Ukisoma juu ya maisha yake (upande wa ufanyaji biashara), utaona ugumu wa kupambana na biashara ya mihadarati,taasisi na maofisa wa serikali ni part of the business. Kuna mdunguaji wake aliwahi kukamatwa akasema "Biashara hii haina mshindi na haiwezi kuisha maana ni biashara ya fedha nyingi".
Kwa mujibu wa KAKA YAKE ambaye ndiye alikuwa mhasibu wa biashara zake, they spent USD 1000 per week kununua mipira ya kufungia pesa (rubber band). Na kwa kuwa pesa nyingi na haikuwa safe zote kuziweka bank, walificha katika gharama maalumu ambapo kila mwaka 10% ya pesa zilikuwa zimeharibika kwa kuoza kwa unyevu au kuliwa na wadudu au panya