zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 20,537
- 31,729
1. Kwanza inaonekana hujui maana ya sampling kwenye takwimu ni upuuzi kudhani wanaotumia social network hawapo kitaa!! Ndio maana sampling inakupa picha tu ya the remaining population ambayo kma ikipata smartphone ingetoa maoni gani. Jiuliza mange kuwa na followers 4M toka aanze kuikosoa serikali inakupa picha gani?? Kweli haireflect kitaa? Hao 4M wapo nchi gani? Hawana friends wa kuwashawishi?Ili aweze kufahamika nje ya mitandao ya kijamii inabidi mfanye kazi kubwa maana asilimia kubwa (>70%) ya wapiga kura hawana simu janja.
Isitoshe kumuuza kwa wapiga kura ni ngumu kwa sababu hakuna alilofanya la kitaifa hata jimboni kwake wanajuta kumchagua kwa vipindi viwili mfululizo.
2. Kuhusu siasa za kitaifa, ni mpuuzi tu atakosoa mchango wa Lissu kwenye siasa za bunge. Kama uliona mjadala wa sheria ya cybercrime/Gesi, ripoti za CAG, Mpango wa taifa wa 5 years basi una haki ya kusema hana alilofanya ila wote wanafahamu hakuna muswada wa CCM uliwahi pita bila kupitia mchujo wa hoja za Lissu. Kwa hili tumpe credit hta kma wamchukia. Na nikwambie tu Leo akienda CCM atapewa uwaziri na ww hutokua na lakufanya zaidi ya kupiga makofi tu.
3. Jimboni kwake hawamtaki?? Lissu ndio mpinzani pekee ambaye uchaguzi serikali za mitaa wa mara ya mwisho upinzani wanashiriki alipata 98% ya serikali za vijiji then unasema walimchoka?? Kwa data zipi mkuu? Nlikuwepo huko Ikungi january huyo mbunge wa CCM hana ushawishi kabisa na yye anajia tu kashika jimbo kimaguvu tu ila come october atapisha tu kwa nguvu ya sanduku.
Na ndio maana aliwapa challenge leo Maalim kma mnakubalika sana kwanini mnaogopa uchaguzi huru na haki?? Jibu ni Mnafahamu akisimama atapukutisha CCM vipande pande kwa facts!!
Turudi wakati wa kampeni utakuwa umenielewa nachosema