GE2025 Polepole: CCM wanakwenda kwenye Uchaguzi sababu wana uhakika kushinda kwakuwa kuna mifumo inawabeba

GE2025 Polepole: CCM wanakwenda kwenye Uchaguzi sababu wana uhakika kushinda kwakuwa kuna mifumo inawabeba

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hakuna kigeni juu ya CCM kuiba kura, hili lipo miaka nenda rudi hata mtoto ndogo anajua.
Maana Kila mgombea Urais kuanzia 1995 aliiba kura mpaka Shujaa 2015 aliiba kura na HP akiwa mshiriki pia.

Tunachotaka kuona miaka yote ni watanzania kuchukua hatua dhidi ya haki yao yakuchagua na kuchaguliwa dhidi ya CCM na Serikali yake.

Hata CDM walipokuja na NRNE maana yake walikuwa uchaguzi hauko huru na sio wa haki hivyo ili uchaguzi uwe huru na haki reform lazima zifanyike.

ndani ya mitaa ya Benghazi Libya.
bulyan'hulu ndio Benghazi?
 
Wajanja tunajua hizi njama kitambo sana! Umesikia wanasema wamejiandikisha watu milioni sijui ngapi. Wale ni watu wa NIDA. 😁

Hii nchi ukishaijua, haikusumbui yaani. Werevu wengi hatupigia kura since 2000. Naam
Ujanja ni mzuri.

Lakini hili suala ni la common sense tu.

Haihitaji mtu uwe rocket scientist kujua kwamba kuna mgongano mkubwa sana wa kimaslahi kati ya mwenyekiti wa CCM, ambaye ni Rais na mgombea urais tena, kuunda safu ya uongozi wa tume ya uchaguzi ambayo itasimamia uchaguzi ambao mtu aliyewateua, naye ni mgombea kwenye uchaguzi huo.

Ni common sense tu.
 
Alichokisema Leo polepole ndio kashfa kubwa ya kisiasa tokea tupate Uhuru. Kwamba kuna mfumo wa Siri wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) umeunganishwa direct na (INEC) Kwa manufaa ya ccm kwenye uchaguzi mkuu. Kwamba mfumo huo utatumika kuiba au kuchakata matokeo ya uongo. Polepole ameongea Kwa hisia na kuvitaka vyama vitakavyoshiriki uchaguzi huo vijiridhishe japo vyote ni vya ccm isipokuwa chadema tu ambao ndio wapinzani wa kweli na wamefunga mikono isivyo haki.
Ubaya wa skendo hii ni kwamba haya mambo yakiwahiwa yakaondolewa mapema na mifumo ikawa huru basi mambo yatakuwa sawa japo tutakuwa tushajua dhamira yao ovu ilikuwa ninini. Lakini jambo hili likiachwa bila kufanyiwa kazi hii ni jinai kuu na itabatilisha hata huo ushindi wa ccm. Moderators msifute Wala kuunganisha huu Uzi.
Ujinga unamfumo alafu washindani niccm b kwa kujibu wake sasa hofu yake nini hapo wakati tupo navyama rafiki hakana hoja je kanafanya kazi nida au tume
 
KNi fedheha kwa jaji wa mahakama kuwa sehemu ya uchafu huu, lakini tufanyeje naye ndoto yake ni kuteuliwa. Jaji wa mahakama ya. rufani na kuwa na uhakika wa maisha Hadi kifo.
 
Mkuu zaman tulikua tunahisia tu , LEO LIMETHIBITISHWA NA MWANDAMIZI MWENYEWE ALOHUSIKA KUULETA .

Nadhani ndio Sababu alisema, potelea Mbali Wacha CCM isambaratike ila Taifa Liponye.
Wewe ulikuwa unaona ni sawa tu tume ya uchaguzi viongozi wake wakiteuliwa na mwenyekiti wa CCM, ambaye ndiye Rais, na ambaye pia ni mgombea urais katika uchaguzi ambao hiyo tume itausimamia?

Kabisa conflict of interest hukuwa unaiona hapo?

Mbona ni suala jepesi sana hilo?
 
Hii kitaalamu ni kuwa CCM amekuwa, na anaweza kuyachezea matokeo ya chaguzi atakavyo.

"Haya ndiyo ambayo wamekuwa wanayapigia kelele Kenya na Odinga kwa kauli mbiu yao almaarufu, wafungue chungu!"

View attachment 3448602

Kwamba mnaweza kuwa mlikuwapo Kila kitu sawa, ghafla bin vuuu! Tarakimu zikabadilika kuwa zozote. Alisema Cheyo kwenda na mkewe kupiga kura, ati kuwa hata mkewe hakumpigia! Akihusisha tukio hilo CCM labda kuwa na majini!

Hii inajibu sababu za kukataa kwa tume kura kuhesabiwa vituoni, vyama kuwa na vituo vyao vya kujumlishia matokeo na longo longo zote kuhusiana wasimamizi wa uchaguzi wa vyama, kura za mapema Zanzibar n.k. Kumbe zote zimekuwa ni hila!

Kwa mtaji huu, wasimamizi wa vyama wasionunulika au kukaba vilivyo hadi penalty aina za kina Mdude, Soka, Ben na wenzao wangenusurika wapi?

Ameomba msamaha Polepole kwa kuhusika kwenye hili. Kwa hakika ni heri yeye vinginevyo tungeujulia wapi u fedhuli huu? Wanasema ni heri nusu shari.

"Mungu ambariki Polepole, Mungu ambariki TAL. Hatuko mbali na nyumbani"

No Reforms no Election!

Pia soma: NRNE na mazagazaga yake ni mpango wa Mungu. Nani ajuaye kuwa Polepole leo, hatutajua walipo wenzetu waliopotea na yote ya uvunguni?
Kumbe ndio maana Gwajima akasisitiza CHADEMA wapewe minimum reforms kisha wakaipige kwenye uchaguzi
 
Swali muhimu zaidi ni : Utawafanya nini?
Swala la wizi wa kura limekuwepo na kufahamika kwa muda mrefu sasa. Kilicho ongezeka ni hiyo njia mpya ya kimtandao.

Sasa kinachotakiwa ni waTanzania kukataa kura zao kuchezewa.

Je, tuanzie wapi? Hili ndilo swali muhimu.
 
Back
Top Bottom