Polepole na Musukuma tuacheni na machinga wenu nasi tupumue

Kwenye hili la wamachinga, hakuna unafki wowote, ni JPM ndie aliwaruhusu, hivyo wamachinga hawana kosa lolote. Waondolewe kistaarabu kwa utaratibu na kupangiwa maeneo mbadala na sio kuwavunjia usiku kama ile ya vingunguti.
P
 
Mwendazake kwa mdomo wake alisema hawa ni wapigakura wakE, nimeona niweke E kubwa unielewe, na mara nyingi amekuwa akirudiarudia neno hilo. Hata hivyo sheria za miji zipo kama sheria za barabara zilivyo, wapo waliopewa viwanja na baadae wanabomolewa jioni! Bila taarifa na hawa wapigakura wanabembelezwa!
 
Mimi ni kada wa CCM na ni strategic communicator na strategic thinker, hivyo sio kweli CCM haina watu hao, inao tena wengi tuu wa kutosha, tatizo ni...
naomba nisimalizie, mwacheni JPM apumzike kwa amani. Lets handle with care hii issue ya machinga.
p
 
Unakubaliana kwamba kila utawala na mipango yake? Mbona Rais na mawaziri wake wanapangua team ya rais wa nchi wa wakati huo then? Kwani kuna kwere P? Kila mtu afanye kazi yake na wajibu wake kwa nafasi na mamlaka yake.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Mi nakuekewa mkuu.
Siyo siri Magufuli hakuwa kada kinda kinda wa CCM.
Na tuseme wazi tu, ndio maana aliwa purge viongozi waandamizi wa CCM na kuwabeza viongozi waliopita ili kujenga CCM ya muelekeo wake.
Magufuli alidiriki kuwateua viongozi toka vyama vingine na kuacha wakereketwa wa chama, ali mradi wateuliwa toka vyama vingine wanaimba yale anayoyataka.
Mwalimu alianzisha msimamo wa Tujisahihishe katika chama, mwaka 1976/77 ili ku inculcate sense of rectifying political mistakes.
CCM isipoendesha ilani ya Tujisahihishe tutakuwa wanafiki.
Msimamo wa Machinga kwa chama ulikuwa na lengo la Magufuli kujipatia political base, nje ya chama.
 
Machinga kazi yake ni kutembeza bidhaa zake, lakini si kupanga sehemu na kuuza. Anayepanga sehemu moja huyo si machinga. Utaratibu na sheria zipo. Uchumi wa nchi hauwezi kuendeshwa na machinga, nchi haiwezi kuwa machinga. Hawa watu ni zao la serikali isiyowafikiria vijana kuhusu ajira, fursa na mazingira ya kujiajiri yamekuwa magumu. Viongozi wetu miaka nenda miaka rudi wanasema tu kujiajiri.
Suluhisho la machinga si kujenga machinga Complex.
Suluhisho la machinga si kuwapanga vizuri.
Suluhisho la machinga ni serikali kufungua milango ya ajira kila idara na kuwekeza kwenye sekta binafsi na mazingira mazuri na rahisi kwa wawekezaji. Kilimo peke yake kukiwa na soko la uhakika lita ajili asilimia 70 ya vijana, tuwe na macho kuangalia Soko kubwa kama China kwa mazao yetu.
 
He was a mistake !. Let bygone be bygone. Let him rest in eternal pièce.
P
 
Aliyewaruhusu machinga kufanya shughuli zao kiholela ni nani? tuanzie hapo kwanza......je, ni polepole na musukuma au ni siasa za kampeni za chama chakavu kulazimisha uungwaji mkono wa machinga kwa kuwatumia kama mtaji wa kisiasa......
Hao wawili wanatumia namna serikali inavyotatua tatizo la machinga kufikisha ujumbe kwa Makalla ambaye ni mfanyakazi anayelipwa mshahara na Mama Samia, hivyo wanampinga rais kupitia Makalla.
 
