Polepole: Kuna mtu alikuja kuniambia kuwa kiongozi wa awamu ya 5 atakufa

Polepole: Kuna mtu alikuja kuniambia kuwa kiongozi wa awamu ya 5 atakufa

Gypsum Screw

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2024
Posts
1,624
Reaction score
1,937
Leo kwenye muendelezo wa mawasilisho yake huko mitandaoni Ndugu Humphrey Polepole amesema kuwa wakati wanakaribia uchaguzi mkuu 2020 kwenye kazi yake ya kusikiliza wananchi kuna bwana mmoja alimfuata akamwambia kuwa kuna watu wanapanga kumuua Rais wa wakati huo!

Anasema alipeleka ujumbe huo kwa muheshimiwa Rais, ambae pamoja na mengine alimwambia kuwa habari hizo akamwelezee msaidizi wake fulani ambae Ndugu Polepole hajamtaja.

Anasema pia palikuwepo dereva Taxi aliyekuwa akipewa bahasha na watu fulani aipeleke sehemu fulani. Siku moja dereva huyo alipewa bahasha ikiwa wazi/haijafungwa hivyo dereva alipata shauku ya kutaka kuona ni nini ambacho amekua akibebeshwa kwenye bahasha siku zote hizo. Ndipo alipofungua bahasha hiyo na kukuta list ya majina mengi ya watu/viongozi yakiwa yameandikwa kwa pamoja na codes zisizoeleweka, Anasema lilikuwemo jina la Rais wa awamu ya 5 na hata la kwake pia Polepole lilikuwepo!

Mwisho, Ndugu Polepole amemwambia muheshimiwa Rais wa sasa kuwa asiende kuchukua fomu kesho kwani kufanya hivyo itakuwa ni kuwatukana watanzania wote wanaoona mbali kuliko anavyoona yeye na hao waliomzunguka wanaomshinikiza kuchukua fomu na kuwania uRais.

Nimetafakari sana, wacha tuone!​

 
Back
Top Bottom