni msumeno. Wakati wanaambiwa kuwa ni vema kuwa na wagombea binafsi, kwa ubinafsi wao walipinga. Wakasema ili uwe "mchezaji ni lazima uwe na timu" - CCM kupitia Malecela. Leo msumeno unawakata upande wa pili...

Tutegemee mabadiliko makubwa sana ya sheria 2020-2025 ili kukidhi matakwa ya udhalimu wa CCM na Magufuli. Katiba itabadilishwa ili ktk scenarios kama hizi CCM na serikali waibuke mshindi. Itakuwa kama walivyobadili kanuni za uchaguzi wa 2020 ili kuruhusu wizi wa kura na kuwasimamisha wagombea wa upinzani kufanya kampeni.
 
Ajiandae kutukanwa na mboga mboga wenzake hususana mataga..mana anaenda kinyume na fikra za mwenyekiti.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kichekesho cha asubuhi,
Akihojiwa na Azam FM Radio, Propesa Kitila Mkumbo amedai kuwa hata baada ya kuvuliwa uanachama, akina Halima watakuwa wabunge wa Jamhuri. Lakini huyohuyo pia kawataka kwenda mahakamani kudai uanachama wao.
Hili famba halijui katiba inasemaje
 
Kama hawa akinadada wapo humu nawashauri wakaombe msamaha ktk chama chao.
Kwani hawatapoteza zaidi japokuwa mm ni ccm.
Wajipime waliko na wanakoelekea
Tatizo waliowabeba wamefanya hivyo kwa maslahi yao, hivyo hawawezi kuwaachia bunge libaki bila wa "upinzani" masharti ya dona kandri yanagoma.
 
Baadae atapigwa bati utasikia nilinukuliwa vibaya sikumaanisha hivyo 😅 😅 😅 😅
Mkuu Rudisha avatar picha yako tuliyokuzoea yule niga ana upara unaong'aa na sura ngumu
 
Ni kweli. Hili halina shaka. Lakini uhuni unaofanywa utabaki kwenye historia na utazidi kuwafunua watanzania, hasa wana CCM umuhimu wa kuchuja viongozi wa ngazi za juu kwa umakini. Juzi ´nilikuwa nazungumza na kiongozi mmoja aliyewahi kuwa kigogo nadani ya serikali na CCM na alikuwa na majuto kweli kweli hapa tulipofikia.
Huyo kigogo alisahau kuwa kila zama na shetani wake
 
Kwani kamaanisha yeye au ni vifungu vya katiba? Atapigwa biti kwani yeye ndio kaandika hiyo katiba? Hili ni suala la kikatiba uwe unataka au hutaki otherwise badilisha sheria.
Ndiyoo, yeye ndo aliandika katiba pamoja na wenzake.
 
Wawe wabunge wa mahakama kwa miaka mitano, ni sawa tu. Huko ndo kuwalinda kwa nguvu zote. Hivi hizi nguvu zilizotumika na zitakazoendelea kutumika ni kwa lengo lipi?
Kama hujui uongozi, ni vyema ukapumzika! Kuna divide and rule mweshimiwa! CCM wanapata ushindi bwelele kwa hili. Maana sasa baadala ya Amsterdam kuwananga CCM, Tototundu na chadema wapo busy kuondoa nyamaume aliye ndani. Wakisawazisha ya ndani, it will be too late. Hizo ndizo siasa za kimkakati mweshimiwa
 
Spika Mstaafu wa Bunge, Pius Msekwa, amesema kwa mujibu wa katiba mpaka sasa Halima Mdee na wenzake 18, hawana tena sifa za kuwa wabunge

Kwa kuwa hawana chama kilichowapeleka Bungeni na hata wakihamia chama kingine hawawezi kupata nafasi hizo, labda mpaka uchaguzi ujao.

====

Mambo yameanza kuwa sio mambo.
Ajue hatuko enzi za Nyerere, siku hizi mambo ya binge yako chini ya watu wawili, watimue bungeni na mimi nitawanyoosha huku.
 
Back
Top Bottom