Tetesi: Polepole kufukuzwa CCM; nafasi yake kuchukuliwa na Mbowe

Wenyewe (CCM) walishaona fursa ilyomo ndani ya Mbowe. Subiri tuone itakavykuwa mkuu.
wewe washasema mwaka huu hawamuachii mtu jimbo, ndio maana unaona Msigwa kapigwa na kitu kizito, labda aombee Samia apate huo uraisi ili apate kuteuliwa
 
Dar es Salaam: Habari za chinichini zinapenyeza kuwa uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) upo mbioni kumfukuza na kumfuta uachana Mh Balozi Humprey Polepole na pia kumuondolea hadhi ya ubalozi. Hayo yanajiri wakati mwanachama huyo nguli wa CCM akiitisha mkutano na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao (zoom meeting) ambapo amesikika akiulaumu uongozi wa CCM hadharani kwa kukiuka taratibu za kumteua mama Samia kuwa mgombea atakayepeperusha bendera ya CCM katika kinyang'anyiro cha urais.

Ikiwa chama kitafanya hivyo, Polepole atakuwa sio mtu wa kwanza kufukuzwa CCM lakini atakuwa mtu wa pili kufutiwa hadhi ya ubalozi baada ya Dr Wilbroad Peter Slaa kufutiwa hadhi hiyo mwaka jana baada ya kutofautiana na viongozi wa CCM, hivyo kumlazimu kurudi CHADEMA.

Kwa kinachoendelea kwa sasa, sio jambo la ajabu kwa mtu kama Polepole kufutwa uanachama na kupokwa hadhi ya ubalozi. Swali ambalo halikuwa dhahiri ni je, baada ya kufukuzwa ni nani atakayeridhi mikoba yake? Swali hili tayari limepata jibu. Taarifa za kiintelijensia zinabainisha wazi kwamba mtu atakeyerithi mikoba ya Polepole ni Mh Freeman Aikael Mbowe, mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA aliyeng'atuka madarakani baada ya kukalia kiti hicho kwa muda wa miaka 21.

Inasemekana kwamba kitendo cha Mbowe kuhudhuria mkutano wa rais Samia wakati akizindua sera ya taifa ya 2025-2050 ulikuwa ni mpangomkakati wa kuanza kumtambulisha mbele ya wanachama na ndio maana alipewa nafasi ya kuongea kwenye mkutano huku akishangiliwa kwa nguvu na wanachama wenzake wa CCM.

Akiendelea mbele zaidi mwanaintelijensia anayefahamu vizuri kinachoendelea ndani ya CCM alisema: "Chama kinasubiri muda muafaka wa kumtambulisha Mh Mbowe kwenye mkutano maalumu utakaoitishwa hivi karibuni kwa ajili ya kumfukuza uanchama Mh Polepole. Itakuwa ni bandika, bandua; kata mti, panda mti". Alisema.

MAONI YANGU
Pamoja na kuwa huenda CCM walishafikia makubaliano kumsajili Mbowe kwenye chama chao, namshauri Mh Mbowe asikubali kamwe kutumiwa na CCM kwa maslahi yao binafsi, hasa wakati huu tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu. Miaka yote 21 aliyoitumikia CHADEMA kwa uaminifu itakuwa bure na atafutika kabisa kwenye harakati za kisiasa za taifa hili kama ilivyotokea kwa akina Said Afi, Aman Kaborou, Sumaye, Lowasa na wengine.

Nawasilisha.
​
Unajua akili zako sijyi nizilinganishe na nani,yaani unamfukuza mtu uanachama halafu nafasi yake anapewa mtu fulani,hii ni akili ya wapi? hebu tafuta uongo mwingine huu umebuma
 
Ila ubalozi is inversely proportional to ubalozi siyo?
 
Unajua akili zako sijyi nizilinganishe na nani,yaani unamfukuza mtu uanachama halafu nafasi yake anapewa mtu fulani,hii ni akili ya wapi? hebu tafuta uongo mwingine huu umebuma
Wakati, ukuta. Kwanini tuandikie mate wakati wino upo? Vuta subira kidogo mkuu.
 
Kwamba mbowe anaenda kuwa mwanachama mtiifu,wa kupeana mikono na mzee wa ubaridini mr msigwa
 
WARAKA WA GODBLESS LEMA KWA MBOWE!

Mhe. Godbless Lema amemuandikia waraka Mhe. Freeman Mbowe. Kwa kuwa waraka huo umebeba maudhui yenye maslahi mapana, sisi tunauweka hapa kusudi kupanua wigo wa fikra.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 17 Julai 2025; saa 2:50 usiku.

Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe!
Kwa heshima, huzuni na uzito wa dhamira, nakuandikia barua hii si kwa hasira, bali kwa mwangwi wa historia inayolilia uaminifu. Sisi tulisimama nyuma yako kwa gharama kubwa kipindi chote ambacho tulikuamini kuwa wewe ni kiongozi wa matumaini ya kizazi kilichojitoa kwa ajili ya Tanzania mpya wakati ulipokuwa Mwenyekiti wetu.

Leo hii umetazamwa ukihudhuria mkutano wa Serikali kuhusu Dira ya Maendeleo ya Taifa, huku Mwenyekiti wetu, Tundu Lissu, akiwa gerezani akikabiliwa na mashtaka ya uhaini na chama chetu hakiruhusiwi kufanya siasa na wanachama wetu wanapotea, wanateswa, wengine wameuawa na bado hujatokea hata mara moja mahakamani, wala kutoa neno la kukemea udhalimu huu unaoendelea mbele ya macho ya Watanzania.

Tulikuwa pamoja nawe wakati ulipokamatwa na kushtakiwa kwa ugaidi na changamoto mbalimbali nyingi katika uongozi wako. Tulilia. Tulipiga kelele. Tulivunjwa. Tukateswa. Lakini tuliendelea kusimama kwa ajili yako kwa sababu tuliamini ulikuwa kiongozi wa haki. Leo, unajibu kwa ukimya. Ukimya usio na ujasiri. Ukimya unaogharimu damu nyingine isiyo na hatia.

“Mungu hadhihakiwi; kwa maana apandacho mtu ndicho atakachovuna.”
Wagalatia 6:7

Kaka, imekuwa ikisemwa kwamba unayo hasira dhidi ya baadhi ya maneno yaliyotamkwa na wanachama wakati wa uchaguzi wa ndani wa chama. Lakini je, unaweza kweli kuwa na hasira dhidi ya maneno hayo ya kawaida kuliko kuwa na hasira dhidi ya waliokufunga kwa kukuita gaidi? Je, unaweza kuwa na uchungu kwa wakosoaji wako wa ndani, lakini ukaishi kwa amani na wale ambao walikutesa na tunao washutumu kwa utekaji, mateso, vifo na dhuluma dhidi ya haki na utu?

Ulikuwa Mwenyekiti kwa zaidi ya miaka 20. Siwezi kuandika hapa majina ya watu waliopoteza maisha kwa sababu waliamini kuwa uongozi wetu ulikuwa na dhamira ya kweli. Tumewazika karibu kila mkoa wa nchi hii, tumewasaidia majeruhi. Tumewaokoa wachache gerezani. Na wengi wao walipigania jina lako. Waliamini katika mfumo uliouongoza. Leo hii, je tuseme nini kwa familia zao? Wakati wao bado wanalipa gharama ya mapambano .
Wakati huo huo, hujawahi hata siku moja kusema au kuandika hadharani kuhusu mateso haya yanayoendelea kwa CHADEMA na viongozi wake haswa kesi mbaya inayo mkabili Mkti wetu Tundu Lissu.

“Kama sauti ya damu ya Abeli ililia kutoka ardhini, ndivyo sauti ya mashujaa wa haki inavyolia kila siku ikitafuta si kisasi, bali uaminifu wa dhamira.” Mwanzo 4:10

Kama tuliweza kuamka kwa ajili yako, ulipokuwa kiongozi wa Chama chetu , kwa nini sasa usiweze kusimama kwa ajili ya haki, maana hata kama unapumzika siasa lakini binadamu mwema hawezi kupumzisha dhamira yake juu ya haki na utu. Unafikiri ni sahihi kukosekana kwa andiko au sauti na uwepo wako mahakamani toka Lissu amekamatwa na kwa ajili ya wengine wengi ambao sasa wako katika hatari kubwa ?

Chama ambacho wewe ni Mjumbe wa Kamati Kuu hakiruhusiwi kufanya mikutano ya hadhara. Vijana wake wanapigwa. Mwenyekiti wake yuko jela na viongozi wake wanateswa. Na bado, hakuna neno kutoka kwako. Hakuna kilio na bado unaweza kushiriki hafla za Serikali bila aibu. Nini kiko nyuma?

“Dhamira safi huwa haipumziki katika meza ya heshima, ikiwa vunjiko la haki linapiga kelele mlangoni.” - Nelson Mandela

Kwa heshima na unyenyekevu wa historia, tunakuomba, usijitenganishe na damu ya mashujaa waliokuamini. Usikubali jina lako kuwa ukuta wa kusahau damu ya wale waliochinjwa kwa jina la mabadiliko. Usikubali kusimama upande wa utulivu bandia unaozima sauti ya walalia haki.

