Hivi DP WORLD wanatoa sadaka huko MISIKITINI???Kama ninavyowaona PhD za kukusanya sadaka , hii habari hawaitaki kabisa , adui wao ni mwarabu tu hata awe upande wao.
Sasa kwa nn mlikuwa mnatusakama sisi , waulize ndugu zako ..Wengine wanadai kwamba wamekuja kusambaza uislamu wakati hawa uhusiano zaidi ya kupiga kazi .Hivi DP WORLD wanatoa sadaka huko MISIKITINI???
Maana kila ukikutana na SHEIKH au MUUMINI wa BAKWATA mnavyokaza CUVU kuwatetea utashagaa?
Au kwasababu mmeambiwa ni kampuni ya MWARABU???
Yaani kwa TZ, DP WORLD hawahitaji hata Afisa Masoko, kwa mnavyoitetea.
Mkuu Pfizer, shukrani kwa kuleta taarifa hii hapa jukwaani. Hata hivyo, tunapaswa kuitazama taarifa hii kwa jicho la tahadhari na uhakiki wa kina badala ya kusherehekea mapema. Hapa kuna mambo ya msingi ya kuzingatia:MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeingia katika hatua ya ziada ya kuboresha ufanisi wa huduma na kupanua miundombinu ya bandari zake, huku ikilenga kukabiliana na ongezeko kubwa la meli na mizigo pamoja na kuimarisha ushindani wa bandari nchini katika soko la kimataifa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja yenye kaulimbiu 'Hatua ya ziada' Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA,Balozi, Ernest Mangu, amesema mafanikio yanayoendelea kupatikana katika bandari yameongeza mzigo wa kazi, hivyo watendaji wanapaswa kuongeza ufanisi kuendelea kuimarisha imani ya watumiaji wa bandari.
Aidha Balozi Ernest Mangu amesema ongezeko la mizigo limekuwa likisababisha changamoto nyingine, ikiwamo msongamano wa malori katika barabara zinazoelekea bandarini na vituo maalumu vya kuhifadhi na kushughulikia mizigo (ICDs), hivyo aliwataka TPA, wasafirishaji na wadau wa sekta ya logistiki kushirikiana kutafuta suluhisho la kero hizo.
Amesema TPA inapaswa kutumia ubunifu na kuangalia mapungufu ya kiutendaji ndani ya taasisi badala ya kutegemea zaidi kutafuta wateja wapya, akisema kuwa ufanisi wa huduma ndiyo msingi wa kuendelea kuvutia na kuhifadhi wateja wa bandari.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa amesema kaulimbiu hiyo inataka watendaji kwenda zaidi ya kutekeleza wajibu wa kawaida kwa kusikiliza wateja, kutoa taarifa kwa wakati, kutatua changamoto kwa haraka na kufanya zaidi ya matarajio yao.
Amesema mafanikio ya TPA yameanza kuonekana katika viashiria vya kimataifa, ambapo Bandari ya Dar es Salaam imepanda kutoka nafasi ya 360 hadi 255 katika ufanisi wa kuhudumia makasha, hatua hiyo imechangiwa na maboresho ya miundombinu na utendaji wa wadau mbalimbali wa mnyororo wa biashara.
View attachment 3684392View attachment 3684393View attachment 3684394View attachment 3684395View attachment 3684396View attachment 3684397View attachment 3684398View attachment 3684399View attachment 3684400View attachment 3684401View attachment 3684402View attachment 3684403View attachment 3684404View attachment 3684405View attachment 3684406View attachment 3684407View attachment 3684408View attachment 3684409View attachment 3684410View attachment 3684411View attachment 3684412
Mkuu Tanganian 🎪🤡, pole sana kwa kuona vizuka vya udini kila mahali! Yaani badala ya kujadili uchumi wa nchi, mifumo ya TEHAMA, na foleni za malori barabarani, wewe akili yako yote inawaza sadaka na kwaya? 🤦♂️Kama ninavyowaona PhD za kukusanya sadaka , hii habari hawaitaki kabisa , adui wao ni mwarabu tu hata awe upande wao.
