Hii kitaalamu ni kuwa CCM amekuwa, na anaweza kuyachezea matokeo ya chaguzi atakavyo.
"Haya ndiyo ambayo wamekuwa wanayapigia kelele Kenya na Odinga kwa kauli mbiu yao almaarufu,
wafungue chungu!"
View attachment 3448602
Kwamba mnaweza kuwa mlikuwapo Kila kitu sawa, ghafla bin vuuu! Tarakimu zikabadilika kuwa zozote. Alisema Cheyo kwenda na mkewe kupiga kura, ati kuwa hata mkewe hakumpigia! Akihusisha tukio hilo CCM labda kuwa na majini!
Hii inajibu sababu za kukataa kwa tume kura kuhesabiwa vituoni, vyama kuwa na vituo vyao vya kujumlishia matokeo na longo longo zote kuhusiana wasimamizi wa uchaguzi wa vyama, kura za mapema Zanzibar n.k. Kumbe zote zimekuwa ni hila!
Kwa mtaji huu, wasimamizi wa vyama wasionunulika au kukaba vilivyo hadi penalty aina za kina Mdude, Soka, Ben na wenzao wangenusurika wapi?
Ameomba msamaha Polepole kwa kuhusika kwenye hili. Kwa hakika ni heri yeye vinginevyo tungeujulia wapi u fedhuli huu? Wanasema ni heri nusu shari.
"Mungu ambariki Polepole, Mungu ambariki TAL. Hatuko mbali na nyumbani"
No Reforms no Election!
Pia soma:
NRNE na mazagazaga yake ni mpango wa Mungu. Nani ajuaye kuwa Polepole leo, hatutajua walipo wenzetu waliopotea na yote ya uvunguni?