Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 819
- 1,093
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeingia katika hatua ya ziada ya kuboresha ufanisi wa huduma na kupanua miundombinu ya bandari zake, huku ikilenga kukabiliana na ongezeko kubwa la meli na mizigo pamoja na kuimarisha ushindani wa bandari nchini katika soko la kimataifa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja yenye kaulimbiu 'Hatua ya ziada' Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA,Balozi, Ernest Mangu, amesema mafanikio yanayoendelea kupatikana katika bandari yameongeza mzigo wa kazi, hivyo watendaji wanapaswa kuongeza ufanisi kuendelea kuimarisha imani ya watumiaji wa bandari.
Aidha Balozi Ernest Mangu amesema ongezeko la mizigo limekuwa likisababisha changamoto nyingine, ikiwamo msongamano wa malori katika barabara zinazoelekea bandarini na vituo maalumu vya kuhifadhi na kushughulikia mizigo (ICDs), hivyo aliwataka TPA, wasafirishaji na wadau wa sekta ya logistiki kushirikiana kutafuta suluhisho la kero hizo.
Amesema TPA inapaswa kutumia ubunifu na kuangalia mapungufu ya kiutendaji ndani ya taasisi badala ya kutegemea zaidi kutafuta wateja wapya, akisema kuwa ufanisi wa huduma ndiyo msingi wa kuendelea kuvutia na kuhifadhi wateja wa bandari.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa amesema kaulimbiu hiyo inataka watendaji kwenda zaidi ya kutekeleza wajibu wa kawaida kwa kusikiliza wateja, kutoa taarifa kwa wakati, kutatua changamoto kwa haraka na kufanya zaidi ya matarajio yao.
Amesema mafanikio ya TPA yameanza kuonekana katika viashiria vya kimataifa, ambapo Bandari ya Dar es Salaam imepanda kutoka nafasi ya 360 hadi 255 katika ufanisi wa kuhudumia makasha, hatua hiyo imechangiwa na maboresho ya miundombinu na utendaji wa wadau mbalimbali wa mnyororo wa biashara.