#COVID19 Polepole ataka kiwanda cha dawa za mimea kupambana na Corona, aomba kikafichwe Jeshini

Mawazo ya huyu mtu ni ya kijinga kabisa. Ni aheri angekaa kimya, watu wasingejua kilichomo kichwani mwake.

Ni nani akahujumu kiwanda cha kutengeneza juice zitokanazo na mimea? Kama kweli tuna dawa ya kutibu corona, kwa nini tusiweke wazi ili zifanyiwe majaribio na vyombo vinavyotambulika kimataifa?

Tunatumia dawa ngapi zilizogundulika katika mataifa mengine, halafu leo tumepata juice inayompa unafuu mgonjwa wa corona, tunasema tukaifiche!! Hopeless kabisa. Huyu hata kwenye huo ubunge wangemwondoa tu, hayupo sawasawa.
 
Kavae barakoa binti.
Umetumia β€˜binti’ kwa nia ya kunidhalilisha au kunikera? Kwa taarifa yako, mama yangu alikuwa binti, nimeoa binti ya Mtu, na nina mabinti zangu wawili, nnao wapenda sana! Kwa hivyo, kuniita binti, pamoja na kwamba mimi ni mwanaume, hakunikeri, kama ulivyo kusudia, bali kunaonesha β€˜ujima’ Wako wa kijinga na udhalilishaji na dharau kwa wanawake!
 
Umevaa barakoa au unabwata tu hovyo mitandaoni?
 
yaani wewe na pole pole hata akili za kuvukia barabara hamna nahisi
Yaani mpaka leo hii anaamini corona inatibiwa na hayo madawa ya Asili?!
Mbumbumbu wewe, babu zako waliishi kwa kula mizizi mpaka wewe ukazaliwa mbona hawakufa?

Mizizi, majani ya miti na magome zote ni dawa za asili na zinatibu kwa ufasaha unaotakiwa.

Umeshakaririshwa kwamba ili upone lazima unywe madawa kutoka Washington DC!

Wakikupa dawa ya muarobaini hutaki, ati wewe ni msomi!!

Msomi gani mjinga tu wewe. Ukishamiliki hako katekno ukaweza na ku google madesa basi na wewe unajitia mjuaji.
 
Ni nani akuhujumu kiwanda cha kutengeneza juice zitokanazo na mimea? Kama kweli tuna dawa ya kutibu corona, kwa nini tusiweke wazi ili zifanyiwe majaribio na vyombo vinavyotambulika kimataifa?.
Mtoto mdogo wewe hujui dunia inavyokwenda!

Jaribu kutengeneza hiyo dawa uone kama hawajakufyeka.

Watakuwekea na vikwazo vya kiuchumi, watakwambia haufwati viwango vya WHO.

Na ukijaribu kuipeleka hiyo dawa WHO ili ikathibitishwe watakwambia haina viwango na haitambuliki.

Dunia imeshikiliwa na matapeli. Hujui kitu wewe kinda.

Lazima tujifunze kujitegemea na kujiamini.
 
Kati ya Mimi na wewe Nani mbumbumbu ?
Tunazungumzia kirusi Cha covid wewe unaleta blaa blaa za mababu zako wa kishumundu wa karne hizo
Hao babu zako waliwahi umwa corona?
 
Umeongea kama bibi yangu aliye kijijini yani umeshindwa kujua Tanzania hatuko kwenye Target yoyote kwa hawa jamaa tusingekuwa tulivo hivi.

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
 
Kati ya Mimi na wewe Nani mbumbumbu ?
Tunazungumzia kirusi Cha covid wewe unaleta blaa blaa za mababu zako wa kishumundu wa karne hizo
Hao babu zako waliwahi umwa corona?
Ndio maana nimekuita mbumbumbu.

Unazidi kujidhihirisha mubashara namna ulivyo kichwa-box.
 
Polepole ameongea Point leo mpaka nimesisimka.
Njia tulizozitumia Mwaka jana zikatuokoa kwanini tusiendelee kutimia sasa.? Wenzetu wametumia njia za Lockdown hatimae uchumi ukashuka na bado wakawa na vifo vingi.

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38] akikutana na wajinga lazima wamuamini
Wewe ndio una akili sana.?!!

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Ngoja nkuhifadhi mkuu
 
Ndio maana nimekuita mbumbumbu.

Unazidi kujidhihirisha mubashara namna ulivyo kichwa-box.
Mtu pori toka chattle mabatini aliwaharibu akili watu Kama ninyi mbaka mnashindwa kutumia bongo zenu vizuri
Halafu unajiona kichwa humu jamvini wakati sisi tunakujua Kama taga tu
Hivi yule mungu wenu aliesema mpige nyungu yupo wapi vile?
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Wewe ndio una akili sana.?!!

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
"Usomi" kwa mujibu wa hawa nyumbu wa mtandaoni, ni kumeza machanjo bila kuuliza.

Ukiuliza mbona hizi chanjo hazina ithibati ya usalama, wanabwata... ooohhhh tunafungulia nchi!

Ati ndio usomi.... usomi gani wa kudungwa masumu ya ajabu ajabu!

Wengine humu ni madalali wa chanjo ambao kazi yao kubwa mitandaoni ni ku-influence public opinion.

Ni matapeli tu kama matapeli wengine.
 
Doh...umemvua nguo mangi mchana kweupee kabakia kukenua meno yake yaliyobungua kutokana na kunywa mbege iliyochacha.
 
Wenzetu huko wana viwanda, maabara na wasomi wa kutosha kutengeneza hizo chanjo na dawa kwa zaidi ya miaka 80-100 sasa na imewachukua mwaka kupata hizo chanjo. Halafu hizo chanjo hamziamini licha ya wao kuanza kutumia.

Huku mnataka kuanzisha kiwanda wakati hata wataalamu wa kung'oa meno tu hatuna sembuse teknolojia. Hiyo mitambo ya viwanda mnayotaka iwe siri watatengeneza JKT?
Kuna watu wakiwa kwenye Viete wanaishi Utopia kabisa na tunaendelea kuwalipa, sisi ni bure kabisa.
 
Polepole una hoja kelele za mazezeta mtu mmoja ID zaida ya kumi usiyasikilize.
yalimhadaa Lissu aanzishe maandamano eti alishinda uchaguzi😁😁😁😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…