GE2025 Polepole: CCM wanakwenda kwenye Uchaguzi sababu wana uhakika kushinda kwakuwa kuna mifumo inawabeba

GE2025 Polepole: CCM wanakwenda kwenye Uchaguzi sababu wana uhakika kushinda kwakuwa kuna mifumo inawabeba

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kwanza Polepole mwenyewe kabembeleza hadi kachoka, pamoja na mizengwe mingi aliyotumia kuwapelekea ujumbe asipasue jipu!

Tulipofikia sasa hivi ni wananchi pekee ndio wanaoweza kuwafikishia ujumbe wa kuwa stua akili na kuwafanya wasite kuendelea na mipango yao miovu.
Naam, na kwakua wananchi bado tumelala tukipata mitano ijayo, tutakua katika position nzuri zaidi. Hivi anavyoongea polepole hakuna jipya alilolisema, vingi ni vitu vilikua vinatajwa muda wote.

kinachotakiwa hapa ni wengi. washuhudie tu hii 2025 kwa umakini, kama 2020 ilianzisha safari hii 2025 itamaliza safari
 
Wizi wa kura sio tuhuma ngeni dhidi ya CCM.
Zipo miaka yote na sidhani kama tunapaswa kushangaa na kuona kitu kigeni.

Kigeni ni kuona watanzania wanaingia barabarani na kudai haki zao bila kutegemea blah blah za wanasiasa ambao nao ni wanufaika wa mifumo mibovu iliyopo.

HP ni part and parcel wa kilichopo na hapaswi kuaminika na ni upumbavu kumuamini HP maana ni yake yake ya EL.
Ina maana EL alikuwa halijui hili kaja kulijuwa HP.
Mbona Lipumba na Dr Slaa mpaka Lyatonga marehemu walishalalamikia juu ya kuibiwa kura?
Ni upumbavu kuendelea kusikiliza hadithi hizi Kila siku bila kuchukua hatua au kuendelea kuomba hisani.
Hakuna jipya kwenye siasa za Tanzania na wizi wa kura wa CCM.

ndani ya mitaa ya Benghazi Libya.
Akili hii nayo ni matope. Unalinfanishaje malalamiko ya akina Slaa na Mrema na hiki alichosema Polepole? Wewe ulikuwa unajua m kwamba mfumo wa NIDA umeunganishwa na CCM?
 
Hapa kuna wazalendo wachache ndani ya mfumo wa serikali (vyombo) ya chama dola kongwe wameamua kuchukua hatua mikononi, kama kashfa maarufu ya Watergate nchini Marekani kuumbua utawala uliopo madarakani na mbinu chafu za kuelekea kutia tick mitano tena

KASHFA YA WATERGATE :

Skandali ya Watergate: THE WATERGATE SCANDAL.
#Historia #Siasa #Marekani

Je, unafahamu kuhusu kashfa ya Watergate iliyoitikisa Marekani miaka ya 1970?
Hii ilikuwa moja ya skandali kubwa zaidi za kisiasa katika historia ya Marekani, iliyopelekea kujiuzulu kwa Rais Richard Nixon mnamo 1974.

Kashfa hii ilihusisha upelelezi haramu dhidi ya chama cha upinzani, kuficha ushahidi, na matumizi mabaya ya madaraka. Wasaidizi wa karibu wa Nixon walihusika katika kuvamia makao makuu ya chama cha Democratic Party yaliyokuwa kwenye jengo la Watergate – ndipo jina hilo lilipotoka!

Wanamwandishi wa habari Bob Woodward na Carl Bernstein wa gazeti la The Washington Post waliufichua ukweli huu kupitia upelelezi wa kina.

Watergate ilibadilisha historia ya siasa za Marekani, ikasisitiza umuhimu wa uwazi, ukweli na uongozi wa kimaadili.

Uchambuzi :

Kashfa ya Watergate: Lini ilitokea na sababu ya kuvunja ofisi kuondoka na vifaa kuelekea uchaguzi​


2012
RAIS WA MAREKANI AJIUZULU KUFUATIA, 'VIBAKA' KUINGIA KATIKA JENGO

View: https://m.youtube.com/watch?v=IHnmriyXYeg

Ingawa umma ulipata upepo wa kashfa hii kwa mara ya kwanza baada ya uvamizi wa Watergate wa Juni 17, 1972, utata ulikuwa wa miaka mingi kuibuka.

Vikundi vilivyo karibu na Ikulu ya White House vilitumia njia zisizo halali kumhakikishia rais wao, Richard Nixon, atachaguliwa kwa muhula wa pili.

Na wizi wa Watergate ulikuwa fursa ya kupeleleza chama cha Democratic.

Haikuchukua muda mrefu kabla ya msururu wa watu kuwafikia watu muhimu katika Chama cha Republican, na ufichuzi ukaanza.

Waandishi wa habari nguli wenyeujasiri Bob Woodward na Carl Bernstein walijitupa kuingia ndani zaidi kubaini tukio hilo la aina yake , na kwa usaidizi kutoka kwa chanzo chao kisichojulikana cha Deep Throat, walisaidia kutatua changamoto zote zilizowekwa na watawala ukweli usijulikane , na hatimaye Kashfa ya Watergate ililazimisha kujiuzulu kwa mara ya kwanza na pekee kwa rais wa Marekani aliyekuwa yupo madarakani
...

