Tetesi: Polepole na Dkt. Hassan Abbas wanawatisha watu wa media

Jamani wanaJF, nimepenyezewa ubuyu hapa na source yangu moja hivi kwamba ktk matukio 2 ya chadema; mkutano mkuu na uchukuaji fomu kule Dodoma. Polepole na mwenzake Hassan Abbas wamekuwa wakivipigia vyombo vya habari simu ili kuvikataza kurusha hotuba za Lisu

Kuna audio ya Polepole nimesikilizishwa (japo source amegoma kuirusha kwambangu, hivyo sitoiweka hapa) na kuna namba ya simu ya Abbas na muda aliyopiga nimetajiwa.

Kama hii kitu ni kweli siyo uzushi, basi ni dhahiri shahili kwamba ccm na mawakala wao akina Abbas wana wasiwasi usio mithilika kiasi cha kukosa usingizi. Na hii inazidi kumpalilia njia Tundu Lisu

My take.
Kama Lisu ameshinda kifo cha risasi basi hata uchaguzi wa hila atashinda kwa kudra zake Mola. Amen!
Fake news
 
Wekeni ushahidi juu ya Polepole na Abbas kutishia wamiliki wa vyombo vya habari. Tena muweke audio clip authentic jinsi wanavyotishia. Vinginevyo ni uzandiki.

Mtu yoyote wa media atakayehudhubutu kuweka huo ushahidi ataenda alipo Azory. Hiyo ndio ujue ccm imepoteza ushawishi imebaki kutumia mabavu kukubalika.
 
Haya ni mambo ya kuhisi na wala huna ushahidi nalo.
Kwa hiyo wewe unaweza kutuonyesha alipo Azory? Maana unasema ataenda alipo Azory! Maana unafahamu alipo.
 
Majungu na Propaganda.
Haya tueleze wewe kwa nini chadema hawapewi airtime kwenye TV kama vyama vingine ,hawana pesa? au awataki,msitufanye mafala ccm wanamgwaya sana lisu na chadema huo ndio ukweli.
 
Jamani wanaJF, nimepenyezewa ubuyu hapa na source yangu moja hivi kwamba ktk matukio 2 ya chadema; mkutano mkuu na uchukuaji fomu kule Dodoma. Polepole na mwenzake Hassan Abbas wamekuwa wakivipigia vyombo vya habari simu ili kuvikataza kurusha hotuba za Lisu

Kuna audio ya Polepole nimesikilizishwa (japo source amegoma kuirusha kwambangu, hivyo sitoiweka hapa) na kuna namba ya simu ya Abbas na muda aliyopiga nimetajiwa.

Kama hii kitu ni kweli siyo uzushi, basi ni dhahiri shahili kwamba ccm na mawakala wao akina Abbas wana wasiwasi usio mithilika kiasi cha kukosa usingizi. Na hii inazidi kumpalilia njia Tundu Lisu

My take.
Kama Lisu ameshinda kifo cha risasi basi hata uchaguzi wa hila atashinda kwa kudra zake Mola. Amen!
Ndio uchahuzi huru na wahaki huo..
 
Sio propaganda ndg. Watumishi wa media wako ktk hali ngumu sana kwa sasa kutokana na mazingira wanayofanyia kazi. Kama huamini we angalia headlines za magazeti ya kila siku zinaongea nn.
Majungu na Propaganda.
 
Hao wamepigwa biti kali..

Kuna viongizi si muda mrefu wataishia jela..

Mabeberu wanatuangalia tuu kama vile simba anaangalia nyumbu wakigombana.

Beberu la Chato linasemajee kuhusu hii hali ??

pesa ndani ya kofia.jpeg
 
Ccm ingekuwa chama cha kiimla ungekuwa unatype huu uzushi? Office za Jf zingevamaiwa acha uzandiki wa kizamani.

Kwani ofisi za jf zikivamiwa unadhani details za watumiaji ziko kwenye daftari la mistari mikubwa na midogo? Taarifa zingekuwa kama kwenye daftari la mahudhurio ya ofisi ya serikali, leo hii wote tunaokosoa tungekuwa na kina ben saa8. Halafu ww unaonekana utakuwa mzee lazima, ndio maana mambo ya online unatolea approch za manually.
 
Media ziko kibiashara mnategemea mteremko, jinga kabisa.Kipindi cha uchaguzi ni cha kufanya biashara unategemea media zitumie mb zake kutangaza pumba za chadema. Zameni mfukoni mtaona media zitakuja kwenu

Unataka Chadema izame kama CCM kwenye haya mambo ??
 
