Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 40,476
- 26,173
Ndugu zangu Watanzania,
Baada ya Polepole kuona anaendelea kupuuzwa na kusahaulika kabisa akilini na midomoni mwa Watanzania, sasa ameanza kutunga uongo, kufanya uchonganishi wa kidini, kupandikiza chuki na uongo wa kila aina kwa lengo la kumchafua Rais wetu mpendwa ambaye anaendelea kukubalika, kupendwa na kuungwa mkono na Watanzania kila uchao.
Eti anasema salamu ya Rais Samia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inafanya kama kufuru kwa Mungu au kushusha thamani ya Mungu.
Ukweli ni kwamba salamu ya Rais wetu mpendwa, ambayo imepokelewa vyema sana na Watanzania wote wa dini zote, inasema kuwa "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania", halafu watu wanaitikia "Kazi iendelee." Kwa hiyo, neno "katika" halipo katika salamu hiyo ambayo inatumiwa na Rais wetu.
Ambapo kusema "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania", halafu wananchi au watu wakaitikia "Kazi iendelee", hakuna makosa, wala siyo kosa, wala haiondoi au kupoka utukufu wa Mungu, au kuchukua nafasi ya Mungu na sifa zake anazostahili kupewa Mungu Mwenyewe.
Ikumbukwe ya kuwa Rais wetu ni mcha Mungu na mwenye hofu ya Mungu sana kifuani pake. Ndio sababu amekuwa ni mtu wa kuhubiri haki na kutenda haki kwa watu wote, pamoja na kukemea vikali sana tabia na matendo yoyote ya uonezi na unyanyasaji kwa watu wasio na hatia.
Hata hivyo, inaonyesha sasa Humphrey Polepole ameanza kuchanganyikiwa na kutapatapa sana. Ameona amelikoroga na kunywa, anashindwa sasa, maana ni shubiri na chungu kama mwarobaini. Ameanza kuunga unga "vistori" visivyo na ukweli wala mashiko. Amebaki kama mtu asiyejitambua na mwenye matatizo kichwani yanayohitaji matibabu.
Mwisho ni kuwa, hata afanyeje na atumie nguvu kiasi gani kuongea uzushi na uongo, lakini kamwe hataweza kumchafua Rais wetu, wala kumshushia heshima yake, wala kumshusha hapo alipo, wala kuondoa imani kubwa waliyonayo Watanzania kwa Rais wetu.
Rais Samia aliinuliwa kwa mkono wa Mungu Mwenyewe, na kamwe hawezi kushushwa kwa mkono wa mwanadamu mwenye chuki binafsi aina ya Polepole na wanaomtuma na kumtumia.
Kazi iendelee. Mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa
Mama anatosha kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Pia Soma: >> Polepole: Salamu ya 'Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.... Kazi iendelee!' inamkiuka Mungu