Tetesi: Polepole kufukuzwa CCM; nafasi yake kuchukuliwa na Mbowe

Tetesi: Polepole kufukuzwa CCM; nafasi yake kuchukuliwa na Mbowe

Dar es Salaam: Habari za chinichini zinapenyeza kuwa uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) upo mbioni kumfukuza na kumfuta uachana Mh Balozi Humprey Polepole na pia kumuondolea hadhi ya ubalozi. Hayo yanajiri wakati mwanachama huyo nguli wa CCM akiitisha mkutano na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao (zoom meeting) ambapo amesikika akiulaumu uongozi wa CCM hadharani kwa kukiuka taratibu za kumteua mama Samia kuwa mgombea atakayepeperusha bendera ya CCM katika kinyang'anyiro cha urais.

Ikiwa chama kitafanya hivyo, Polepole atakuwa sio mtu wa kwanza kufukuzwa CCM lakini atakuwa mtu wa pili kufutiwa hadhi ya ubalozi baada ya Dr Wilbroad Peter Slaa kufutiwa hadhi hiyo mwaka jana baada ya kutofautiana na viongozi wa CCM, hivyo kumlazimu kurudi CHADEMA.

Kwa kinachoendelea kwa sasa, sio jambo la ajabu kwa mtu kama Polepole kufutwa uanachama na kupokwa hadhi ya ubalozi. Swali ambalo halikuwa dhahiri ni je, baada ya kufukuzwa ni nani atakayeridhi mikoba yake? Swali hili tayari limepata jibu. Taarifa za kiintelijensia zinabainisha wazi kwamba mtu atakeyerithi mikoba ya Polepole ni Mh Freeman Aikael Mbowe, mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA aliyeng'atuka madarakani baada ya kukalia kiti hicho kwa muda wa miaka 21.

Inasemekana kwamba kitendo cha Mbowe kuhudhuria mkutano wa rais Samia wakati akizindua sera ya taifa ya 2025-2050 ulikuwa ni mpangomkakati wa kuanza kumtambulisha mbele ya wanachama na ndio maana alipewa nafasi ya kuongea kwenye mkutano huku akishangiliwa kwa nguvu na wanachama wenzake wa CCM.

Akiendelea mbele zaidi mwanaintelijensia anayefahamu vizuri kinachoendelea ndani ya CCM alisema: "Chama kinasubiri muda muafaka wa kumtambulisha Mh Mbowe kwenye mkutano maalumu utakaoitishwa hivi karibuni kwa ajili ya kumfukuza uanchama Mh Polepole. Itakuwa ni bandika, bandua; kata mti, panda mti". Alisema.

View attachment 3410897
MAONI YANGU
Pamoja na kuwa huenda CCM walishafikia makubaliano kumsajili Mbowe kwenye chama chao, namshauri Mh Mbowe asikubali kamwe kutumiwa na CCM kwa maslahi yao binafsi, hasa wakati huu tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu. Miaka yote 21 aliyoitumikia CHADEMA kwa uaminifu itakuwa bure na atafutika kabisa kwenye harakati za kisiasa za taifa hili kama ilivyotokea kwa akina Said Afi, Aman Kaborou, Sumaye, Lowasa na wengine.

Nawasilisha.
​
Chadema mnaweweseka sana, Mbowe anachukuaje nafasi ya Polepole? Kwahiyo Mbowe atakuwa katibu mwenezi na balozi mstaafu?
 
aisee mnambagaza sana mbowe

kajenga chama tangu kina mtu mmoja mpaka sasa wapo milioni 8

halafu wewe maandazi unamtukana kwamba ni usalama ?

si angekiua mapema?

mpaka january 21 kilikua safi na hakijayumba,kawaachia ofisi,sasa kimeyumba mnataka mtupia yeye lawama sio nyie mlioko ofisini?
Hawa nyumbu chama kimewashinda wanamsingizia Mbowe, walimchafua sana wakati wa kampeni na wakashangilia alivyoangushwa sasa mwamba kakaa kimya wao wanawashwawashwa.
 
Wanasema Mbowe anakwenda kuthibitishwa ndani ya ccm.maana anajulikana ni mwanccm alikuwa akiiongoza chadema.Ndiyo maana hofu ilitandanda walipoona Lisu anagombea uenyekiti chadema.


Siasa za Tanzania ni kuganga njaa.kila mtu anataka uongozi kwa sababu ya njaa yake binafsi.

Angalia uwekezaji wanaoufanya wagombea ubunge wa sisiem walioko kwenye mchakato wa kupitishwa tatu bora.

Wengi wa wabunge ambao ni wafanyabiashara wakubwa wanaingia bungeni ili kulinda biashara zao
Lema ,Lissu,Heche hawana njaa?

Wana maendeleo sana ya kifedha hawana NJAA?

Really?
 
Mvowe nafasi ambayo anaweza kuikubali ndani ya CCM labda awe PM kinyume na apo hana njaa ambayo inaweza mfanya achukue nafasi chini ya apo... Mbowe ni Tajiri tena Tajiri haswaaa
Anafanya biashara gani?
 
Back
Top Bottom