Polepole: Hii sio awamu ya Sita bali ni ya Tano kipindi cha pili, aliyeondoka ni Magufuli peke yake

Polepole: Hii sio awamu ya Sita bali ni ya Tano kipindi cha pili, aliyeondoka ni Magufuli peke yake

Kwa hiyo Mwinyi ndiye awamu ya kwanza? Sijui Kati yako na yeye nani mwenye au asiye na akili!

Tatizo haya mambo yanaenda kwa kufikirika, hakuna sehemu iliyoandikwa awamu zihesabiweje. Hivyo, ndio maana kila mtu anajiona kuwa sahihi.

Mwinyi alikuwa awamu ya pili.
Suala lisilo na taratibu mara nyingi huleta shida pale kinapotokea kitu kisichotarajiwa na hapo kwa wenzetu ndo hujifunza kuweka policy au protocol juu ya jambo husika.

Kuna watu wanahesabu mihura:
1: kichwa cha rais/mtu kubadilika(haiko kwa taratibu za serikali)

2: Miaka kumi ya uongozi husika(haipo kitaratibu za serikali)
Hapa bila miongozo kila mtu ni mshindi.
 
Wakuu,

Mbunge wa kuteuliwa na mtunga Sheria Humphrey Polepole, anadai hii awamu ya rais Samia sio awamu ya sita.

Rais Samia alisema yeye ndiye rais ya awamu ya Sita. Kwamba ni awamu ya sita kipindi cha kwanza.

"Hii serikali sio mpya,haikupigiwa kura, huwezi ukaita awamu ya sita, awamu lazima iwe na miaka10, ilani na Sera zinazopaswa kutekelezwa ni zile tulizozinadi 2020, asiwadanganye mtu kuwa hii ni awamu ya sita,Kwa sababu aliyeondoka ni Magufuli peke yake" kasema polepole.

RAIS SAMIA ANASEMA UFISADI ULIFANYIKA AWAMU ZILIZOPITA SIO AWAMU YAKE YA SITA
"Kuna makundi wanajua wanayoyafanya ndani ya serikali, na yanageuka kusema serikali ya awamu ya 6 ufisadi umerudi mambo yako hovyo kumbe wao ndio wako hovyo, mambo hayo yalifanyika huko nyuma, gari bovu linaangushiwa awamu ya 6 sitakubali"
Rais Samia Suluhu akiwa Bandarini.

Je, nani yupo sahihi na Sheria inasemaje?

View attachment 2041066
Huyo Polepole ni mpuuzi. Hivi ni wapi kwenye katiba yetu au sheria zetu ambapo imetamkwa kuwa awamu ni kipindi cha miaka 10 au 5?

Hapa kinachofanyika ni mazoea tu. Hivi ingetokea mwaka 2020 ule uchaguzi uwe ni uchaguzi wa kweli, na Tundu Lisu akashinda na kutangazwa kuwa ndiye Rais, bado ingeendelea kuwa ni awamu ya 5?

Awamu, kwa mazoea inaambatana na Kiongozi mkuu wa Serikali. Ndiyo maana tunasema awamu ya kwanza, awamu ya Mwalimu Nyerere. Tena wala siyo miaka 10, bali ni miaka 26. Ndani humo ni Nyerere akiwa Waziri Mkuu wa Tanganyika, Mwalimu Nyerere akiwa Rais wa Tanganyika na Mwalimu Nyerere akiwa Rais wa Tanzania.

Polepole ni mjinga, kushikilia jambo ambalo siyo la kisheria wala kikatiba. Katiba haitambui awamu bali hutambua mihula ya Urais. Kitu kisicho cha kikatiba wala kisheria, kila mtu ana uwezo wa kukitafsiri kwa namna yake, kwa namna inayoleta mantiki.

Kwa sasa mantiki iliyopo ni kuwa:

1) Awamu hutajwa kwa kigezo cha Rais. Rais mwingine, Serikali nyingine, awamu nyingine.

2) Awamu haina kipindi maalum bali huangalia mabadiliko ya Rais.

3) Uhalali wa Serikali hutajwa na katiba wala siyo uchaguzi. Kuna nchi ambazo hazimpigii kura kumchagua Rais, lakini bado anakuwa Rais na huunda Serikali.

NB: Ili kuondoa hizi kelele, ni vema katiba mpya iingize neno awamu kwenye katiba, na itoe tafsiri ya awamu. Watu wanasumbuliwa na kitu kisicho na mantiki kikataiba wala kisheria. Hivi tukisema hii ni awamubya 6 au awamu ya 5, ni nini kitakachobadilika? Au anaumizwa inapoonekana wao waliokuwa vinara wa awamu ya 5 wakisemwa kuwa walikuwa wauaji, wabambikiaji kesi, watekaji, wakanyagaji wa katiba na sheria, watu wenye mitazamo finyu ya kiuchumi?
 
