PM Majaliwa anafahamu maana ya uwajibikaji? Ajali 3 kubwa zimetokea ofisi yake imeshindwa kuokoa watu lakini yupo tu

Rekebisha hiyo miaka mkuu

Halafu huwa hakuna utaratibu wa kuacha kazi huko na hawajali
Kwanza watakushangaa ingawa kila leo tunataka watu wawajibike ila kama hakuna sheria hiyo ya kujiuzuru
 
Na nyinyi wananchi mnatakiwa kujitafakari, kwanini miaka nenda rudi mnakubali kutawaliwa na watu ambao akili zao zimeshachoka kuzalisha suluhu ya matatizo ya jamii zenu.
 
Baba Kibonge Vitenge Kangomba Diblo Dibala miyeyusho sana!!!
Masuala ya Disaster Management yapo Ofisi yake lakini chenga tupu.
 
Nani atakusaidia haya maisha upo mwenyewe aliokufa tuwaombee tu hakuna namna eti Mimi walimuacha Mzee wangu ICU halafu walipokuja wanasema anapelekwa kcmc na bado kcmc ambulance ilichelewa kufika yaani maisha kumpeleka walahawajielewi tumelipa 1.2ml ya ambulance ambulance yenyewe imezeeka inanuka uvundo ila selian ni ujinga tu ndio upo kufika Sasa huko kcmc hawajielewi baba yangu akifariki Kwa ujinga wa manesi na madaktari bado muhimbili nawao wanasema wampe dawa za maumivu Kwa maana daktari bingwa hayupo anakuja baada ya wiki mbili kiforce life akaletwa mwingine akamfanyia operation weh kumbe naye hajielewi nakumbuka wiki tatu baadae nipo kwenye mitihani naambiwa Mzee hatunaye Tena kafariki alikufa tarehe 14/10/2008 hapo bado mie Binti mdogo sana .

Hakuna wakunilipia ada Wala Nini mateso ndio yakaanzaga hapo nililia sana .
Kwani ndugu walichukua kila kitu Wana choona kinafaa na mengi yalitokea .


So Kwa serikali hii hakuna misaada All in All ni Mungu pekee ndio anaweza kukusaidia yeye ndiye anayeweza kukuepushia jambo lolote liwe gumu au rahisi .

Kufiwa jambo baya unamwona baba Yako Kawa mweusi kwenye jeneza na unaambiwa muage mara ya mwisho aloo ....
Humuoni Tena hapo hujui hata ulie kwanini bado gundu huu ya gundu uachwe na kimeo pia .

Eti anaona humfai wewe kufiwa ni jambo ambalo ni baya sana
 
Pole sana mkuu,
 
2028?
 
Kesho ofisi yake itatoa majeneza 19 bure ndo kazi anaweza.
 
Kuanzia huyo cha uongo mpaka piko kichwani mpaka Vasco Da Gama ambae ndio kiongozi wake wote wapumzishwe tu. Wameshindwa kutumikia nafasi zao.
 
Majaliwa mnamuonea jamaniiii.Mbona yakitokea mazuri hasifiwi??anasifiwa mwingine na yule anayeogelea sifa mnataka na hili hasilaumiwe?

Mfumo wa utawala tanzania ni maamuzi ya mtu mmoja kwa hiyo wengine wanakuwepo kama vivuli.
KATIBA KATIBA KATIBA sivyo tutaendelea na haya majanga wakiangalia na kusifia na
Kesho wataunda tume!?!!
 
Kwani majaliwa ndo kasababisha ajali ?
 
Kwahy yeye ndio kasababisha hizo ajali mbona hukusema magufuli aachie ngazi ilivyotokea ile ya MV ukerewe au umeona majaliwa tu ndio wa kuachia ngazi
Hao achana nao Wana agenda zao behind , ajali ni kificho tuu
 

Tukipatwa na Mafuriko au janga la Tetemeko kama timu ya maafa iliyo chini ya Waziri Mkuu Response yake ipo hivi wote tutakuwa pamoja na meko mbinguni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…