Poleni sana Wakazi wa hii Mikoa tajwa Tanzania kwa Joto Kali mnalolipitia sasa

Poleni sana Wakazi wa hii Mikoa tajwa Tanzania kwa Joto Kali mnalolipitia sasa

Pemba, kummmke.
Huku kuna joto sijawahi ona tangu dunia imeumbwa.
Hawa wapemba sijui wanaishije.
Halafu nimegundua wapemba wengi hawapendi kulala na feni.
Hapa nateseka sana.

Nawaza vingi 🤔 ila ngoja niishie hapa.
 
Nimetoka kutizama Taarifa ya Habari muda si mrefu na kuona Watanzania wenzangu huko mliko mnavyotaabika sasa kwa Joto Kali ambalo huenda likawa limevunja Rekodi

Polemi sana Wakati wa Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Tanga na Zanzibar (Unguja na Pemba)

Nilipo Mimi Kampala, Mubende na Fort Portal nchini Uganda Hali ya Hewa ni nzuri kabisa kwakuwa Waganda wana Nidhamu kubwa mno ya Kutunza mazingira na hata kama Kampala kuna Joto ila siyo Kali kama la huko Nyumbani ambako Nidhamu ya Kutunza mazingira iko chini na Mkazo mkubwa umewekwa katika Kuwahudumia Machawa, Kumsifu Mtu hadi Kukufuru, kujadili Simba na Yanga na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ujao ambao hata Mwendawazimu anajua nani atashinda kwa Kampeni zisizo rasmi ambazo Mbabe Zuzu kazianza ila Mnyonge Makini nae akitaka kuanza zake anazuiwa.

Hata Wakazi wa hii Mikoa tajwa hapo juu GENTAMYCINE nawaombeni sana kuwa jitahidini muwe Mnaoga mara kwa mara, mnywe Maji mengi na kamwe msipendelee kwenda Kubanduana Mchana katika Gesti zilizoezekwa Mabati kwani mtachemka na hata Kufa.

Naomba baada ya hii Hali mbaya ya Hewa (ya Joto Kali) kumalizika mwezi wa Tatu katikati kwa mujibu wa Wataalam Serikali ije na Sheria Kali ya kuwataka Watanzania wote popote pale walipo (Majumbani Kwao) Wapende Miti 20 kuzunguka Nyumba zao na asiyetii Amri awekwe Ndani.

Pia Serikali iishurutishe Mamlaka inayohusika na Misitu (TFS) igawe bure kabisa Miche ya Miti kwa Watanzania wote ili waipande na Mimi yangu waniwekee kama 100 ambapo nikirejea nataka nikaipande yaliko Makazi yangu Tukuka Masaki Dar es Salaam, Mapinga Bagamoyo, Butuguri Mara na Chigugu Mtwara.
Kumbe somo ni jirani yangu hapa Masasi ( chigugu)
 
Joto linakwenda hadi 36°C kudadadinya kama sio kiama basi ni kitu gani hii tena.
 
Pemba, kummmke.
Huku kuna joto sijawahi ona tangu dunia imeumbwa.
Hawa wapemba sijui wanaishije.
Halafu nimegundua wapemba wengi hawapendi kulala na feni.
Hapa nateseka sana.

Nawaza vingi 🤔 ila ngoja niishie hapa.
Umempelekea mpemba akuweke halafu feni hana!

Bahari huwa inatema mvuke, usishangae hata ukalale nyumba ya beach front utakutana na joto la kibabe.
 
Back
Top Bottom