Attachments

  • Rushwa CCM.mp4
    15.4 MB
Kwani ofisi za jf zikivamiwa unadhani details za watumiaji ziko kwenye daftari la mistari mikubwa na midogo? Taarifa zingekuwa kama kwenye daftari la mahudhurio ya ofisi ya serikali, leo hii wote tunaokosoa tungekuwa na kina ben saa8. Halafu ww unaonekana utakuwa mzee lazima, ndio maana mambo ya online unatolea approch za manually.
Mimi ni mzee kweli we dogo. Lakini hapo umebugi na umeonyesha uelewa mdogo. Mimi kusema ofisi za Jf kuvamiwa sijamaanisha ili kupata Id za users,bali kuivuruga kwa risasi kama zilivyvo nchi za kiimla.
Na kwa taarifa zako hata wewe IP adrdress yako inapatikan kiurahisi sana kupitia Tcra ndio maana wanakuacha upotoshe upuuzi tu.
 
Kwani mkiweka ushahidi halisi nani atabisha? Acheni upotoshaji kisa mnataka kick.

Kwanini tuende mbali, Paskali Mayalla si ni mwanahabari na member wa JF, muulize kipi kilimkuta mpaka akaporwa press card yake? Na hivi juzi alivyorudishiwa baada ya kunyooka, akawa anafurahi kama kuku kufunguliwa bandani? Wanachofanyiwa waandishi wa habari na media kwa ujumla mbona kiko wazi?
 
Kwanini tuende mbali, Paskali Mayalla si ni mwanahabari na member wa jf, muulize kipi kilimkuta mpaka akaporwa press card yake? Na hivi juzi alivyorudishiwa baada ya kunyooka, akawa anafurahi kama kuku kufunguliwa bandani? Wanachofanyiwa waandishi wa habari na media kwa ujumla mbona kiko wazi?
Ahaaaa. Lazima kuna maadili alikiuka maana mbona wengine hawanyag'anywi?
Mimi hoja yangu hapa ni kuwa Tanzania sio nchi ya kiimla. Ndio maana platforms kama JF zipo huru. Huyo Paschally kuna sehemu alibugi.
 
Jamani wanaJF, nimepenyezewa ubuyu hapa na source yangu moja hivi kwamba ktk matukio 2 ya chadema; mkutano mkuu na uchukuaji fomu kule Dodoma. Polepole na mwenzake Hassan Abbas wamekuwa wakivipigia vyombo vya habari simu ili kuvikataza kurusha hotuba za Lisu

Kuna audio ya Polepole nimesikilizishwa (japo source amegoma kuirusha kwambangu, hivyo sitoiweka hapa) na kuna namba ya simu ya Abbas na muda aliyopiga nimetajiwa.

Kama hii kitu ni kweli siyo uzushi, basi ni dhahiri shahili kwamba ccm na mawakala wao akina Abbas wana wasiwasi usio mithilika kiasi cha kukosa usingizi. Na hii inazidi kumpalilia njia Tundu Lisu

My take.
Kama Lisu ameshinda kifo cha risasi basi hata uchaguzi wa hila atashinda kwa kudra zake Mola. Amen!
Polepole na Abbas wote ni viazi hafifu vya mfalme juha
 
Ccm wanawakati mgumu kuliko hata 2015.. mtu mliyeona ana faa kuwapa ushindi hauziki.. miaka 5 amekuwa akiwa udhi wananchi kwa kauli zake za kebei na dharau..

Cha msingi ccm mjiandae kuiba kura nyingi zaidi ya zile mzilizo iba 2015.. mkizembea mkaiba kidogo Lissu atachukua nchi asubuhi.

Hakuna goli la mkono mara hii , Tukiwashika TUNAKATA MIKONO 😛 😛 😛 😛 😛 😛
 
Mimi ni mzee kweli we dogo. Lakini hapo umebugi na umeonyesha uelewa mdogo. Mimi kusema ofisi za Jf kuvamiwa sijamaanisha ili kupata Id za users,bali kuivuruga kwa risasi kama zilivyvo nchi za kiimla.
Na kwa taarifa zako hata wewe IP adrdress yako inapatikan kiurahisi sana kupitia Tcra ndio maana wanakuacha upotoshe upuuzi tu.

Kama TCRA wanapata ip address yangu, kipi kinawafanya walazimishe Melo awape taarifa za user aliyeleta taarifa za Oilcom? Kwanini wasifuate hiyo ip address ya huyo user, badala ya kumshitaki Melo ili kupata details za user? Kaa kimya maana huna ujualo.
 
Ahaaaa.Lazima kuna maadili alikiuka maana mbona wengine hawanyag'anywi?
Mimi hoja yangu hapa ni kuwa Tanzania sio nchi ya kiimla. Ndio maana platforms kama JF zipo huru. Huyo Paschally kuna sehemu alibugi.

Ile kesi ya kubambikizwa ya uongozi wa JF hujaisikia ??
 
Back
Top Bottom