PM Majaliwa: Bwawa la umeme kukamilika Juni 2022

PM Majaliwa: Bwawa la umeme kukamilika Juni 2022

Diary yangu.... Mwezi wa June 2022. Nikiwa hai nitafuatilia
 
Sina tatizo na hii project kabisa ila sina imani kabisa na wanasiasa wa ccm, hizi calculations tulishapigiwa sana lakini hakuna tulichoambulia.

Lakini pia tukipiga hesabu hizo lazima tujue kuwa Hydro inaonekana ina bei nafuu kwa sababu gharama za uharibifu wa mazingira haziingizwi kwenye hizo hesabu.

Ni kama vile mkaa unaonekana ni nafuu kuliko gesi kwa sababu gharama za deforestation haziingizwi kwenye bei. Tungekuwa tunajumuisha na gharama ya kupanda upya miti na athari katika tabia nchi, bei ya mkaa isingeshikika.

ghalama za uhalibifu wa mazingira yapi??

ukitaka hivyo hata barabara itapigiwa hesabu za uharibifu wa mazingira halafu maana itapotea kabisa.
 
Mh!naikumbuka gesi ya mtwara,tulijidai nayo kuwa inakuja kumaliza matatizo ya umeme nchi lakini kilichotokea kila mmoja wetu anajua[emoji45][emoji45][emoji45]
Aliekwambia si yupo,mbona hamumuulizi na kwenye misiba yupo anaonekana.
 
Tuseme kuwa PM bado hajapangwa? Maana hawa tayari:
Mama yetu, Ndugai na Wabunge wanafiki na vilaza washasetiwa tayari ili team Msoga iingize vitu vyake.
Ukimuangalia PM ni kama vile ule mtandao wakumchafua Magu ashaushitukia, na ndiyo kiongozi mwandamizi pekee ninayemuona hajatoka kwenye line, swali linabaki moja, atauweza huu mtandao uliomua Magufuli?
Wewe tangu Magu atutoke, sisikii tena TANZIA. Washenzi hawa walizitumia ili kumflustrute our hero.

R.I.P mwamba
Mkuu, tanzia ni kweli hazitangazwi kama kipindi kile! Sasa ni kwamba watu/maaskofu hawafi? Au wakifa hawatangazwi?

Mimi kwa upande wngu naona misiba imepungua sana baada ya kushindwa na kufa kwa yule muovu"
 
Heshima ya mama Samia amalize miradi hiyo miwili SGR na STIEGLER GORGE. Kinyume cha hapo atazua hasira za utanganyika kama mzee Mwinyi vs Malecela kusapoti ssrikali tatu. Mama Samia ajue ameshika check kike kwa mapenzi ya Mungu lakini kwa mechanism ya ccm hakuna mzanzibar angetawala Tanzania tote. Akitawala vyema ana nafasi ya kutuondolea umajimbo wa watanzania bars. Lakini akicheza kete vibaya na muungano utavunjika mikonkni masks. Maswala yanayoleta uchumvu ni kuwapa wawekezaji madini yetu kwa mikataba mibovu. Kuchimba gas yetu kwa mikataba ya ovyo. Watanzania bara hawatavumila rais mzanzbari acheze madini na mali za serikali kama mzee Mkapaalivyobinafsizha mashirika yetu. Hata harmonization ya ushuru wa bara na visiwani aende kea tahadhari asionekane kutuuza kea wavisiwani kwakd. Namalizia , mama Samia ni chaguo la Mungu ,anatarajiwa atende kila jambo kwa mapenzi ya Mungu. Akifanya hivyo atatuunganizha ,sasa tanganyika ilivubikaa na ukabila na ujimbo yuko nafasi nzuri ya kutuunganisha.
Mkalimani anahitajika hapa.
 
Wataalamu wanisaidie, Kidatu, Kihansi, Hale (1& 2) na Nyumba ya Mungu ambao wanazalisha umeme wa maji kwa pamoja wanazalisha mw ngapi? Na mitambo isiyotumia maji inazalisha kiasi gani?
Kwa sasa watumiaji wadogo (wanyonge) wanalipa karibu shilingi 100 kwa unit. Kutoka Shilingi 36 hadi 100 ni parefu.
 
Wanaopinga mradi huu ni mafisadi ambao wamepewa fedha na mabeberu kwa ajili ya gas ha mtwara na symbion.

