Fanfa
JF-Expert Member
- Sep 25, 2009
- 2,399
- 3,775
Pole pole anaongea na umma na wadau wa uchaguzi. Umma ndo wenye nguvu kubwa ukijua vizuri jambo fulani na ukiamua kulipinga. Wanasiasa peke yao hawawezi bila kutushirikisha umma.Asante mkuu 'Fanfa'.
Sasa tatizo si lipo hapa! Ni wao ndio wenye uamzi wa kuyakubali au kuyakataa mapendekezo hayo aliyotoa Polepole.
Sasa fikiria mwenyewe, jambo rahisi kama kufanya tu "marekebisho" wanayoyadai CHADEMA ikawa nongwa, na sasa tunakwenda kwenye kampeni za uchaguzi.
Polepole anayo nyenzo gani ya kuwafanya wasitishe jambo ambalo ndilo linawahakikishia ushindi?
Hiyo ndio ilikuwa maana yangu ya kusema "Tutawafanya nini"?
Kumbuka wameshika kila kona: Mahakama, wateule wote kwenye taasisi za maamuzi; na zaidi ya yote, mitutu ya akina Jumanne Mulilo!
WaTanzania wafanye nini ili hayo aliyo pendekeza Pole pole yafanyiwe kazi?
Polepole anawaambia umma ushenzi unapofanyikia. Tumpongrze na tumuunge mkono.