PM Majaliwa anafahamu maana ya uwajibikaji? Ajali 3 kubwa zimetokea ofisi yake imeshindwa kuokoa watu lakini yupo tu

PM Majaliwa anafahamu maana ya uwajibikaji? Ajali 3 kubwa zimetokea ofisi yake imeshindwa kuokoa watu lakini yupo tu

Hayo mazuri ni wajibu wake anatimiza, tuache kuwa watu wa kujikomba kwa watawala.
Majaliwa mnamuonea jamaniiii.Mbona yakitokea mazuri hasifiwi??anasifiwa mwingine na yule anayeogelea sifa mnataka na hili hasilaumiwe?

Mfumo wa utawala tanzania ni maamuzi ya mtu mmoja kwa hiyo wengine wanakuwepo kama vivuli.
 
Kwa sababu wameshika na kuchimbia mizizi yao kwenye vyombo vyote vya dola.
Na nyinyi wananchi mnatakiwa kujitafakari, kwanini miaka nenda rudi mnakubali kutawaliwa na watu ambao akili zao zimeshachoka kuzalisha suluhu ya matatizo ya jamii zenu.
 
Majaliwa mnamuonea jamaniiii.Mbona yakitokea mazuri hasifiwi??anasifiwa mwingine na yule anayeogelea sifa mnataka na hili hasilaumiwe?

Mfumo wa utawala tanzania ni maamuzi ya mtu mmoja kwa hiyo wengine wanakuwepo kama vivuli.
Uko sahihi ila kweli kweli Waziri Mkuu Majaliwa hawezi kuwajibika hata kwa 30% kweli ? katika hali ya DHARULA? YEAH HE IS VERY HUMBLE PERSON LAKINI SIYO MUWAJIBIKAJI KABISA KABISA .
 
Mbona yule chifu wa mchongo kutoka zenji hamumwambii ajiuzulu?
 
uwajibikaji ni yeye kusafiri kwa ndege kwenda kuzika na kuaga miili.
 
PM Majaliwa ana roho ngumu sana. Na ninadhani anatuona wananchi kama wanyama tu. Kwann hawajibiki pale maovu na uzembe vinapotokea kwenye serikali?

Au hatambui maana ya cheo ni dhamana?

2020 Mv Ukerewe iliua watu wengi yeye akiwa waziri mkuu. Shughuli za uokozi zilikuwa za kiwango cha chini kiasi cha kutia aibu. Majaliwa yupo tu!

2020... Ajali ya moto Msamvu iliuwa watu zaidi ya 100. Uokoaji ulifanyika kizembe na hata tiba za watu wale hazikuwa za kiwango cha kitaalamu Majaliwa yupo tu.

Leo 06/11/2020 ajali ya ndege ya Precision imetokea na kuua watu 19. Huku uokoaji ukiwa imetawaliwa na dhihaka ya kiwango cha SGR..... Majaliwa yupo tu.

Are the tanzanians subjects or objects? Why leaders are not accountable?

Eti sasa tunaqmbiwa serikali inaandaa mazishi ya heshima kwa marehemu wa ajali ya ndege. Hatutaki mazishi ya heshima, tunataka maisha yalindwe kwa heshima

View attachment 2408822
View attachment 2408823

Anahitaji kukumbushwa kidogo.
 
Kuna watu humu ni mabox kabisa. Kuwajibika kwa waziri mkuu ni lazima kwa sababu shughuli hizi zinaratibiwa na ofisi yake. Tuna ujinga mwingi kama taifa.
 
Watu weusi mpaka tufikie kuwa binadamu kamili ni mchakato mrefu. Bado tupo kwenye muundo wa namna yetu wa kipekee hapa ulimwenguni.
 
Nani atakusaidia haya maisha upo mwenyewe aliokufa tuwaombee tu hakuna namna eti Mimi walimuacha Mzee wangu ICU halafu walipokuja wanasema anapelekwa kcmc na bado kcmc ambulance ilichelewa kufika yaani maisha kumpeleka walahawajielewi tumelipa 1.2ml ya ambulance ambulance yenyewe imezeeka inanuka uvundo ila selian ni ujinga tu ndio upo kufika Sasa huko kcmc hawajielewi baba yangu akifariki Kwa ujinga wa manesi na madaktari bado muhimbili nawao wanasema wampe dawa za maumivu Kwa maana daktari bingwa hayupo anakuja baada ya wiki mbili kiforce life akaletwa mwingine akamfanyia operation weh kumbe naye hajielewi nakumbuka wiki tatu baadae nipo kwenye mitihani naambiwa Mzee hatunaye Tena kafariki alikufa tarehe 14/10/2008 hapo bado mie Binti mdogo sana .

Hakuna wakunilipia ada Wala Nini mateso ndio yakaanzaga hapo nililia sana .
Kwani ndugu walichukua kila kitu Wana choona kinafaa na mengi yalitokea .


So Kwa serikali hii hakuna misaada All in All ni Mungu pekee ndio anaweza kukusaidia yeye ndiye anayeweza kukuepushia jambo lolote liwe gumu au rahisi .

Kufiwa jambo baya unamwona baba Yako Kawa mweusi kwenye jeneza na unaambiwa muage mara ya mwisho aloo ....
Humuoni Tena hapo hujui hata ulie kwanini bado gundu huu ya gundu uachwe na kimeo pia .

Eti anaona humfai wewe kufiwa ni jambo ambalo ni baya sana

Kweli kabisa Kiongozi,Pole Sana
 
Back
Top Bottom