Nchi imejaa siasa kila Kona.
Mkuu, hoja yako ya kusubiri ushahidi ni sahihi, lakini haiwezi kutumika kufuta ushahidi uliopo sasa. Kama CPPI imeonyesha kupanda kwa nafasi ya Bandari ya Dar es Salaam, hilo ni jambo linalopimika kwa vigezo vilivyowekwa na ripoti hiyo; huwezi kulipuuza kwa kusema “tusubiri CAG,” kwa sababu CAG haikagui wala kuamua nafasi ya bandari kwenye CPPI. Vivyo hivyo, ukweli kwamba bandari shindani zilishuka hauondoi moja kwa moja maboresho yaliyofanyika Dar es Salaam.Mkuu Pfizer, shukrani kwa kuleta taarifa hii hapa jukwaani. Hata hivyo, tunapaswa kuitazama taarifa hii kwa jicho la tahadhari na uhakiki wa kina badala ya kusherehekea mapema. Hapa kuna mambo ya msingi ya kuzingatia:
Ushauri wa Balozi Mangu kuwa TPA ijikite kurekebisha mapungufu ya ndani badala ya kukimbilia kutafuta wateja wapya ndio msingi wa kila kitu. Tusubiri ripoti za wakaguzi huru na uhalisia wa mifuko yetu ndipo tupongeze.
- Ni Mapema Mno Kusherehekea (Historia Inatufundisha): Tumeshasikia kauli na ripoti nyingi za namna hii huko nyuma zilizosifu ufanisi mkubwa wa mashirika yetu ya umma, lakini baada ya muda hali halisi uwanjani inakuja kuwa tofauti kabisa. Kupanda kwa nafasi kwenye makaratasi ni jambo moja, lakini uendelevu wa ufanisi huo katika uhalisia wa kila siku ni jambo jingine.
- Tusubiri Ripoti ya CAG: Ukweli kamili wa kama ufanisi umebadilika na una tija ya kiuchumi utajulikana pale Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) atakapokuja na ripoti yake ya ukaguzi wa kiutendaji (Performance Audit). CAG ndiye atakayethibitisha kama kupanda huku kwa nafasi kunaendana na ongezeko la kweli la mapato na kupungua kwa mianya ya upotevu, au ni mikakati tu ya "wapiga debe" kujaza watu upepo ili kutuliza hasira na manung'uniko ya wananchi yaliyotokana na mijadala ya hivi karibuni ya uendeshaji wa bandari yetu kupewa DP World.
- Mtego wa Takwimu za CPPI za Nyuma: Tukizitazama takwimu hizi za Benki ya Dunia (CPPI) kwa miaka ya nyuma, utaona graph yetu haijawahi kuwa imara—tunapanda leo, kesho tunaporomoka. Mara nyingi kupanda kwetu kunachangiwa pia na kuporomoka kwa ufanisi wa bandari shindani za ukanda huu (kama Mombasa au Durban), na si kwa sababu mifumo yetu ya ndani imekamilika kwa asilimia 100.
- Changamoto ya Nchi Kavu (Hinterland Logistics): Kauli ya Mwenyekiti wa Bodi kuhusu msongamano mkubwa wa malori kuelekea bandarini na kwenye vituo vya ICDs inathibitisha hoja ya wadau wa logistiki (kama TAFFA). Inakuwaje bandari isifiwe kuwa na kasi ya kushusha makasha kutoka kwenye meli, lakini makasha hayo hayo yakamilishe wiki mbili nchi kavu yakisubiri mifumo ya TEHAMA (kama TANCIS) au kukwama kwenye foleni ya barabarani? Ufanisi wa bandari unapimwa kwa mnyororo mzima kuanzia baharini hadi mzigo unamfikia mlaji.
Hivi DP WORLD wanatoa sadaka huko MISIKITINI???