Ni kweli hii ni awamu ya tano( 5) lakini Rais ni wa sita hivi wanamdanganya nani
Hiyo tafsiri imetoa wapi? Au ni fikra zako binafsi? Kama ni fikra zako binafsi, wewe una haki gani tofauti na yule anayesema kuwa hii ni awamu ya sita kwa sababu aliyepo sasa ni Rais wa 6?
 
Nyerere aliyetawala Tanzania kwa miaka 21 alitawala kwa awamu ngapi?
Hiyo ni awamu ya kwanza kwa ujumla wake. Wakati ule hakukuwa na utaratibu wa idadi ya mihula ya kutawala ingawa bado uchaguzi ulifanyika kila baada ya miaka mitano.

Baada ya Nyerere utaratibu ukawekwa wa rais kutawala vipindi viwili iwapo atataka kugombea tena.
 
Unapotumia neno AMIRI JESHI maana yake ni kama unamtisha asitoe maoni yake
Anaesema hii ni Awamu ya Sita ni Amiri Jeshi Mkuu!

Kama anapinga hii sio Awamu ya sita inamaanisha anapingana na Amiri Jeshi Mkuu na anamdharau waziwazi!

Sasa ndo atajua kuwa Samia ni Rais na Amiri Jeshi Mkuu. Mark my words
 
Wewe kubali tu tuko awamu ya 5. 2020 tumemchagua magufuli wewe jitahidi kuendeleza msimamo wa kimagufuli ndio watu walimchagua. Ukifanikisha hilo hakika watu watakupenda sana. Mungu akubariki mama yetu.
Magufuli alichaguliwa au alijichagua?
 
Hata ikiwa ni awamu ya kumi hiyo itatusaidia nini sisi?
Kwangu mimi awamu maana yake ni kipindi cha mtawala akiwa madarakani, na hapa Tz mtawala ni rais.
Rais=awamu
Nyerere (awamu ya kwanza)
Mwinyi (awamu ya pili)
Mkapa (awamu ya tatu)
Kikwete (awamu ya nne)
Magufuli (awamu ya tano)
Samia (awamu ya Sita)
Chakubanga (awamu ya saba?!)[emoji1787]
Huyo Chakubanga, ni takataka, ondoa asionekane hata kwenye kumbukumbu. Yeye ni miongoni mwa minara ya shetani. Alichokifanya 2020 na mashetani wenzake hastahili kuwa hata balozi wa nyumba 10.
 
Inawezekana polepole yuko sahihi kwa maana kwamba aliyebadilika ni rais peke yake. Kwa hiyo tunaweza kusema Samia ni rais wa sita katika awamu ya tano
Kwani awamu ni nini?

Ulikwishawahi kusikia:

1) Awamu ya Mwalimu Nyerere

Au

2) Awamu ya kwanza, ya Mwalimu Nyerere?

Unaelewa nini?
 
Ila ulifanyika uchaguzi..kupata serikali mpya na wabunge wapya chini ya mwinyi kama rais..hivyo ikaitwa awamu ya pili mwinyi akiwa rais wa pili..nikuulize wewe mchumia tumbo..baada ya JPM kufa kuna uchaguzi uliofanyika? ili kuharalisha kua hii ni awamu nyingine..au ni kumalizia awamu ya 5 kwa mujibu wa katiba?

#MaendeleoHayanaChama
Tatizo mnajadili kwa hoja za juu juu tu. Nani alikuambia kuwa Serikali wakati wote huundwa baada ya uchaguzi? Serikali huundwa kwa mujibu wa katiba na siyo kwa sababu uchaguzi umefanyika.

Mwalimu Nyerere alipounda Serikali yake ya kwanza, na yeye akiwa Waziri Mkuu, kulikuwa na uchaguzi Mkuu wa kumchagua Waziri Mkuu?

Wapi kwenye sheria zetu palipoelezwa kuwa awamu huundwa baada ya uchaguzi?
 
Ni ya 6 Kwa sababu rais hakuwa Samia; maamuzi alikuwa anafanya mwingine; Samia hausiki kabisa Na Makosa ya awamu ya 5
Mkuu miongozo haimtaji mtu kuwa awamu, inataja uchaguzi kuwa awamu, kwa hyo kinachozaa awamu Ni uchaguzi, kwa Sasa tupo awamu ya 5 Ila tuna rais wa 6,

Nyogeza tu kidg, baada ya nyerere aliekaa madarakani miaka 20+ Toka mwaka 1985- Sasa tuna awamu za vipindi vya miaka 5, na kwa rais miaka 10, kwa hyo ingetokea tumefanya uchaguzi, Basi rais angekuwa ktk awam ya 6 Ila kwa Sasa Ni awamu 5 ya kazi iendeleee, Kama unabisha, njoo unipige@drmsukuma
 
Raisﹰ ﹰSamia ni rais wa awamu ya sita, Awamu moja haiwezi kuwa na rais wawili.
 