Huu si mwaliko wa ugomvi. Hii ni sauti ya dhamira. Kilio cha kizazi kilichoumizwa, lakini bado kinabeba matumaini kwamba kuna waliotumwa kusimama kwenye ufa wa taifa.

“Haki haipotei, hata ikizikwa kwenye vumbi la kisiasa huibuka tena kwa sauti ya waliojeruhiwa.”

Na hata kama haukumbuki vilio vya waliopotea, kumbuka hili ,mahali ambapo Tundu Lissu anateseka leo Mahakama Kuu ya Tanzania si mbali sana kama Dodoma ulipokuwa ukishiriki kwenye mkutano wa Serikali. Ni safari ya dhamira tu inayotenganisha hatua zako na hatua ya hakika.

Godbless Lema, 17 Julai 2025
 
kama mnamuweka mbowe anawasaliti kweupe yani ccm mshachanganyikiwa.Mbowe anakiuza chama
Mbowe anakiuza chama kwa CCM kwa vipande 30 vya fedha kama Yuda Eskarioti alivyomuuza Yesu kwa mafarisayo. Mbowe ni Yuda.
 
Mbowe amejingea heshima kwa miaka 21, nitamshangaa sana kama heshima hii kubwa ataiuza kwa vipande 30
 
Watu wa Dar Fanyeni maamuzi achaneni na tetesi mnatuchanganya sie wa huku.

tetesi zinasaidia nini kama siyo majungu.
 
Dar es Salaam: Habari za chinichini zinapenyeza kuwa uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) upo mbioni kumfukuza na kumfuta uachana Mh Balozi Humprey Polepole na pia kumuondolea hadhi ya ubalozi. Hayo yanajiri wakati mwanachama huyo nguli wa CCM akiitisha mkutano na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao (zoom meeting) ambapo amesikika akiulaumu uongozi wa CCM hadharani kwa kukiuka taratibu za kumteua mama Samia kuwa mgombea atakayepeperusha bendera ya CCM katika kinyang'anyiro cha urais.

Ikiwa chama kitafanya hivyo, Polepole atakuwa sio mtu wa kwanza kufukuzwa CCM lakini atakuwa mtu wa pili kufutiwa hadhi ya ubalozi baada ya Dr Wilbroad Peter Slaa kufutiwa hadhi hiyo mwaka jana baada ya kutofautiana na viongozi wa CCM, hivyo kumlazimu kurudi CHADEMA.

Kwa kinachoendelea kwa sasa, sio jambo la ajabu kwa mtu kama Polepole kufutwa uanachama na kupokwa hadhi ya ubalozi. Swali ambalo halikuwa dhahiri ni je, baada ya kufukuzwa ni nani atakayeridhi mikoba yake? Swali hili tayari limepata jibu. Taarifa za kiintelijensia zinabainisha wazi kwamba mtu atakeyerithi mikoba ya Polepole ni Mh Freeman Aikael Mbowe, mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA aliyeng'atuka madarakani baada ya kukalia kiti hicho kwa muda wa miaka 21.

Inasemekana kwamba kitendo cha Mbowe kuhudhuria mkutano wa rais Samia wakati akizindua sera ya taifa ya 2025-2050 ulikuwa ni mpangomkakati wa kuanza kumtambulisha mbele ya wanachama na ndio maana alipewa nafasi ya kuongea kwenye mkutano huku akishangiliwa kwa nguvu na wanachama wenzake wa CCM.

Akiendelea mbele zaidi mwanaintelijensia anayefahamu vizuri kinachoendelea ndani ya CCM alisema: "Chama kinasubiri muda muafaka wa kumtambulisha Mh Mbowe kwenye mkutano maalumu utakaoitishwa hivi karibuni kwa ajili ya kumfukuza uanchama Mh Polepole. Itakuwa ni bandika, bandua; kata mti, panda mti". Alisema.

MAONI YANGU
Pamoja na kuwa huenda CCM walishafikia makubaliano kumsajili Mbowe kwenye chama chao, namshauri Mh Mbowe asikubali kamwe kutumiwa na CCM kwa maslahi yao binafsi, hasa wakati huu tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu. Miaka yote 21 aliyoitumikia CHADEMA kwa uaminifu itakuwa bure na atafutika kabisa kwenye harakati za kisiasa za taifa hili kama ilivyotokea kwa akina Said Afi, Aman Kaborou, Sumaye, Lowasa na wengine.

Nawasilisha.
​
KOSA lake nn? Kusema ukweli?
 
Back
Top Bottom