Maana kila ukikutana na SHEIKH au MUUMINI wa BAKWATA mnavyokaza CUVU kuwatetea utashagaa?
Au kwasababu mmeambiwa ni kampuni ya MWARABU???
Yaani kwa TZ, DP WORLD hawahitaji hata Afisa Masoko, kwa mnavyoitetea.
Hata wewe comment yako imetawaliwa na chuki ya udini,Tatizo la Bongo, mtu akiwa anaswali Msikitini basi anafikiri na yeye ni Mwarabu .... hakubali mtu amseme Mwarabu vibaya hata kama anakosea. Hili tatizo la kuhusisha dini na Waarabu naona linaiharibu sana Tanzana.
Mkuu Pfizer, shukrani kwa majibu yako yenye mtazamo chanya na hoja inayofikirisha. Ni kweli kabisa kuwa vigezo vya CPPI ni vya kisayansi na vina umuhimu wake katika kupima kasi ya upakuaji mizigo melini. Nia yangu haikuwa kupuuza takwimu hizo, bali kuweka angalizo la msingi kuhusu namna tunavyopaswa kuzipokea kwa tahadhari.Mkuu, hoja yako ya kusubiri ushahidi ni sahihi, lakini haiwezi kutumika kufuta ushahidi uliopo sasa. Kama CPPI imeonyesha kupanda kwa nafasi ya Bandari ya Dar es Salaam, hilo ni jambo linalopimika kwa vigezo vilivyowekwa na ripoti hiyo; huwezi kulipuuza kwa kusema “tusubiri CAG,” kwa sababu CAG haikagui wala kuamua nafasi ya bandari kwenye CPPI. Vivyo hivyo, ukweli kwamba bandari shindani zilishuka hauondoi moja kwa moja maboresho yaliyofanyika Dar es Salaam.
Kama una ushahidi kwamba nafasi hiyo imetokana na “wapiga debe,” au kwamba takwimu hizo si sahihi, ni bora ulete ushahidi huo badala ya kugeuza dhana kuwa hitimisho. Kukosoa ni muhimu, lakini kukosoa taarifa kunahitaji ushahidi unaopingana nayo.
Mkuu, hili ni swali zuri sana linalogusa saikolojia ya jamii, na ni muhimu tulitazame kwa mapana yake badala ya kuishia kwenye dhana ya "kuchukia nchi". Kimsingi, hakuna Mtanzania mwenye akili timamu asiyetamani kuona nchi yake inapiga hatua; sote tunasafiri barabarani, tunahitaji huduma za afya, na tunapenda sifa njema ya taifa letu.Kwanini kuna wabongo hua wanachukia maendeleo ya nchi yao wao wenyewe? Yani unakuta mtu akisikia jambo jema au mafanikio kwenye nchi yake anakua anapandisha na hasira?
Hivi hii hua inasababishwa na nini? Wataalamu wa Saikolojia labda mtusaidie kwenye hili,hua nashangaa sana!
Mkuu mdogoee, hapo umezungumza jambo la msingi sana na kwa mtazamo wa kiweledi kabisa. Hakuna anayekataa kuwa ongezeko la ufanisi kutoka nafasi ya 360 hadi 255 katika ripoti ya CPPI ni hatua inayopimika na ni kiashiria chanya kwa uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.Imekuwa Siasa tena mambo ya Mafanikio ya Kiuchumi kutoka 360 kuja 255
Tunapaswa kujivunia uhongozi bora chini ya Rais DKT Samia Suluhu Hassan ✍️
Hakuna mtu anachukumua maendeleo.Kwanini kuna wabongo hua wanachukia maendeleo ya nchi yao wao wenyewe? Yani unakuta mtu akisikia jambo jema au mafanikio kwenye nchi yake anakua anapandisha na hasira?
Hivi hii hua inasababishwa na nini? Wataalamu wa Saikolojia labda mtusaidie kwenye hili,hua nashangaa sana!