Hivi magufuli aliwahi kushinda uchaguzi wote tangu akiwa mbunge ??
Magufuli kwa uhakika wa 100% hajawahi kushinda uchaguzi wowote katika Ulimwengu huu! Tangu akiwa mbunge, yeye ilikuwa ni kutumia mbinu chafu tu. Uchafu huo huo aliupeleka mpaka kwenye uchaguzi mkuu. Hakuwa muumini wa demokrasia, haki wala uhuru wa watu.

Magufuli was born a dictator and lived it.
 
Tatizo mnajadili kwa hoja za juu juu tu. Nani alikuambia kuwa Serikali wakati wote huundwa baada ya uchaguzi? Serikali huundwa kwa mujibu wa katiba na siyo kwa sababu uchaguzi umefanyika.

Mwalimu Nyerere alipounda Serikali yake ya kwanza, na yeye akiwa Waziri Mkuu, kulikuwa na uchaguzi Mkuu wa kumchagua Waziri Mkuu?

Wapi kwenye sheria zetu palipoelezwa kuwa awamu huundwa baada ya uchaguzi?
Mkuu serikal haiundwi na mtu inaundwa na watu, ingekuwa inaundwa na mtu leo hii Samia asingekuwa rais, Ila kwa kuwa inaundwa na watu ndo maana Samia rais, Tena Wala hatuna shida kabisa, t

Tatzo Ni kuchanganya Kati ya rais 6 na awamu ya 6, fullstop..
 
Tumia Akili Awamu ZIMEANZA kutumika kuanzia Utawala wa Mwinyi
Sasa mbona Kikwete alihesabika kama Rais wa awamu ya nne na sio ya 3 kama awamu zilianza kuhesabika kipindi cha Mwinyi?

Wewe ndo hovyo kabisa.
 
Anaesema hii ni Awamu ya Sita ni Amiri Jeshi Mkuu!

Kama anapinga hii sio Awamu ya sita inamaanisha anapingana na Amiri Jeshi Mkuu na anamdharau waziwazi!

Sasa ndo atajua kuwa Samia ni Rais na Amiri Jeshi Mkuu. Mark my words
Akili yako ndogo, kwanini usiseme mwekiti wa Ccm au Rais?

Uamiri jeshi unakujaje tunapozungumzia AWAMU za utawala?

Jua kila cheo kina mahali pake kutajwa.

Kulitumia kila mara ni dalili za udhaifu na kutojiamini.
 
Anaesema hii ni Awamu ya Sita ni Amiri Jeshi Mkuu!

Kama anapinga hii sio Awamu ya sita inamaanisha anapingana na Amiri Jeshi Mkuu na anamdharau waziwazi!

Sasa ndo atajua kuwa Samia ni Rais na Amiri Jeshi Mkuu. Mark my words
Akili yako ndogo, kwanini usiseme mwekiti wa Ccm au Rais?

Uamiri jeshi unakujaje tunapozungumzia AWAMU za utawala?

Jua kila cheo kina mahali pake kutajwa.

Kulitumia kila mara ni dalili za udhaifu
 
Kama kinachozaa awamu ni uchaguzi wa kila baada ya miaka mitano kwa sasa tuko awamu ya kumi na moja
Mkuu miongozo haimtaji mtu kuwa awamu, inataja uchaguzi kuwa awamu, kwa hyo kinachozaa awamu Ni uchaguzi, kwa Sasa tupo awamu ya 5 Ila tuna rais wa 6,

Nyogeza tu kidg, baada ya nyerere aliekaa madarakani miaka 20+ Toka mwaka 1985- Sasa tuna awamu za vipindi vya miaka 5, na kwa rais miaka 10, kwa hyo ingetokea tumefanya uchaguzi, Basi rais angekuwa ktk awam ya 6 Ila kwa Sasa Ni awamu 5 ya kazi iendeleee, Kama unabisha, njoo unipige@drmsukuma
 
Magufuli kwa uhakika wa 100% hajawahi kushinda uchaguzi wowote katika Ulimwengu huu! Tangu akiwa mbunge, yeye ilikuwa ni kutumia mbinu chafu tu. Uchafu huo huo aliupeleka mpaka kwenye uchaguzi mkuu. Hakuwa muumini wa demokrasia, haki wala uhuru wa watu.

Magufuli was born a dictator and lived it.
Mkuu uko sahihi, hakuwahi kushinda Ila aliwahi kuchaguliwa, Sasa wale wenye maamzi ya kutangaza mshindi ndo hao waliosema amechaguliwa, hebu nenda kafuatilie matamshi ya mtangaza uchaguzi uone alichosema...
 
Back
Top Bottom