Point za madaraja - Matokeo ya form four yako kisiasa zaidi

Hivi hawa baraza la mitihan (NECTA) wametuona sisi watanzania ni wajinga kiasi cha kwamba wanatuganya waziwazi namna hii!

Yaana wanadriki kutuambia asilimia ya ufaulu umeongezeka kwa asilimia 15.kwa kulinganisha na ufaulu upi?

Ina maana ufaulu wa sasa wa mwanafunzi kuwa na DIV -IV -42 ndo wanataka waulinganishe na ule wa mwaka jana ambapo mwenye div -iv-34 ilikuwa ni ziro?

Na kama A ya mwaka jana ilianzia na 81 ndo wame compare na A ya kuanzia 71!?

Sasa kama ni hivyo basi watangaze sis tuliosoma miaka ya nyuma turudishe vyeti vibadilshwe kwendana na ufaulu wa sasa.
 
Asante mdau kwa kuliona hili.Nimeona kuna na B+,E haaaa haaa kama vyuo vikuu vile.Naomba serikali irudishe mfumo wa Zamani hii "DILUTION" ya ALAMA si nzuri hata kidogo kwa nchi yetu.
 
mim nafikiri hapa serekali inajaribu kucheza na akili za watanzania kwasababu kiwango cha elimu kushuka sio kwa sababu ya madaraja au mgawanyo wa alama ni kwasababu ya nchi kukosa sera na dira ya elimu kwa muda mrefu sasa hivyo wanashindwa watekeleze nini ndo maana kila siku wanabuni cha kufanya na kuzidi kuharibu ubora wa elimu.Kinachotakiwa kufanyika sasa ni kutengenezwa kwa sera na kupatikana kwa mipango ya muda mrefu ili kuikwamua sekta ya elimu ambayo ndiyo chimbuko la wanataaluma wa kada mbalimbali.
 
Asante mdau kwa kuliona hili.Nimeona kuna na B+,E haaaa haaa kama vyuo vikuu vile.Naomba serikali irudishe mfumo wa Zamani hii "DILUTION" ya ALAMA si nzuri hata kidogo kwa nchi yetu.

Usiogope mabadiliko ndugu, mbona advance kuna "E", halafu ili kupima maendeleo ya elimu yeyote ni lazima kuwe na mfumo ulio sawa kuanzia mwanzo hadi mwisho wa madaraja ya watahiniwa, hapo mwanzo kila daraja lilikuwa linajitegemea, primary kivyao, o,level kivyao, advance kivyao na chuo kivyao, je kwa hali hii unaweza kuelewa maendeleo ya elimu?

Uwepo wa B+, B na "E" si tatizo, chakuangaliwa ni marks na uhalisia wa ufaulu.
 
Wallahi hii ni kuudanganya uma wakati elimu inateketea!! Tena bila aibu eti ufaulu umeongezeka! Kweli ?? Hivi wanatumia kichwa kufikiri ama ?? Hii serikali hapana kwakweli!! Ptuuuuuu!!!!
 
Nina maoni hasa katika kipindi hiki muhimu cha kutunga katiba kuwa waziri wa Elimu asipendekezwe bali aombe kazi.wazira ya Elimu iitwe MWAMLAKA YA ELIMU TANZANIA " ili wanataaluma ndio wawe na MWAMLAKA ya kubadili mwenendo wa Elimu! Katika hali ya kushangaza na ya kusikitisha ni pale Elimu ya Tanzania inavyoshuwa kwa nguvu ili kuendana na joto la kisiasa! Na hili kila mtu ameliona baada ya mtokeo ya kidatoa cha nne! Kiwango cha kufeli kimesushwa kwa kuanzishwa grade nyingi sana za ufaulu! Bila kusahau kuwa chanzo kikubwa cha kufeli wanafunzi ni ongezeko la shule za kata na shule za binafsi ambazo hazina ubora! Huku fani ya ualimu ikidhalauliwa! imefika wakati sasa hii wizara iendeshwe na wanataaluma wenyewe!
 
Tatizo kila anayeingia baraza anataka atoke na historia yake ya nini alichokibadilisha
 
Mm acha nipite tu maana nina hasira mbaya. yani kama ndo sasa iv mm ningekuwa na 1.7 kama vipi turudishe vyeti haiwezekani.
 
Kama ni kelele tumepiga sana
Kelele zetu kama MAJI YA MOTO hayakawii kupoa
Serikali yetu kama pakacha bovu ukiziba huku kule kunavuja
Siku,miezi mwaka ,miaka inapita
Kelele, kelele , elimu duni,waalimu hawatoshi malipo kidogo,wanafunzi wanakaa chini madawati hakuna na sasa matokeo du???

Huduma za afya hoi ukiandikiwa asprin ukanunue dukani,Kina mama wanajifungulia chini hosptalini vitanda hakuna

Umeme mgao au unakatika katika bila sababu na bei juu

Polisi Mahakamani bila chochote file halionekani au kesi itapigwa tarehe hadi mashahidi wako watakuchoka kesi dismiss

Wimbo mmoja kila siku kelele hadi watawala wetu wametuchoka wanasema sisi watanzania mazuzu tutawachagua tu kwani
kama maji ya moto hatukawii kupoa
Ni kweli ngoma ya watoto haikeshi

Hebu na tukue mwakani uchaguzi tucheze ngoma ya watu wazima mpaka kuche giza limezidi
 
sasa Mama Mdogo,kwani hata kama angekuwa hajaenda secondary ndo apate 4 ya 43!au wanaogopa kuwawekea ziro!eti ziro ina athari kisaikolojia!
 
Last edited by a moderator:

mimi kinaniumiza kichwa kuhusu sifa za mtu anayetakiwa kujiunga na advance,kwani mwanzo ilikuwa C tatu ila sasa nasikia ni C tano,je wale ambao wamemaliza mwaka juzi na walikuwa wana C mbili wakategemea kurisiti ili kupata C moja waweze soma advance inakuwaje?au ndio maumivu?
 
Mm acha nipite tu maana nina hasira mbaya. yani kama ndo sasa iv mm ningekuwa na 1.7 kama vipi turudishe vyeti haiwezekani.

tunaanza lini kurudisha?mana namimi ilibidi niwe na 1 ya 8
 


Hii maana yake nini?

Wote point 43, mmoja Div 0 na mwingine IV
 
..............................
 
This is nonsense BRN at work. You are wondering 43 points been division IV, how about 47point??it's also division IV!!!!!!This means having six Fs and one E you passed , really??Our leaders where are we taking our education, our children????Please have mercy to this nation, I beg you
 
sasa Mama Mdogo,kwani hata kama angekuwa hajaenda secondary ndo apate 4 ya 43!au wanaogopa kuwawekea ziro!eti ziro ina athari kisaikolojia!

Haya yote yamesababishwa na ukimywa wa Mheshimiwa Waziri Kawambwa na ujasiri wa Naibu Waziri Mlugo kuamua anavyoona bila kujua athari yake katika kipindi cha muda mfupi na kipindi cha muda mrefu. Hii hali inaitwa Mlugoism: Strongly believing that what you are saying is true; while in actual sense it is not very true!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…