Tetesi: Polepole kufukuzwa CCM; nafasi yake kuchukuliwa na Mbowe

Kwanini atoe siri za chama na kuwakosoa viongozi wakati yeye ni mgeni kwenye chama?
Pole pole sio mgeni kwenye CCM.
Anasema amekaa vikao vyoote hakuna alichobakiza. Amefanya kazi na heavy weights kama Salim, Waryoba, Butiku, Baregu, Magufuli. Kuna walio join chama 77 hawajawahi hata kuongea na hao wazito.
 
Sito shangaa. ILA HUYO atabaki upinzani ILI atumike VIZURI lisuu aki susa
 
Kuna uwezekano hata kesi ya mchongo ya Lissu huenda amehusika kuwapelekea CCM siri za CHADEMA. Haaminiki huyu.
 
Dar es Salaam: Habari za chinichini zinapenyeza kuwa uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) upo mbioni kumfukuza na kumfuta uachana Mh Balozi Humprey Polepole na pia kumuondolea hadhi ya ubalozi. Hayo yanajiri wakati mwanachama huyo nguli wa CCM akiitisha mkutano na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao (zoom meeting) ambapo amesikika akiulaumu uongozi wa CCM hadharani kwa kukiuka taratibu za kumteua mama Samia kuwa mgombea atakayepeperusha bendera ya CCM katika kinyang'anyiro cha urais.

Ikiwa chama kitafanya hivyo, Polepole atakuwa sio mtu wa kwanza kufukuzwa CCM lakini atakuwa mtu wa pili kufutiwa hadhi ya ubalozi baada ya Dr Wilbroad Peter Slaa kufutiwa hadhi hiyo mwaka jana baada ya kutofautiana na viongozi wa CCM, hivyo kumlazimu kurudi CHADEMA.

Kwa kinachoendelea kwa sasa, sio jambo la ajabu kwa mtu kama Polepole kufutwa uanachama na kupokwa hadhi ya ubalozi. Swali ambalo halikuwa dhahiri ni je, baada ya kufukuzwa ni nani atakayeridhi mikoba yake? Swali hili tayari limepata jibu. Taarifa za kiintelijensia zinabainisha wazi kwamba mtu atakeyerithi mikoba ya Polepole ni Mh Freeman Aikael Mbowe, mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA aliyeng'atuka madarakani baada ya kukalia kiti hicho kwa muda wa miaka 21.

Inasemekana kwamba kitendo cha Mbowe kuhudhuria mkutano wa rais Samia wakati akizindua sera ya taifa ya 2025-2050 ulikuwa ni mpangomkakati wa kuanza kumtambulisha mbele ya wanachama na ndio maana alipewa nafasi ya kuongea kwenye mkutano huku akishangiliwa kwa nguvu na wanachama wenzake wa CCM.

Akiendelea mbele zaidi mwanaintelijensia anayefahamu vizuri kinachoendelea ndani ya CCM alisema: "Chama kinasubiri muda muafaka wa kumtambulisha Mh Mbowe kwenye mkutano maalumu utakaoitishwa hivi karibuni kwa ajili ya kumfukuza uanchama Mh Polepole. Itakuwa ni bandika, bandua; kata mti, panda mti". Alisema.

MAONI YANGU
Pamoja na kuwa huenda CCM walishafikia makubaliano kumsajili Mbowe kwenye chama chao, namshauri Mh Mbowe asikubali kamwe kutumiwa na CCM kwa maslahi yao binafsi, hasa wakati huu tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu. Miaka yote 21 aliyoitumikia CHADEMA kwa uaminifu itakuwa bure na atafutika kabisa kwenye harakati za kisiasa za taifa hili kama ilivyotokea kwa akina Said Afi, Aman Kaborou, Sumaye, Lowasa na wengine.

Nawasilisha.
​
Mbowe hawezi ofa za chini hivyo
 
Pole pole sio mgeni kwenye CCM.
Anasema amekaa vikao vyoote hakuna alichobakiza. Amefanya kazi na heavy weights kama Salim, Waryoba, Butiku, Baregu, Magufuli. Kuna walio join chama 77 hawajawahi hata kuongea na hao wazito.
Sio ugeni huo unaosema wewe mkuu. Kwani Polepole alijiunga lini na CCM ukilinganisha na hao makada wengine uliowataja?
 
Mbowe hawezi ofa za chini hivyo
Unadhani ni ofa gani anayoweza kukubali mkuu? Hii labda ni ofa ya kuanzia na baada ya hapo watampa cheo kikubwa zaidi.
 
Tayari huko jamani. Mkutano maalumu unaketi leo kumfuta Polepole uanachama na hadhi ya ubalozi. Inasemekana na Gwajima naye atafukuzwa. Ngoja tuone.
1000247583.jpg
 
Mvowe nafasi ambayo anaweza kuikubali ndani ya CCM labda awe PM kinyume na apo hana njaa ambayo inaweza mfanya achukue nafasi chini ya apo... Mbowe ni Tajiri tena Tajiri haswaaa
 
Dar es Salaam: Habari za chinichini zinapenyeza kuwa uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) upo mbioni kumfukuza na kumfuta uachana Mh Balozi Humprey Polepole na pia kumuondolea hadhi ya ubalozi. Hayo yanajiri wakati mwanachama huyo nguli wa CCM akiitisha mkutano na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao (zoom meeting) ambapo amesikika akiulaumu uongozi wa CCM hadharani kwa kukiuka taratibu za kumteua mama Samia kuwa mgombea atakayepeperusha bendera ya CCM katika kinyang'anyiro cha urais.

