Swala ni darasa d
POLENI sana ndugu zangu Wasukuma kwa kufanya utani kwenye uchaguzi na kuacha vigezo vya uwezo wa kiakili ninyi wenzangu mnaangalia mtu ambaye ana uwezo wa kuwanunuliwa vitumbua, ubwabwa, soda na kuwagawia shilingi elfu 5 tano matokeo yake mnapeleka wabunge bungeni ambao hawana uwezo wa kujua jema au baya na wao wanaangalia wanapataje hela kupitia tenda na serikali na kuwasahau na kusahau hata hoja zenu kanda ya ziwa.
Mfano Angalia Majimbo ya Mkoa wa Mwanza, Kuna Tabasamu Darasa la 7, kuna Mnyeti elimu yake hata haijulikani, kuna Mansoor wa Kwimba hata elimu yake haijulikani, Angalia Jimbo la Magu Kiswaga elimu yake haijulikani, nenda Geita Msukuma darasa la 7, Maganga jimbo la Mbogwe darasa la 7, Amar jimbo la nyangwale darasa la 7, Jimbo la Ushetu, Cherehani elimu yake haijulikani, Solwa Ahmed elimu yake haijulikani, Jimbo la Kishapu Butondo elimu yake haijulikani. Nenda Simiyu jimbo la Itilima Njalu Darasa la 7.
Sasa kwa mfumo wa wasukuma kuendelea kuchagua wabunge wa darasa la 7 wakifika bungeni hawawezi kusoma miswada ya sheria, hawawezi kusoma mikataba inayopitishwa na bunge, wawezi hata kubeba hoja za wananchi wa kanda ya ziwa kama za pamba, mifugo na samaki matokeo yake sekta zote zimekufa kwa kukosa wasemaji bunge.
Lakini nenda Mkoa wa Kilimanjaro, Tanga, Arusha, Kagera na maeneo mengine huwezi kukuta ujinga wa darasa la 7 na ndiyo maana hata linapokuja suala la watu kupewa uwaziri wanaangalia majimbo yenye wasomi angalau digrii 2 na kuendelea.
Swala ni darasa au lugha? Mm ni darasa la Saba nimefanya kazi na mnayemwita msomi wa UDOM Pale Morogoro 21st century Maboss wetu ni wahindi mpaka leo. Nilikuwa na uwezo wa kupokea maelekezo ya kazi na kutoa maelezo ya kazi kuliko huyo msomi Kwa issue ya lugha. MSITUDHARAU wengine tulifaulu ila hatukuchaguliwa. Wakati huo siyo kila aliyefaulu alichaguliwa nafasi zilikuwa chache. Ok naamini tunahitaji wenye uchungu na nchi. Hv Tulia na Mbunge Msukuma bora Nan? Hv Tulia na huyo Mbunge aliyemsimamisha vikao 15 nani bora?Kusema kweli sijawahi kufika mkoa wa Kilimanjaro. Ni kule kujimwambafai kwa Wachagga tu ndo kulinipotosha na kudhani kwao pako vizuri.
Ila nilichobaini ni kwamba watu wengi wana misconception kuhusiana na Wasukuma kama huyu mleta mada. Kuna watu hata utafiti wa kisosholojia hawajawahi kufanya ila wanapayuka tu kuwa Wasukuma hiki, Wasukuma kile kwa njia hasi.
Hao wanaojisifu wana Wabunge wasomi wamesaidiwa nini na usomi wa Wabunge wao? Yule Prof.Jumanne Maghembe alifanya kipi cha maana kule Upareni? Vipi Prof.Simon Mbilinyi kule Ruvuma au Prof.Philemon Sarungi kule Ujaluoni?
N.B:Nisieleweke kwamba sipendi Wabunge wasomi laaah,nawapenda ikizingatiwa kuwa mimi pia nina elimu, sasa naanzaje kuichukia? Ila namkosoa mleta mada kwa namna alivyofanya shambulizi dhidi ya kabila moja tu nchini kana kwamba huko kwingine mambo yako vizuri.