Waziri mkuu wa Tanzania Bwana Majaliwa leo ametembelea mradi wa ujenzi wa bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere na kuangalia maendeleo ya ujenzi.

Majaliwa ameridhika na kasi ya ujenzi wa mradi huo na amesisitiza utakamilika kwa wakati mwaka 2022 mwezi wa 6 kama majubaliano yalivyo.

PM amesema mradi utakamilika kama ilivyopangwa kwani pesa zipo hakuna sababu ya kuchelewesha mradi.

PM amasema mradi huo utatoa faida kubwa kwa uchumi wa nchi yetu kwani mradi utaleta umeme wa bei nafuu sana kwa watanzania.

Kwa wasiojua.
Kuzalisha Unit moja ya umeme wa maji hua ni TZS 36, Nuclear TZS 66, Jua TZS 105, Joto Ardhi TZS 114.5, Gas 150 na Mafuta mazito 460.

Kwa kuangalia hizo unit price unaona wazi kabisa kua hakuna source yoyote ya nishati yenye gharama ndogo kama maji.

 
Gas ya mtwara imesha chukuliwa na mabeberu na dalali wao ni muhongo.
Mh!naikumbuka gesi ya mtwara,tulijidai nayo kuwa inakuja kumaliza matatizo ya umeme nchi lakini kilichotokea kila mmoja wetu anajua[emoji45][emoji45][emoji45]
 
Sequel ya Stori ya kusisimua -"trillioni ya cubic feet gesi" coming soon too a theatre near you "maelfu ya megawati umeme"
 
Heshima ya mama Samia amalize miradi hiyo miwili SGR na STIEGLER GORGE. Kinyume cha hapo atazua hasira za utanganyika kama mzee Mwinyi vs Malecela kusapoti serikali tatu. Mama Samia ajue ameshika cheo kile kwa mapenzi ya Mungu lakini kwa mechanism ya ccm hakuna mzanzibar angetawala Tanzania yote. Akitawala vyema ana nafasi ya kutuondolea umajimbo wa watanzania bara. Lakini akicheza kete vibaya na muungano utavunjika mikononi mwake Maswala yanayoleta uchungu ni kuwapa wawekezaji madini yetu kwa mikataba mibovu. Kuchimba gas yetu kwa mikataba ya ovyo. Watanzania bara hawatavumila rais mzanzbari achezee madini na mali za serikali kama mzee Mkapaalivyobinafsisha mashirika yetu. Hata harmonization ya ushuru wa bara na visiwani aende kwa tahadhari asionekane kutuuza kwa wavisiwani kwake. Namalizia , mama Samia ni chaguo la Mungu ,anatarajiwa atende kila jambo kwa mapenzi ya Mungu. Akifanya hivyo atatuunganisha ,sasa tanganyika iligubikwa na ukabila na ujimbo, yuko nafasi nzuri ya kutuunganisha.
 
Hivi unafikiri transformer, Generators na control system zote zitafungwa za mwaka 70 kwa akili yako!!?..[emoji3][emoji3]Labda CAG yeye mwenyewe au team yake hawako compitent juu ya feasibility study ya mradi wowote wa umeme, wanaposema imetumika feasibility ya miaka ya 70 sijui wameisoma vyema hiyo feasibility ilichokuwa inakihitaji kitimie na ingetumika kwa miaka mingapi kutoka wakati huo na je! Hizo MW2100 zitakazozalishwa na mradi huo hazitaleta ongezeko chanya la umeme kwenye mfumo wetu wa sasa wa umeme!?.
sawa wataweka electrical generating system ya hivi sasa lakn mabadiliko ya tabia nchi tangu kipindi hicho mpaka hv sasa ni bora wangeacha tu ile Hifadhi ya Selous kuliko kuiharibu bureee [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nami naona shida Sio feasibility study ya miaka 70, naona ni kuisha..

kama hiyo ya miaka ya 70 inatekelezeka kwanini tuangaike tena kupata 2017?

Nilitegemea CAG aitumie elimu yake kuweka mambo bayana mfano mradi hautafanya kazi KWA kwa sababu feasibility study ya miaka 70 na si kutajataja tu...
Wangeupdate feasibility study tungejiridha maan hapa tulipo kama tunabet
 
Back
Top Bottom