#COVID19 Polepole ataka kiwanda cha dawa za mimea kupambana na Corona, aomba kikafichwe Jeshini

Unaweza kuficha kiwanda mbali mabeberu washindwe kufika!!
Iran wana kiwanda cha nuclear wamekuficha lakini mabeberu wanafahamu.
Huyu Polepole mweupe sana,bora aendelee kukaa kimya siku iingie
Ni kampeni meneja aliyepewa ubunge kwa mataarisho ya nafasi kubwa zaidi katika Ufalme wa miaka saba ya nyongeza.
 
Bado ana element za mwendazake. Maana yeye kila kitu jeshi. Korosho Jeshi, kuteka maduka ya fedha Jeshi, Kuiba uchaguzi Jeshi. Yaani yeye yuko kwenye Jeshi jeshi jeshi jeshi. Apuuzwe tu. Corona sio homa ya kideri ya kuku.

Duniani koote, wanasayansi wakubwa wanapatikana jeshini. Kwa kiwango fulani yuko sahihi. Tunapaswa na sisi kufanya kitu kuhusu janga hili. Siyo kusubiria tu. Jana nilikuwa nasikiliza DW Radio wanasema Tanzania wameanza kufanya utafiti kutumia panya kubaini maambukizi ya uviko-19. Walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kwenye TB, sasa wanafanya kwenye uviko 19. Wataalam wa SUA wanasema mafanikio yanaonekana. Panya wataweza kufanya kazi hiyo na kwa ufanisi.
 
Polepole mchangie huyo Kada ulimchosha sana
 
Eti ni vita! Bado ana msongo wa mawazo huyu chakubanga.

Yaani hamjui hata adui yake anaepambana nae, badala ashauri nguvu za kupambana na korona anawaza vita na mabeberu tu ambao bahati mbaya nao wana pambana na korona hiyo hiyo!

Hawa jamaa waambiwe ujinga wa kutuaminisha vita na tupo vitani ili watupige hela na kutufanya wanyonge haupo tena
 
Corona ni local problem??

Kwanza nani alimchagua huyu kwenda bungeni??

Haya mambo ya kuteuliwa yanaleta shida sababu ni kwa hisani tu hakuna vigezo vyovyote vyenye mantiki
 
Duniani koote, wanasayansi wakubwa wanapatikana jeshini. Kwa kiwango fulani yuko sahihi. Tunapaswa na
tupe mfano wa hao wanasayansi
Mkuu jitahidi ukitoa statement angalau iwe na uthibitisho ili kuondoa hearsays.
 
Huyu jamaa ndio alikuwa anamdanganya hayati pia kuhusu vita ya kiuchumu.. Kweli kabisa nani anataka vita na Tanzania na kwa sababu zipi? Ukiona Congo na Ivory Coast ndio utaelewa wakiamua lao hawashindwi, vita ambayo tunayo ni ya umasikini na ujinga tu hizo nyingine ni illusion..

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
 
tupe mfano wa hao wanasayansi

Mkuu jitahidi ukitoa statement angalau iwe na uthibitisho ili kuondoa hearsays.

Bwana mdogo mbona kila kitu kiko wazi? Wewe hujui, kwenye mataifa makubwa wanasayansi wakubwa wanapatikana wapi.

Hii ya panya, nenda SUA utaona hata jina la panya aliyepewa tuzo ya kutegua mabomu mengi zaidi ya ardhini huko Cambodia.
 
Anawaza kuhujumiwa tu kaka yetu,😂 japo ushauri wake siyo mbaya kiviiiile.
Mkuu ushauri wake ni mbaya. Bado ana mawazo "Tunaonewa wivu", "Tunahujumiwa". Mpaka sasa hatujafanya utafiti wa corona (uviko) lakini tayari tumeshakimbilia kutengeneza kiwanda cha dawa tena za mimea. Huyu bado anazungumzia bupiji, covidol, nimcarf na kadhalika. Kwa sasa angejikita zaidi kwenye vitu tunavoweza - kujikinga na kuchukua tahadhari!! Swala la mimea dawa (home remedies) tuachiwe majumbani mwetu!!
 
Yupo sahihi [emoji817] na huo ndo ukwel wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…