Mkuu umejibu vizuri sana na nimekuelewa vizuri tu,ila huenda kuna mambo mengine ambayo yapo nje ya hizo sababu ulizo ziweka,Mkuu, hili ni swali zuri sana linalogusa saikolojia ya jamii, na ni muhimu tulitazame kwa mapana yake badala ya kuishia kwenye dhana ya "kuchukia nchi". Kimsingi, hakuna Mtanzania mwenye akili timamu asiyetamani kuona nchi yake inapiga hatua; sote tunasafiri barabarani, tunahitaji huduma za afya, na tunapenda sifa njema ya taifa letu.
Kisaikolojia na kiutendaji, kile kinachoonekana kama "hasira" au "kupinga" mara nyingi husababishwa na mambo makuu mawili:
Kuhimiza uwazi, uwajibikaji, na usahihi wa takwimu si kuichukia nchi. Ni namna ya kuhakikisha kuwa "mafanikio" tunayoambiwa kwenye majukwaa yanaakisi uhalisia wa maisha ya kila siku ya mwananchi wa kawaida. Uzalendo wa kweli unaenda sambamba na kuhoji ili kulinda maslahi ya kizazi cha sasa na kijacho.
- Uzoefu wa Kuaminishwa Visivyo na Ubadhirifu wa Rasilimali (Trust Deficit & Economic Alienation): Wananchi wengi hawapingi maendeleo, bali wanahoji uwasilishaji wake na matokeo ya usimamizi wake. Katika saikolojia ya jamii, watu wanapoona ripoti za kila mwaka za CAG zikifichua ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma, mikataba mibovu, na upotevu wa rasilimali, huku wao wenyewe wakikabiliana na ugumu wa maisha ya kila siku, inatengeneza hali ya kisaikolojia inayoitwa Economic Alienation (hisia ya kutengwa kiuchumi). Hasira inayojitokeza haitokani na chuki kwa nchi, bali ni matokeo ya wananchi kuona kuwa "keki ya taifa" inanufaisha kikundi kidogo cha watu wachache, huku wao wakiachwa pembezoni. Hali hii inajenga mfumo thabiti wa kujilinda unaoitwa Skepticism (tahadhari ya kutoamini haraka), ambapo hata habari njema za maendeleo zinapokuja, zinapokelewa kwa mashaka makubwa kwa hofu ya kupotoshwa tena kama ilivyowahi kutokea huko nyuma (kama vile kuambiwa miradi inatekelezwa kwa fedha za ndani pekee lakini baadae ripoti za ukaguzi zikaonyesha mikopo mikubwa).
- Giza Kwenye Mikataba na Maeneo ya Kimkakati: Ili jamii iwe na umiliki (ownership) na ushabiki wa dhati wa mafanikio, inahitaji uwazi. Wakati maeneo muhimu ya mikataba ya kimkakati yanapowekwa siri, au yanapoacha maswali mengi kuliko majibu, kisaikolojia inatengeneza hisia za kutoshirikishwa (disenfranchisement). Wananchi wanapohisi kuna kitu kinafichwa kwenye rasilimali zao za urithi wa kitaifa, wanakuwa na haki ya kuwa na tahadhari, na tahadhari hiyo isitafsiriwe kama chuki.
Bakwata inaingiaje hapa kwenye comment yangu? Kama umegombana na mumeo basi hasira zako usiniletee mimi,malizana nae huko huko chumbani kwenu.Hakuna mtu anachukumua maendeleo.
Watu aanahitaji kujua mkataba kati ya serikali na DP WORLD ukoje.
Msilete sfori za kibakwata hapa
Siasa za kishambaKwanini kuna wabongo hua wanachukia maendeleo ya nchi yao wao wenyewe? Yani unakuta mtu akisikia jambo jema au mafanikio kwenye nchi yake anakua anapandisha na hasira?
Hivi hii hua inasababishwa na nini? Wataalamu wa Saikolojia labda mtusaidie kwenye hili,hua nashangaa sana!