Msiba wa marehemu Kudula Madoda anayedaiwa kuwa mchumba wa mbunge wa viti maalumu Catherine Magige, umetawaliwa na vituko ya aina yake Mara baada ya Magige na kundi lake kuvunja geti ili kushiriki maziko ya marehemu baada ya kuzuiwa.
Marehemu Madoda amezikwa leo katika shamba lake eneo la Nduruma,ambapo katika mazishi hayo yaliyoratibiwa na ndugu wa marehemu Magige hakutakiwa kuingia kaburini na wapambe wake baada ya familia hiyo kueleza kwamba watakao ingia kaburini ni wachache.
Hata hivyo Mbunge Magige akiwa na kundi lake aliamua kuvamia kwa kuvunja lango la kuingilia ndani ya shamba Hilo na kufanikisha kushiriki mazishi kwa kuweka shada la maua kaburini.
Watu walipokuwa kwenye kaburi walijawa na taharuki kuona Mbunge huyo akiongoza kundi la wanawake kuingia ndani ya shamba ambako mwili wa marehemu ulizikwa.
Kabla ya mazishi hayo Magige alidai marehemu alikuwa mchumba wake lakini ndugu wa marehemu wakidai huyo alikuwa mwizi Kama wezi wengine wa wanaume na familia inamtambua mke halali wa marehemu ni Aziza Msuya.
Marehemu ameacha watoto watatu wa mke wake wa ndoa Aziza Msuya aliyefunga naye ndoa ya kikristu mwaka 2003mjini Dodoma.