Polepole Amepotosha na kusema Uongo juu ya Salamu ya Rais Samia ya 'Jamhuri ya Muungano wa Tanzania'. Na huu ndio ukweli wake

Polepole Amepotosha na kusema Uongo juu ya Salamu ya Rais Samia ya 'Jamhuri ya Muungano wa Tanzania'. Na huu ndio ukweli wake

Serikali ya Rais Samia ni imara
Sawa ila hakuna serikali isiyo na mapungufu maana haingozwi na malaika au unataka kutushawishi hii serikali chini ya Samia haina madhaifu? Kama yapo mbona hatuoni kukosoa hayo madhaifu?
 
Sawa ila hakuna serikali isiyo na mapungufu maana haingozwi na malaika au unataka kutushawishi hii serikali chini ya Samia haina madhaifu? Kama yapo mbona hatuoni kukosoa hayo madhaifu?
Kwani wewe huoni juhudi na jitihada za serikali yetu katika kupambana na changamoto na kero mbalimbali? Au wewe unaangalia kwa jicho lipi? Marekani kwenyewe kuna changamoto chungu nzima
 
Kwani wewe huoni juhudi na jitihada za serikali yetu katika kupambana na changamoto na kero mbalimbali? Au wewe unaangalia kwa jicho lipi? Marekani kwenyewe kuna changamoto chungu nzima
Huko Marekani si tu kwamba kuna changamoto bali pia kuna mapungufu na makosa yenye kufanywa na serikali na watu huyakosoa, ila wewe hapa Tz si tu kwamba unayafumbia macho makosa ya serikali na kuyakodolea macho yale tu unayoona mazuri ya kusifiwa bali unaona wenye kukosoa ni maadui hapaswi kukosoa.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Baada ya polepole kuona anaendelea kupuuzwa na kusahaulika kabisa akilini na midomoni mwa Watanzania. Sasa ameanza kutunga uongo ,kufanya uchonganishi wa kidini ,kupandikiza chuki na uongo wa kila aina kwa lengo la kumchafua Rais wetu Mpendwa ambaye anaendelea kukubalika ,kupendwa na kuungwa mkono na watanzania kila uchao.

Eti anasema salamu ya Rais Samia ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inafanya kama Kufuru kwa Mungu au kushusha thamani ya Mungu.

Ukweli ni kwamba Salamu ya Rais wetu Mpendwa ambayo imepokelewa vyema sana na watanzania wote wa Dini zote inasema kuwa 'Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ' halafu watu wanaitikia 'kazi iendelee. Kwa hiyo neno 'katika' halipo katika salamu hiyo ambayo inatumiwa na Rais wetu.

Ambapo kusema Jamuhuri ya Muungano Wa Tanzania. Halafu wananchi au watu wakaitikia kazi iendelee,hakuna makosa wala siyo kosa wala haiondoi au kupoka utukufu wa Mungu . Au kuchukua nafasi ya Mungu na sifa zake anazostahili kupewa Mungu Mwenyewe.

Ikumbukwe ya Kuwa Rais wetu ni mcha Mungu na mwenye hofu ya Mungu sana kifuani pake. Ndio sababu amekuwa ni mtu wa kuhubiri haki na kutenda haki kwa watu wote pamoja na kukemea vikali sana tabia na matendo yoyote ya uonezi na unyanyasaji kwa watu wasio na hatia.

Hata hivyo inaonyesha sasa Humphrey Polepole ameanza kuchanganyikiwa na kutapatapa sana. Ameona amelikoroga na kunywa anashindwa sasa ,maana ni shubiri na chungu kama mwarobaini. Ameanza kuunga unga vistori visivyo na ukweli wala mashiko. Amebaki kama mtu asiyejitambua na mwenye matatizo kichwani yanayohitaji matibabu.

Mwisho ni kuwa hata afanyeje na atumie nguvu kiasi gani kuongea uzushi na uongo lakini kamwe hataweza kumchafua Rais wetu wala kumshushia heshima yake ,wala kumshusha hapo alipo wala kuondoa imani kubwa waliyonayo watanzania kwa Rais wetu.

Rais Samia aliinuliwa kwa Mkono wa Mungu Mwenyewe na kamwe hawezi kushushwa kwa mkono wa mwanadamu mwenye chuki binafsi aina ya polepole na wanaomtuma na kumtumia.View attachment 3426519

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Hako kajamaa kenu kamechanganyikiwa na ni kapumbafu.

Kwamba Slow Slow ametumwa na Mwenyezi Mungu kusema salamu aliyoasisi Rais inakinzana na Mungu?

Endeleeni tuu kumchekea .

Mwisho ni kwamba aambie salamu nyingine ni "Mitano Tena"
 
Ni kashamba na kalimbukeni sanaa
 
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya muungano ya wa Tanzania!!! Hahaha
 
Back
Top Bottom