Source : http://www.WatchMojo.com learns more about the Watergate Scandal


Ninakazia:

IMG_20240428_070927.jpg


Hawa watu ni wahaini!
 
Wakuu maana ya Hili ni kua


SERVERS za Tume ya Taifa ya Uchaguzi , zimedukuliwa na CCM .


Servers za NIDA zimedukuliwa na CCM.


Kwahiyo CCM wanauwezo wa kutumia Taarifa za NIDA tu kupiga Kura, na kufeed Matokeo Yao kwenye Servers za Tume ya Uchaguzi.😡😡😡😡😡😡😡😡😡😡
Hapo umechemka ndugu. Umejionyesha kuwa hujui kitu kuhusu mifumo ila ndo unajifanya much know.

Tofautisha kudukua na mifumo kuunganishwa ni vitu tofauti.

Kudukua ni "fishing" au "sniffing" na kuunganisha mifumo ni "systems integration".

Kudukua ni uhalifu. System integration siyo uhalifu.

Walichofanya ccm na tume ya uchaguzi ni kuunganisha mfumo wa tume na wa CCM pamoja na NIDA kwa ajili ya kuchukua data kutoka mfumo wa CCM kurahisisha uchakachuaji kwa akili zaidi. CCM wanatumia akili kuiba kura kwa kushirikiana na tume.
 
Una hoja Sana ila wanavyojibu ndo maana tunaitwa nyumbu

Hata Mimi nimebaki kujiuliza how mfumo uibe wakati kura zinahesabiwa ndani ya chumba mbele ya mawakala
Najua CCM wanaibaga kura Ila labda uniambie kwavituo hewa,rushwa kwa mawakala n.k

Hili la inec na NIDA sijalielewa
 
Naam, na kwakua wananchi bado tumelala tukipata mitano ijayo, tutakua katika position nzuri zaidi. Hivi anavyoongea polepole hakuna jipya alilolisema, vingi ni vitu vilikua vinatajwa muda wote.

kinachotakiwa hapa ni wengi. washuhudie tu hii 2025 kwa umakini, kama 2020 ilianzisha safari hii 2025 itamaliza safari
Dah, wewe ni mtu mwenye subira sana.
Unataka mitano mingine chini ya Samia na Genge lake?

Hapa tulipo fikia imetosha mkuu, hiyo mitano mingine ya kushuhudia ni kuliumiza taifa hili bila ya sababu muhimu.

Samia na genge lake mwisho wao ni 2025; siyo 2030.
 
Kuna maswali hapa nimeulizwa ambayo yametokana na alichosema Polepole:

1. Tupo kwenye zama za kidigitali ,je kuna kosa vyama kulink taarifa za wapigakura wake na mfumo wa NIDA ili kurahisisha utambuzi ?

2. Utaratibu wa kupiga kura na kuhesabu ni kwa kutumia karatasi , je mifumo hiyo imesaidia vipi ushindi kwa CCM?

3. Je Kuna tatizo gani CCM kulink mfumo wake na wa NIDA ikiwa hata taasisi nyingine zinafanya hivyo? Je, tatizo ni kwa CCM?

Akamaliza kwa kusema Polepole kwa sasa hajui asemalo ,amepuuzwa kabisa
Ccm hamuwezi, kusafishika, kwa, dhambi zenu,hata kwa, damu, ya kristo!
Kama, bado upo kwenye denial kuhusu uovu wa ccm, inabidi wakuwaishe hospital ya vichaa milembe
 
Hapo umechemka ndugu. Umejionyesha kuwa hujui kitu kuhusu mifumo ila ndo unajifanya much know.

Tofautisha kudukua na mifumo kuunganishwa ni vitu tofauti.

Kudukua ni "fishing" au "sniffing" na kuunganisha mifumo ni "systems integration".

Kudukua ni uhalifu. System integration siyo uhalifu.

Walichofanya ccm na tume ya uchaguzi ni kuunganisha mfumo wa tume na wa CCM pamoja na NIDA kwa ajili ya kuchukua data kutoka mfumo wa CCM kurahisisha uchakachuaji kwa akili zaidi. CCM wanatumia akili kuiba kura kwa kushirikiana na tume.
Hahaha, duh kwahiyo hicho ndio kipimo cha akili??
 
Si huwa nawaambia msishiriki chaguzi zinazoendeshwa na kuratibiwa na tume ya uchaguzi iliyoundwa na CCM lakini huwa mnaniona hamnazo!

Hadi aseme Polepole ndo muamini kwamba mnajisumbua?

Where is your common sense?
Their common sense is at rest.
 
Pole pole ni kiboko aisee naona wakikaa watamuachia yule jamaa yao waliedhani kuwa ni hatari kwao hii inanikumbusha SA walimuua Stive Biko akatokeza John Mahlangu akawa hatari zaidi kuliko Biko nae wakamnyonga hapo Tswane ndio wakajitokeza watu wengi zaidi Mbeki,Mandela,Zuma,Sesulu na Mzee Oliver Tambo ambae yeye alikua anasafiri sana nje kusaka amani ya Nchi yake na ndio kisa cha uwanja wao wa ndege wakampa jina lake Oliver Tambo International Airport.
 
Back
Top Bottom