Polepole: Nilitegemea kuona kuna Mawaziri watajitokeza na kulaani ile kauli ya kula kwa urefu wa kamba

Polepole yupo tayari kupoteza maisha yake ili kukemea maovu
 
Ovyooo! Kuna Waziri aliyejitokeza kulaani Ile kauli ya VIETEEE???
Alikuwa anakula Kwa urefu WA kamba yake! Walimchunia!
 
Watalaani vipi kauli ya boss wao
 
Rais amebariki rasmi ufisadi serikalini. Mfano angalia jinsi askari wa usalama barabarani wanavyopokea rushwa hadharani bila uoga na takukuru wanapokea mishahara na kupandishwa vyeo
 
Mzee, hatujasahau tunaomba chenji ya ile pesa ya manunuzi ya wabunge na madiwani wa CDM.
 
Polepole tuambie nani alimpiga Lisu risasi haya mengine ni mambo yenu ya kihayawani tangu zamani
akikujibu hilo swali, rudi hapa na mrejesho. tumshukuru sana mama alienda hadi nairobi kumjulia hali pamoja na shinikizo na hofu zilizokuwa zimetawala kipindi kile, alienda, pamoja na kwamba lisu bado amemuona hana maana.
 
Aliwasema lini na wapi? Weka ushahidi hapa.
Kumbe hakuna aliyetaka kumuua?
Ndio maana nasema ni mnafki na muongo analichafua Taifa kujifanya mkimbizi kwa Amsterdam.
 
Watanzania kwa kupenda kupotosha kauli wanastahili PHD. Kula kwa urefu wa kamba ni kula kwa kutegemea mshahara wako wa halali, imepotoshwa kisiasa na huyu mnafiki nae kaingia mazima katika upotoshaji.
 
Anacho kisema Pole pole ni kweli hasa!!huwezi sema vile!!na majibu yenu ya kejeli kwake mtakuja ficha nyuso zenu!!muda si mrefu mtayapata na Pole pole atakuwa shujaa!!
Umekuwa nabii wa majanga, unayetegema kufeli badala ya kufanikiwa.
 
Polepole ni mwanasiasa wa ajabu sana asiyejitambua, asiyesoma alama za nyakati, aliyeko gizani na anaejaribu kupapasa akiwa pekupeku. Ni kama anatamani ndoto tamu iendelee bila kukubaliana na ukweli kwamba kumekucha. Sorry for him!
 
Umekuwa nabii wa majanga, unayetegema kufeli badala ya kufanikiwa.
Mbona we ni mkongwe kabisa jf?naamini umejiunga kabla yangu humu?ina Maana huoni hata kinachoendelea jamvini!!!??Huwa unasoma nyuzi zipi?? Pole pole ni mbwa anaebweka mwenye Mbwa yupo nyuma yake!!!!sasa kama una akili ungejiuliza Mwenye Mbwa ni nani?ni maiti iliozikwa chattle au ni nani hasa???!!!jitahidi kuwa na macho au hauli mboga za majani siku hizi??aiseh!!!acha niishie hapa!!
 
Watanzania kwa kupenda kupotosha kauli wanastahili PHD. Kula kwa urefu wa kamba ni kula kwa kutegemea mshahara wako wa halali, imepotoshwa kisiasa na huyu mnafiki nae kaingia mazima katika upotoshaji.

Wanasiasa wakati mwingine wanajipalia mkaa wao wenyewe; mtachoka tu kuwatetea! Sasa Rais anawaambia mawaziri wake, “…jipimieni…” What’s that nonsense?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…