Kampeni za CCM 2020 tunazifanya kisayansi, tumegawanya viongozi waandamizi wa chama kwenye maeneo tofauti. Msafara mkuu unaongozwa na Dkt. Magufuli, msafara mwingine wa Mhe. Samia Suluhu, na mwingine unaongozwa na Kassim Majaliwa, sisi hatutumii chopa." - Humphrey Polepole.
Mzee Jakaya Kikwete yupo Ukanda wa Kusini kule anavuruga, Mzee Pinda na Spika Job Ndugai nao wanaendelea. Muziki ni mzito mpaka sasa tunapozungumza kuna mgombea mmoja amekimbia yupo nje ya nchi, ameona maji yamemfika shingoni, tunafanya kampenzi za kisayansi." -Humphrey Polepole
Tangu Mhe. Magufuli aingie madarakani hakujawa na mfumuko wa bei, tumefanya kazi nzuri mno, bidhaa haiongezeki, Mhe. Magufuli amefuta kodi kwa wenye mishara midogo, hawa wanaosema ni wapotoshaji, tumelazimika kuwajibu, tunawaambia wasifanye siasa na hivyo." - Humphrey Polepole.
"Ukisema kushuka kwa Diplomasia ni uongo, Mhe Magufuli ameingia tu madarakani akapewa Uenyekiti wa EAC, ameendeleza mwendo wa kubana matumizi, miradi mikubwa imefanyika, ameacha alama, SADC amefanya mambo makubwa, MSD inapeleka dawa nchi zote za SADC." - Humphrey Polepole.
Tumefuatilia na kujiridhisha kwamba ni uongo mtupu, na TCAA imeshatoa ufafanuzi, lakini unajiuliza nini dhamira ya kusema uongo, kwamba mmezuiliwa kwenda kufanya kampeni maana yake unataka kupandikiza chuki, na hata hakukuwa na mpango wa safari"