Kwanza mfahamu kuwa machinga hawezi jengewa eneo. Humo walipo ndiyo maeneo ya machinga. Waacheni wanyonge watafute mkate.
Waachwe wazibe mitaro ya maji taka,waachwe wapange bidhaa zao barabarani,wazibe milango ya wafanyabishara wengine tena wanaolipa kodi na wazibe njia za watembea kwa miguu pia wahodhi mabanda ya kukalia abiria stendi za mabasi!
 
Kwa Nini Hamza alienda kuua polisi, wakati angevaa nguo za CCM na kwenda kudili na viongozi hata 10
hahahahahaha we jamaa umenifurahisha Sana unajua umewaza nje ya box Sana?

Hiyo mbinu ilikua murua Kabisa
Unavaa zako sare za kijani unawatimbia kina Madelu piga Shaba!
 
Mimi naungana nao, they are very right.
P
Kwa mujibu wa sheria ipi ?

Kwa mujibu wa utu sawa kila mtu anahitaji kujipatia kipato cha kuweza kukidhi maisha yake..., ila solution si kuzagaa na kubangaiza bila security na kuhatarisha maisha yao na yetu...., bali ni kutengeneza sera ambazo zitafanya watu waishi kama wananchi na sio wakimbizi...

This is a time bomb and when it erupts there won't be any peaceful place for any of us to hide...
 
Paskali, jana Jumapili Musukuma alijitambulisha kuwa mmachinga wa Kariakoo kwa sauti yake mwenyewe alijitetea yeye na wamachinga wenzake kuwa wanafanya biashara kutafuta senti za kulisha familia zao, hii ilikuwa akihojiwa Wapo Radio.
 
Two wrongs does not make a right.., haifai yoyote apore mali ya yoyote..., kwenye kuvunja vibanda inabidi wapewe muda wa kutoka kistaarabu sasa swali linakuja wasipotoka inakuwaje waongezewe muda to infinity ?
na muwatafitie mahali karibu na masoko kufanya biashara,
Waliopo karibu na masoko walitafutiwa na nani ?, huenda na mimi ningependa niwe na duka mtaa wa Samora au pale mlimani City ila je Can I afford the place... Kumbuka kuna sehemu maeneo ni premium hence gharama tofauti, tusipoangalia value za sehemu zinaweza kushuka...
muwapange vizuri, wajengewe vibanda vizuri standard na uniform wafanye biashara zao rasmi na sio holela.
P
Kuwapanga vizuri na kuwajengea kila mtu angependa ila ujenzi huo ili uendelee kuwa mzuri na msafi una gharama na kuhitaji pesa (usafi, maitanance, rent na kodi kadha wa kadha) je hao wachuuzi watalipa hizo gharama au uwezo wanao..., sababu so called machinga ku-move sehemu na sehemu sio kwamba wanapenda ni uduni wa kipato, maisha yao ni ya kuokoteleza kwahio kama kweli tunawajali na kuwapenda tuhakikisha wanaondoka katika Umachinga..., majengo mengi ni matupu kwanini watu wasiingie huko ? (jibu ni kipato na mzunguko wa pesa ni mdogo) je machinga complex iliishia wapi ? Je ni kweli tunahitaji wachuuzi zaidi au wanahitaji kupungua kwa kwenda kwenye uzalishaji mwingine ?

 
Kama tatizo ni ccm hao machinga wanaishi Burundi ambako madhila yanayotokana na ccm hayafiki!? Nao sio victim kama wewe unavyojiona victim!?
 
Paskali, jana Jumapili Musukuma alijitambulisha kuwa mmachinga wa Kariakoo kwa sauti yake mwenyewe alijitetea yeye na wamachinga wenzake kuwa wanafanya biashara kutafuta senti za kulisha familia zao, hii ilikuwa akihojiwa Wapo Radio.
Polepole ni political oppurtunist.
Na kama yeye kweli ni machinga basi inabidi achukuliwe hatua za kisheria kwa kukwepa kodi, kukiuka sheria za biashara, kukiuka sheria za mipangomiji na usafi wa Jiji.

Imefika wakati tusiwachekee hawa wanasiasa uchwara.
 
Ni ngumu sana kwani huwa hawajihusishi moja kwa moja, wao huweka watumishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…