Ikiwa chama kitafanya hivyo, Polepole atakuwa sio mtu wa kwanza kufukuzwa CCM lakini atakuwa mtu wa pili kufutiwa hadhi ya ubalozi baada ya Dr Wilbroad Peter Slaa kufutiwa hadhi hiyo mwaka jana baada ya kutofautiana na viongozi wa CCM, hivyo kumlazimu kurudi CHADEMA.

Kwa kinachoendelea kwa sasa, sio jambo la ajabu kwa mtu kama Polepole kufutwa uanachama na kupokwa hadhi ya ubalozi. Swali ambalo halikuwa dhahiri ni je, baada ya kufukuzwa ni nani atakayeridhi mikoba yake? Swali hili tayari limepata jibu. Taarifa za kiintelijensia zinabainisha wazi kwamba mtu atakeyerithi mikoba ya Polepole ni Mh Freeman Aikael Mbowe, mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA aliyeng'atuka madarakani baada ya kukalia kiti hicho kwa muda wa miaka 21.

Inasemekana kwamba kitendo cha Mbowe kuhudhuria mkutano wa rais Samia wakati akizindua sera ya taifa ya 2025-2050 ulikuwa ni mpangomkakati wa kuanza kumtambulisha mbele ya wanachama na ndio maana alipewa nafasi ya kuongea kwenye mkutano huku akishangiliwa kwa nguvu na wanachama wenzake wa CCM.

Akiendelea mbele zaidi mwanaintelijensia anayefahamu vizuri kinachoendelea ndani ya CCM alisema: "Chama kinasubiri muda muafaka wa kumtambulisha Mh Mbowe kwenye mkutano maalumu utakaoitishwa hivi karibuni kwa ajili ya kumfukuza uanchama Mh Polepole. Itakuwa ni bandika, bandua; kata mti, panda mti". Alisema.

View attachment 3410897
MAONI YANGU
Pamoja na kuwa huenda CCM walishafikia makubaliano kumsajili Mbowe kwenye chama chao, namshauri Mh Mbowe asikubali kamwe kutumiwa na CCM kwa maslahi yao binafsi, hasa wakati huu tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu. Miaka yote 21 aliyoitumikia CHADEMA kwa uaminifu itakuwa bure na atafutika kabisa kwenye harakati za kisiasa za taifa hili kama ilivyotokea kwa akina Said Afi, Aman Kaborou, Sumaye, Lowasa na wengine.

Nawasilisha.
​
Mbowe sio mjinga hivyo ndugu
 
Siaz za ushabiki za hovyo sana😂
ushabiki maandazi sana

hawa machalii walioachiwa chama cha chadema aisee,it shows how incompetent they are

yaani badala watumie nguvu zao kupambana na ccm wanatumia nguvu zao kupambana na mzee wa chama chao aliowalea sijui wanapata faida gani?
 
Yaani kuongea leo polepole, baada ya nusu saa tetesi zimeshatoka kuwa nafasi yake kuchukuliwa na Mbowe

Moderator hii siyo tetesi ni uhuni kama aliokuwa anausema Polepole. Futa uhuni huu!
We msee unakuanga emotional sana.
 
Ndiyo na ni gaidi kweli. Uliza familia ya Chacha Wangwe na Ben saanane. hata katibu Mkuu wake Dr. Slaa alithibitisha ugaidi wa Mbowe mara kadhaa. Sema Dereva mpya wa basi baada ya Jiwe kushuka hakuambiwa mapema kama Mbowe ni mtu wao na alikuwa akishiriki na kuwezesha ule ugaidi kwa maslahi yao CCM. Alipojulishwa aliahirisha habari za kumshikilia.
aisee mnambagaza sana mbowe

kajenga chama tangu kina mtu mmoja mpaka sasa wapo milioni 8

halafu wewe maandazi unamtukana kwamba ni usalama ?

si angekiua mapema?

mpaka january 21 kilikua safi na hakijayumba,kawaachia ofisi,sasa kimeyumba mnataka mtupia yeye lawama sio nyie mlioko ofisini?
 
Ndiyo na ni gaidi kweli. Uliza familia ya Chacha Wangwe na Ben saanane. hata katibu Mkuu wake Dr. Slaa alithibitisha ugaidi wa Mbowe mara kadhaa. Sema Dereva mpya wa basi baada ya Jiwe kushuka hakuambiwa mapema kama Mbowe ni mtu wao na alikuwa akishiriki na kuwezesha ule ugaidi kwa maslahi yao CCM. Alipojulishwa aliahirisha habari za kumshikilia.
Inachukua miezi mingapi taarifa kusafiri?
 
Back
Top Bottom